Habari wana JF mimi naishi mkoani Dodoma nimejiingiza katika biashara ya ufugaji kuku wa nyama. Shida yangu natafuta vifaranga wa kuku wa nyama wa kununua kwani nimekuwa nikiagiza kwa wafanya biashara wa hapa mkoani lakini changamoto yake ni oda inakaa hadi mwezi sijaletewa nikifatilia adithi za sungura na fisi azihishi. Na lengo langu ilikuwa kila baada ya wiki 1 au 2 naingiza bach, sasa bach yangu ya kwanza ina wiki 6 hiyo ya pili mpaka leo sioni hata daliki za kuipata! Nimejaribu kufanya mawasiliano na baadhi ya wadau humu jf wanaodai wanauza vifaranga lakini sioni kama wako kibiashara zaidi, unauliza jinsi tutakavyofanya biashara anakujibu shortcut kama vile ana nia. Naomba msahada wenu wana jf wapi nitapata vifaranga wazuri na kwa bei nzuri na kwa muda muafaka ili niendeleze biashara yangu.