Wapi nitapata nguo nzuri za mitumba kwa Mwanza

T 2021 SSH

Member
Joined
Apr 26, 2021
Posts
20
Reaction score
42
Natafuta chimbo zuri la kupata mzigo mzuri wa nguo za mtumba grade one kwa Mwanza ni wapi naweza pata, nataka nifanye biashara ya nguo na mtaji wangu ni kidogo siwezi kununua belo lakini pia naogopa kupata lonya ipo 250k

Naomba msaada kwa wajuzi?


 
Fanya utafiti pale Makoroboi na Mlango mmoja utafahamu wanapotolea japo wao wananunua kwa belo kisha wanauza reja reja.

NB: Sijajua ile mitumba ya pale ni grade ngapi
 
Nguo za wadada jumatatu na alhamis wanafungua Belo makoroboi gauni grade one Bei ni 7000 Hadi 10000 na sketi wengi wanauza 5000 kwa siku wanayofungua ila hata ukienda siku zingine(kasoro jmosi na jpili) utapata nguo nzuri kwa Bei ya kawaida sketi 3000 na gauni 4000 Hadi 5000.

Mlango mmoja sijawahi kwenda ila niliambiwa jumatatu asubuhi Sana saa 12 uwe umefika utakuta wengi tu Wanakata Belo siku hiyo za nguo zote watoto,wakubwa, mashuka na pochi kwa kuanzia nakushauri Anzia na mlango mmoja kwanza kuna option nyingi.
 
Wewe pia upo Mwanza mkuu!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…