Mimi ni manusra wa ajali ya noah iliyotokea tarehe 18 asubuhi maeneo ya dakawa MOROGORO na kuchukuwa maisha ya watu 10 kati ya 13.Nina maumivu kwenye paji la uso,mataya ya meno na mbavu.Watu wananishauri nifanye CT scan ili nijue nimepata athari kiasi gani mwilini mwangu.Sasa kwa hapa moro sielewi nitapata wapi huduma hii na kwa gharama zipi.
CT scan morogoro huwezi kupata
Lazima tuwe wakweli kwenye ukweli tusifarijiane uongo.. Nchi nzima hii hospitali zenye CT scan hazizidi 4.. Ambazo muhimbili japokuwa msomaji wasiwasi, Agakhan Dsm, hizo mbili nimekadiria tu but CT scan ni kipimo bei kali sana duniani, na mashine ya CT scan bei yake si mchezoooo si unakumbuka mgomo wa madaktari walisema hata muhimbili hakuna CT scan ndio serikali ikanunuaaa CT scan used...
So kuipata hospitali za moro ni ndoto ya mchana kweupeeee hiyo sio microscope iwepo kila hospitali, hata huko india na south africa CT scan ni kwenye Best Health Centres only...
Kwa nchi hii lazima uende Dar tu ndio utaipata,, hakuna hospital ya mkoa nje ya Dar yenye Ct scan,,
Mimi ni manusra wa ajali ya noah iliyotokea tarehe 18 asubuhi maeneo ya dakawa MOROGORO na kuchukuwa maisha ya watu 10 kati ya 13.Nina maumivu kwenye paji la uso,mataya ya meno na mbavu.Watu wananishauri nifanye CT scan ili nijue nimepata athari kiasi gani mwilini mwangu.Sasa kwa hapa moro sielewi nitapata wapi huduma hii na kwa gharama zipi.
pole sana Jaguar kwa maumivu ya ajali uliyoipata,sina uhakika kama morogoro kuna hospitali yenye CT Scan,nakushauri nenda dar muhimbili au Aga khan wanayo CT SCAN Watakuhudumia na ninakuombea upone haraka,Ila naomba kukujulisha mkuu MKATA KIU sio kweli kwamba kipimo cha CT scan hakipatikani nje ya dar,marehemu kaka yangu alifanyiwa CT SCAN KCMC MOSHI mwaka 2004 na pia nina uhakika Aga Khan Health centre Arusha wanayo CT SCAN.
CT scan ya kcmc imekufa siku nyingi..... about 4 yrs now na badoFuatilia mgomo wa madaktari mwaka jana, mojawapo ya sababu ni kukosekana kwa hiyo mashine nchi nzima zaidi ya agakhan Dar ndio serikali ikarekebisha muhimbili..
Na kuna daktari alisema CT scan ni bei ya VX moja tu la milion 200 alikuwa anaponda serikali kununua magari kuacha CT scan, raisi JK akamjibu mtu anaesema CT scan ni bei ya VX aende akapewe hela akainunue hiyo mashine kwa hiyo bei huyo DR akanywea..
Kuna vipimo kama CT scan na MRI vipimo ghali na vinavyohitaji utaalamu wa hali ya juu kusoma results zake ndio maana hospital ndogo ndogo zinashindwa ku afford,
Hiyo CT scan ya KCMC sina uhakika sana lakini sijawahi kusikia hospital ya mkoa nje ya Dar yenye hivyo vipimo, ila inawezekana ikawepo maana KCMC ni hospital kubwa