Wapi naweza pata mkopo kwa kutumia hati ya kiwanja?

Wapi naweza pata mkopo kwa kutumia hati ya kiwanja?

french

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2017
Posts
3,572
Reaction score
3,726
Habarini wakuu.

Nina hati ya kiwanja, ninashida ya mkopo kama mil 2-3. Wapi naweza pata mkopo kutumia hati nimejaribu benki kama 2 hivi nimekosa.
 
Subiri wanakuja wanaombaga mikopo watakusaidia mimi sijui
 
Nijuavyo hata Taasisi za kukopesha zikiwepo Benki hutaka kujiridhisha kama unachoenda kufanya kweli kuna matumaini ya kurejesha hiyo pesa.

Tofauti na hapo uangukie kwa Wajanja watakaokuwa interested na hicho kiwanja kuliko hata unachoenda kufanyia hizo pesa...hao hata ukiwaambia unataka pesa za kukeshea baa hawana shida...na masharti yao yatakuwa yanaelemea kwao.

Usiwasikilize sana Wanasiasa wanaohamasisha Majukwaani kuwa ukiwa na hati ya kiwanja basi unapata mkopo kwenye taasisi za kifedha..mambo sio rahisi hivyo.
 
Atumie kitambulisho cha machinga/ujasiriamali tu, si waliwahi kuambiwa vitakuwa na kazi hiyo pia? [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kiwanja kiuze tu. Ukizungusha hiyo pesa utanunua kingine.

Mikopo ya pesa haipatikani kiurahis rahis hata siku 1 kwa sababu una kiwanja
 
Aisee mimi natafuta mkopo kwa kutumia kadi ya gari niongeze mbegu za mifugo ktk ufugaji wangu niko Dar.
Kuna ka kampuni fulani nimekasahau jina, lake, wako Sinza Mori kwenye jengo lililopo mbele ya kituo cha mafuta. Wanakopesha ila kwa miezi mitatu

Kama unaona utaweza kurudisha ndani ya miezi mitatu nenda na gari yako waione.
 
Back
Top Bottom