Nina mshikaji wangu ambaye aliondokewa na mke wake kiasi cha miaka minne iliyopita. Anatambua umuhimu wa kupima virusi ili kuishi kwa matumaini ila tatizo ni kwamba hataki kupima hospitali bali anataka kujipima mwenyewe. Je kuna sehemu vinauzwa/vinapatikana vifaa hivi?
mi naona labda aende Mabala aeleze ukweli halafu wamuelekeze anaweza kujipima mwenyewe.
Njia ambayo ni sahihi ni kupata kwanza pretesting counseling na hata baada ya kupimwa, post counselling hii itakusaidia kuyapokea matokeo hata kama hayatakuwa mazuri. Nakushuri nenda kwenye VCT (voluntary couselling and testing) yeyote iliyo karibu, maana VCT ni entry point ya care and treatment ili kama maethirika ataingia kwenye mpango wa taifa wa dawa ART, hizi short cut si nzuri kabisa ndugu yangu, nenda waone Angaza ama AMREF wanaconsellors wazuri sana wala hutakiwi kuwa na hofu kuogopa matokeo, tumaini la kuishi bado lipo, acha njia za mkato si nzuri
Masa
Nina mshikaji wangu ambaye aliondokewa na mke wake kiasi cha miaka minne iliyopita. Anatambua umuhimu wa kupima virusi ili kuishi kwa matumaini ila tatizo ni kwamba hataki kupima hospitali bali anataka kujipima mwenyewe.
Je kuna sehemu vinauzwa/vinapatikana vifaa hivi?