Wapi zinakouzwa t-shirt mpya kwa gharama nafuu hapa tanzania?

LULAMSO

Member
Joined
Apr 26, 2013
Posts
56
Reaction score
9
Wadau naomba msaada wenu tafadhali. Nahitaji sana T-SHIRTS mpya zisizo na maandishi yoyote popote za aina tofauti, rangi tofauti, zenye kola na zisizo na kola, za mikono mifupi na mirefu. Nazihitaji sana kwaajili ya kikundi chetu cha ujasiliamali.
NB: Zisiwe zile zinazotanuka shingo mara tu baada ya kufuliwa kama zilivyo nyingi mtaani.
Ukinisaidia mawasiliano ya simu ya wahusika utakuwa umenisaidia sana.
 
nenda kariakoo, mtaa wa nyamwezi karibu na njia ya kuingia shimoni au mtaa wa mchikichi.. kuna maduka hapo
 
Nashukuru sana mkuuu. Mzigo uko wapi na bei zake zikoje kwa wastan?
 
nenda kariakoo, mtaa wa nyamwezi karibu na njia ya kuingia shimoni au mtaa wa mchikichi.. kuna maduka hapo

Ahsante sana kwa maelekezo mkuu nitafanyia kazi mapema iwezekanavyo! Vp huna mawasiliano ya wauzaji wakubwa wenye bei nzuri kwa maisha ya kitanzania?
 
Nashukuru sana mkuu. Huo mzigo uko wapi na bei zake zikoje kwa wastani?

bei inaenda na gram za t shirt na quantity ulikuwa unataka ngapi, round neck au polo?? nikupe quotation,
 
15000 bei ya jumla, made in vietnam piga 0713110771
 
bei inaenda na gram za t shirt na quantity ulikuwa unataka ngapi, round neck au polo?? nikupe quotation,

unaposema polo unamaanisha nn? Ni zile zenye kola?
NB: Kuhusu bei toa tu mchanganuo wake ulivyo hii itatoa frursa hata kwa wengine wenye uhitaji kama mm. Mchanganuo utakaonipa utanipa base nichukue zp kulingana na uwezo wa mfuko.
 
Ninahitaji tshirt aina ya manga plain, nitapata kwa shiling ngapi wadau... zinahitajika zaid ya mia
 
Ninahitaji tshirt aina ya manga plain, nitapata kwa shiling ngapi wadau... zinahitajika zaid ya mia
Unapatikana wapi mkuu..!! Me Niko dar naweza kukusaidia sina duka ila naweza kukusaidia bei ni elfu 7500- 8000 bei ya jumla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…