Wapi naweza kupata mkopo kuanzia elfu 10 mpaka elfu 50?

toplemon

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2017
Posts
4,612
Reaction score
4,721
Waungwana
Poleni na majukumu ya ujenzi wa taifa
nipo chuo bado still ni mwanafunzi wa ngazi ya stashahada naomba niende moja kwa moja kwenye mada

Jee naweza kupata mkopo wa kuanzia elfu 10 mpaka ellfu 50 online?
Jee ni tovuti gani wanazotoa mkopo online ukiondoa branch?Kinachonikwamisha branch ni kuwa sina kitambulisho cha mpiga kura nilikipoteza

Pamoja na kuwa ni mwanafunzi nataka nianzishe biashara ndogo ndogo hata ya kuuza ubuyu lengo ni kuweza kujimudu tu maana wengine tunasomeshwa kwa misaada ya watu wazazi wetu ndo bhasi tena uwezo wao duni

Najua kuna watu wanazielew sites ambazo naweza kupata mkopo online nitafurahi mno maana ndo kikwazo kwangu
Asanteni mno
 
Nakuombea ufanikiwe

Jr[emoji769]
 
Mkuu unatafuta lawama tu na MTU au Taasisi watakao kukukopesha..
Tz ya Leo laki1 ni kama elf 10 ya Tz ya wakati uleeeeee..!!!
Sasa unatafta mtaji ati wa buku10 au 50 !!!!!!!
Au labda unataka tu Pesa za matumizi kwa Siku mbili tatu

Sent from Calculator Phone vesion007
 
nimeishiwa full
 
Acha kujidanganya 10_50 thou hutaweza kuzifanyia kitu sanasana utakula msingi buuree usababishe lawama.
 
kama kweli ishu ni kukopa nakushauri ukope kwa washkaji unaosoma nao, hiyo hela ni ndogo sana utapata tu mtu wa kukuazima hapo.... Ilimradi uwe mwaminifu kwake
 
kama kweli ishu ni kukopa nakushauri ukope kwa washkaji unaosoma nao, hiyo hela ni ndogo sana utapata tu mtu wa kukuazima hapo.... Ilimradi uwe mwaminifu kwake
nataka online app ambayo nitakua nakopa nakurejesha halafu kadri navyilokopa ndo kiwango kinaongezeka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…