Mshobaa
JF-Expert Member
- Apr 7, 2013
- 1,714
- 677
Wapiga Debe katika Stendi ya Daladala ya Mbezi Luis wamekuwa kero kubwa kutokana na yale wanayoyafanya kila siku kutuoni hapo kwa nia ya kutafuta Abiria wanaoelekea katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli Bus Terminal.
Kwanza Daladala ikiwa inaingia hasa majira ya asubuhi ambapo kuna mpishano wa watu wengi kituoni hapo, wao wanadandia magari yanapoingia kituoni na kuyakimbiza, jambo linahatarisha usalama wao na watumiaji wengine wa stendi.
Daladala ikisimama wanaanza kuwasumbua abiria wanaoshuka na hata wale wanaotaka kupanda kwenye usafiri huo, wakiona kuna Abiria anayeelekea Stendi Kuu ya Magufuli ndio kabisaa kero inazidi
Wanaanza kuwavutavuta Abiria wenye mizigo, wanajidai wanawasindikiza na kutaka kubeba mizigo yao bila ridhaa ya Abiria na wapo wanaotumia nafasi hiyo kufanya vitendo vya wizi.
Kuna matukio kadhaa yametokea ya wizi hasa wakati wa msongamano wa Abiria wanaoshuka na wanaoingia kwenye daladala huku Wapiga Debe hao wakiwa ni kati yao kwenye kundi hilo
Mamlaka zinazohusika na kituo hicho zinapaswa kufanya jambo kwa kulishughulikia suala hili kwa kina ili kudhibiti watu hawa, kwani baadhi yao hujichomeka kwa lengo la kusaidia abiria kumbe ni vibaka na wengine wana malengo mabaya zaidi.