Wapi nitapata mkopo wa haraka na masharti nafuu?

Mabrek

Senior Member
Joined
Sep 17, 2013
Posts
125
Reaction score
21
helo great thinkers ninaombeni kwa mwenye ufahamu juu ya mikopo isiwe bank kwani lengo langu,ni kukopa fedha kidogo ili niongezee mtaji katika biashara yangu nipo tukuyu mbeya,kaz yangu ni mwalimu karibu,kwa ushauri ndugu zangu
 
Kama shs ngapi? Kuna watu binafsi wanakopesha lkn uwe na kitu cha kuweka dhamana, ila uwe makini kwenye urejeshaji usipitishe tarehe mliyokubaliana kwani hutakuta hiyo mali uliyowekeza!
 
kama laki saba tu naongezea kwa mtaji tu kaka hebu nipe mwongozo
 
Aisee,
Haya,sijui kwanini Mwalim anakwepa Bank wakati ndio sehem salama kwake.

siwez kukopa bank pesa kidogo namna hyo wakati wangu ukifka ntakopa,bank chamsingi ni kupanga malengo na kuyatimiza kwa wakati sahihi kama unavojua watu hawapangi kushindwa ila wanashindwa kupanga
 
mnaambiwa mjiunge vicoba hamtaki...unaona sasa...
ndio hapo sasa,halafu anasema pesa ndogo,sasa mbona hana pa kuipata.
Wakati kukopa hakuangalii ni Bank au wapi,we mtu binafsi atakukopesha kwa riba si chini ya 30%,sasa hapo si zaidi ya Bank?
Siku hizi hakuna mtu anatoa pesa kirahisi,na kama ni mtu binafsi basi jiandae dhamana yako kuuzwa,maana kuna kamchezo kao ka kulizana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…