Bastian360
New Member
- Feb 6, 2023
- 1
- 0
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya watanzania kudharau mambo muhimu na ya kimsingi hasa yanayofanywa na watanzania wenzetu wazalendo, jambo linalopeleka kulikwamisha Taifa letu kwenye kupiga hatua za kimaendeleo.
Tabia hii imekuwa ni ya kudumu na imeendelea kukua kwa miaka na miaka hali inayopelekea kuwapoteza na kuwakatisha tamaa watanzania wenye uwezo na nia ya dhati ya kufanya mambo mbalimbali kwa weledi na ari katika kuhakikisha wanapeleka maendeleo ya Taifa letu mbele.
Tabia hii ya wapiga dili, kanjanja, watu wenye kuweka maslahi yao mbele kujijali wao kuliko Taifa imekuwa inadhorotesha mipango ya kimaendeleo na hatimaye kuharibu kabisa mambo mazuri yaliyopangwa kufanywa ndani ya Taifa na watanzania hawa wenye nia thabiti ya kuboresha na kuimarisha maisha ya watanzania.
Mfano mzuri ni ndani ya Shirika la Umeme nchini Tanzania (TANESCO) ambapo hivi karibuni kumekua na mapinduzi na maboresho makubwa sana ya kihuduma na ya kiuwekezaji yanayofanywa na shirika hilo chini ya Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti yake.
Licha ya changamoto zote za Shirika hilo tunazozifahamu kwa miaka na miaka ambazo bila shaka Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti wamekutana nazo lakini wamejitahidi sana kwa kipindi kifupi katika kuhakikisha wanafanya mabadiliko kwenye maeneo mengi ya kimuundo na hatimaye matokeo yameanza kuonekana.
Tangu kuingia kwa bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti mpya ya TANESCO, uwezo wa uelewa wao juu ya kupambana na changamoto na kutoa majibu umeonekana wazi wazi hasa katika utekelezaji wa mipango.
Miradi mingi na mikubwa ya uzalishaji umeme nchini imetekelezwa huku miradi mingine ikiongezeka kasi maradufu ndani ya muda mfupi.
TANESCO kwenda kidigitali katika mfumo wa kuomba kuunganishwa na umeme kupitia Application ya Nikonekt, TANESCO kupata hati safi kwenye ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG na kuboresha hali ya uchapaji kazi kwa wafanyakazi na watendaji wa Shirika hilo ni baadhi ya vitu vichache vinavyofafanua wazi wazi upambanaji wa Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya shirika hilo, wamekuwa watu wawazi na wenye kuweka kila kitu hadharani na mara zote wamekuwa tayari kukutana na watu wa aina zote na kujibu changamoto zao na hata kutoa maelezo pale wanapohitajika.
Mabadiliko haya yamesababisha kuzibwa kwa mirija ya wizi na upendeleo iliyokuwa imesimikwa huko nyuma na wapiga dili, jambo linalowafanya kuingizwa kwenye orodha mkakati ya kuvurugiwa mipango yao ndani ya Shirika na watu hao walioweka maslahi yao mbele.
Haitakuwa sawa hata sekunde moja kuwakalia kimya watu hawa kwani watataka kuvuruga kila jambo ili mradi mipango yao miovu iendelee na tukiwa tunafahamu wazi hakuna chochote wanachojali kwenye Taifa hili zaidi ya maslahi yao.
Watanzania kuendelea kupata maendeleo makubwa kwao siyo kipaumbele kama matumbo yao, watu hawa wanajulikana, wapigwe vita na waache tabia hiyo mara moja kwani muda muafaka ukifika majina yao yatawekwa hadharani.