Wapi nitapata mashine ndogo ya kuvunia mpunga?

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
12,001
Reaction score
27,175
Wakuu Salaam,

Kwa wanaojua ni wapi naweza kupata mashine ya kuvuna mpunga kwa hapa Tanzania kwa maana ya kununua au pia kuagiza nje ya nchi pamoja na bei yake?

Mashine ninayohitaji ni ndogo sio zile kubwa(Combine harvester),na itakuwa vizuri kama nitajua bei ya kwa maana ya iliyotumika au mpya.

Kwa yoyote mwenye ufahamu naomba anijulishe pia na uwezo wake wa kuvuna mpunga kwa saa.

Nimeambatanisha na picha kutoka mitandaoni ila zisikufunge kutoa ushauri.

Ahsante.

1686394704126.jpg
images.jpg
images%20(1).jpg
 
Kama uko dar es salaam nenda kisutu kule kuna maduka kibao unapata
 
Hiyo Kubota DC 60 ni combine sio mashine ndogo. Bei yake Ina range kati ya milioni 60 - 80. Hicho kimashine Cha chini usinunue utachezea mpunga tu. Kanafaa Kwa eneo dogo Sana na huvuna mpunga ukiwa haujakauka vizuri. Jikaze uchukue huo mtambo mkubwa bhaaas
 
Ikitokea umeamua kununua aina hii tafuta isiokuwa na mataili, yenye mataili inakwama sana kwenye tope, lkn ili uwe na mashine hii na ufanye kazi kwa uhuru ni vema ukawa na trekta kwanza maana hii mashine haina spidi huwa inabebwa kutoka shamba moja hadi jingine
 
Ni kweli lazima kuwa na trekta au gari la kuhamishia iwapo mashamba yapo mbali mbali hasa ya vibarua.
 
Hiyo Kubota DC 60 ni combine sio mashine ndogo. Bei yake Ina range kati ya milioni 60 - 80. Hicho kimashine Cha chini usinunue utachezea mpunga tu. Kanafaa Kwa eneo dogo Sana na huvuna mpunga ukiwa haujakauka vizuri. Jikaze uchukue huo mtambo mkubwa bhaaas
Asante kwa ushauri,hio milioni 60 ni bei ya mpya?kwa used ni bei gani kama unajua?

Na ina uwezo gani hio Kubota DC 60?
 
Ikitokea umeamua kununua aina hii tafuta isiokuwa na mataili, yenye mataili inakwama sana kwenye tope, lkn ili uwe na mashine hii na ufanye kazi kwa uhuru ni vema ukawa na trekta kwanza maana hii mashine haina spidi huwa inabebwa kutoka shamba moja hadi jingine
Unaposema aina hii unazungumzia ipi hasa,maana jamaa kataja mashine mbili hapo?
 
Sorry kwa kuingilia mada yako, je mashine ya kupandia mpunga inauzwaje kwa nwenye uelewa?
 
Mkuu mi nakupa hongera, hongera sana kwa kilimo.
kilimo unampa mtu hongera, aisee
mara mvua imekosekana, mara mafuriko shamba limeenda na maji
vibarua wanataka hela nyingi
hatari sana
nalima ya chakula tu siyo kibiashara
 
Wakuu Salaam,

Kwa wanaojua ni wapi naweza kupata mashine ya kuvuna mpunga kwa hapa Tanzania kwa maana ya kununua au pia kuagiza nje ya nchi pamoja na bei yake?

Mashine ninayohitaji ni ndogo sio zile kubwa(Combine harvester),na itakuwa vizuri kama nitajua bei ya kwa maana ya iliyotumika au mpya.

Kwa yoyote mwenye ufahamu naomba anijulishe pia na uwezo wake wa kuvuna mpunga kwa saa.

Nimeambatanisha na picha kutoka mitandaoni ila zisikufunge kutoa ushauri.

Ahsante.

View attachment 2652560View attachment 2652562View attachment 2652563
 
Back
Top Bottom