Evans Richard Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 11, 2018
- 366
- 759
Husika na kichwa hapo juu, naomba kufahamu wapi nitapata connection kutoka kwa wachina viwandani au kuagizia china nipate kununua pikipiki kwao moja kwa moja bila kwenda madukani kwa bei ya rejareja au kwemda kwa mawakala wa mikoani au wilayani.
Nataka kufungua duka kwa ajili ya kuuza pikipiki aina ya sinoray, Fekon, Kinglion, TVS etc pamoja na vifaa vya pikipiki kwenye duka hilohilo.
Naomba kufahamu connection kwa mtu mzoefu wa hizi kazi au kwa yoyote mwenye uelewa wa pikipiki kutoka viwandani zikishafika Dar Es Salaam au Pwani kwenye Warehouses.
Nimejaribu kuulizia kwa wafanyabiashara wa pikipiki ila wanafanya kama siri ili wasiwe wengi kwenye biashara zao ila natamani niwe na duka langu binafsi la kuuza pikipiki au kununua pikipiki kwa bei ya jumla kutoka kiwandani na kutoa kwa vijana kwa MIKATABA.
Kama connection itahitaji kuwezeshana pia nitakuwa tayari kwa hilo.
Natanguliza shukrani kwenu.