Wapi pazuri kuwekeza hisa, bond au fixed deposit au UTT?

Hyo imetokana na nini? Na kuna siku za nyuma hapo zilipanda mnoo
Wanasema kushuka na kupanda inategemea na soko la hisa,coz hizi fedha za mfuko wa bond fund nao UTT wanazipeleka kwenye masoko ya hisa
 
Wanasema kushuka na kupanda inategemea na soko la hisa,coz hizi fedha za mfuko wa bond fund nao UTT wanazipeleka kwenye masoko ya hisa
Mfuko wa Bond, makusanyo yake hayapelekwi kwenye hisa mkuu. Tofaut na mifuko mingine ambayo makusanyo yake huenda kuwekezwa kwenye hisa...hyo ni kwa maelezo yao.

Mfuko wa bond, makusanyo yake hupelekwa ama huwekezwa kwenye mapato ya kudumu ikiwemo dhamana za serikali na Account za riba kwenye mabenki.

Ila najua ni kwa nini unasema hisa zimeshuka,..kama ni mgeni naweza kukuelekeza especially mwanzoni mwa kila mwezi pesa huwa inapungua,, lakini vipande huongezeka..
 
Mkuu hebu nipe elimu zaidi coz bado ni mgeni huko UTT nimeanza June mwaka huu
 
Ok,labda nkuulize Account yako ya UTT uliomba uwe unapata gawio na kuingizwa kwenye account yako ya benk ama unakuza mtaji bila kuchukua Faida??
Mimi nakuza Mtaji bila kuchukua faida, Account nimefungua tatu
Liquid
Bond
Umoja
 
BOT ni kuzuri ila bond zinauzwa madalali kwa mdada. Ina ugumu kupata. Gawio lake inakaribia 1.6M per month kama utawekeza kuanzia miaka 20. Na unaweza kopa 80% ya kiasi ulichoweka na ukatumia kiasi hicho kununua hatifungani zingine. After 5 yrs unaweza kuwa na uwekezaji wa 180M gawio likiongezeka na kuwa more than 2.5 per month. Ila unalipwa kwa Instalment ya miezi sita. Kwa vyovyote vile zile 20b za Simba More alipeleka huku na ana enjoy gawio la more than 4B per yr wakati akisubiri mchakato. ukamilike.

UTT unapata gawio la 1% per month which means utakuwa ukipata 1M per month.. na uzuri wa huku unaweza kuwithdraw kiwango fulani pale unapopata matatizo kwa kutoa taarifa. UTT hawana mlolongo mwingi kama Bank ya nchi.

Huko kwingine sijui
 
Mimi nakuza Mtaji bila kuchukua faida, Account nimefungua tatu
Liquid
Bond
Umoja
Ok,kila mwanzoni mwa mwezi kwa yule mwenye option ya kukuza mtaji..huwa wanatoa amount fulani kutoka kwenye mtaji,,na wana update idadi ya vipande...baada ya kama siku mbili hivi utakuta ile amount iliyo ondolewa kununua vipande imerejea pale pale.

Mwanzoni nilipata pia mawazo lakini nilieleweshwa baada ya kuwapigia simu.
 
Shukrani sana mkuu, na hii ni kwa kila mfuko wa UTT au Mfuko wa Bond tuu
 
Shekheee, hizi ofisi za brokers waliosajiliwa na DSE. Sio vishoka kama nyie. Fanya kazi na brokers wenye leseni, sio vishoka janja janja
Sasa kwa nini umpeleke mafichoni badala ya kuongelea hapa hapa ili na wengine wanufaike? Ndiyo maana wanasema mmeanza utapeli!
 
Mkuu, nicheki kwenye WhatsApp 0788893364 nikupe ushauri professional. Niko kwenye kampuni ya securities ambayo ndio broker wa hizo vitu
Huu utapeli sasa, kwanini akupigie simu? Kama hutaki kutoa huo ushauri hapa, umefuata nini humu?
 
Mimi nina bond pekee, huwa nina experience hivyo. Sina account za mifuko mingine. Na pia kila mwanzoni mwa mwezi bei huwa inaanzia chini halafu mwisho wa mwezi inakuwa juu. Graph huwa inaenda hivyo
Unaweza kushare experience yako kipi kilikuvutia ukaamua kufungua Bond na sio mfuko mwingine? Inaonekana umepata elimu na maelezo ya kutosha kutoka kwa wahusika sio vibaya ukatuambukuza elimu hiyo wengine hapa
 
Mkuu, nicheki kwenye WhatsApp 0788893364 nikupe ushauri professional. Niko kwenye kampuni ya securities ambayo ndio broker wa hizo vitu
Kwanini iwe whatsapp? Huwezi weka hapa tukafaidika kwa pamoja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…