Wapi nitapata mkopo kwa kuweka dhamana ya nyumba?

Siwezi kuuza,maana ilipo ndio na Mimi nakaa nyumba ya uwani. Nauzaje sasa? Nina shida tu na hiyo pesa
Ungeweka wazi hio shida watu wangekupata ufumbuzi,Ili usiipoteza nyumba hio maana pesa ya mkopo huwa ni tamu,kulipa chungu.
 
Wewe mtu akikukopesha akili hana kwa maelezo uliyotoa hiyo pesa hutarudisha

Vyanzo vya uhakika vya Mapato ni ajira ya kueleweka na biashara

Wewe hivyo vyote viwili huna hiyo.pesa ya kurudisha marejesho utatoa wapi ?
 
Mimi nataka Mkopo wa Tshs 30 Million naweza lipa kwa Miaka 2 dhamana ni Nyumba ipo Dar ina thamani ya Tshs 200 na zaidi ipo sehemu zuri sana sema haina Hati ina Karatasi za Serikali ya mtaa… Nisaidieni…. Kama naweza pata sehemu mkopo Bank nimefiatilia mpk nimechoka…
 
Watu mnahitaji sana elimu kuhusu mikopo. Huna ajira wala biashara kwanini ukope? Mkopo wa kuanzishia biashara ni risk kubwa na wengi wameishia kupoteza mali zao.
 
MORTGAGE COMPANY SIFAHAMU KWA NINI HAZIPO TANZANIA, ULAYA ZIPO, WAKITATHMINI MJENGO WAKO, UNAPATA FEDHA FASTA WITHIN 24HRS, BANK HUWA NI MATATIZO MATUPU,MLOLONGO WAKE SIO WA KITOTO, KIBAYA LAZIMA UTOE RUSHWA KWA MAAFISA MIKOPO, NA SIKU YA KUWA KUKUDAI HUWA HAO HAO NDIO WANYAMA NAMBARI MOJA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…