Wapi twende kipindi hiki cha sikukuu

Wapi twende kipindi hiki cha sikukuu

ZINDAGI

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2015
Posts
1,118
Reaction score
1,430
Ngoja tuondoe stress za Corona kidogo, kwa hii ndoto.

Iwapo utapewa nafasi ya kuchagua pa kwenda kipindi hiki utoke ulipo na familia yako kwa muda wa miezi kama sita hivi na utalipiqa gharama zote, wapi utachagua pa kwenda? Kumbuka safari inaanza siku chache tiu zijazo.

Mimi ningechagua kwenda visiwa vya Kiribati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi kuhusu kazi kama umeajiriwa? mi naona bosi bora ukomae hapo hapo hizo hela ukafanyia mambo mengine.

Umesikia watu wa Dar wameanza kukimbilia shamba? bora tukajichimbie huko, kazi tutaangalia hali itakapokua shwari.
 
Umesikia watu wa Dar wameanza kukimbilia shamba? bora tukajichimbie huko, kazi tutaangalia hali itakapokua shwari.
Sawa, lakini vipi kama nyie wa Dar mkaupeleka huko shamba, mi niko shamba na huku pia kuna tetesi tetesi kuna mjinga mmoja katoroka karantini (sio yule wa Iringa) wamemkamata baada ya siku kadhaa, kwa hiyo kila mtu atulie tu kwake ili tuzuie kuusambaza zaidi.
 
Off course tutachukua hatua muhimu, halafu tukifika huko tutajiweka quarantine kwa muda wa siku 14 ndio tutoke tujichanganye na wanakijiji wenzetu
 
Back
Top Bottom