Wapiga kelele kuadhibiwa Kenya

Wapiga kelele kuadhibiwa Kenya

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2008
Posts
2,268
Reaction score
335
Wapiga kelele kuadhibiwa Kenya

Sheria mpya inayoazimia kudhibiti kiwango kikubwa cha kelele nchini Kenya ilipitishwa Jumapili.

Serikali inasema amri hiyo itawaathiri wale wanaohusika na matendo yanayosababisha kelele nyingi.

Wanaolengwa ni pamoja na wahubiri, wachuuzi na mashirika yanayotumia vipaza sauti.

Mkurugenzi wa taasisi ya mazingira nchini Kenya, Dk Muusya Mwinzi, anasema polisi watahakikisha kwamba wanaovunja sheria hiyo watakamatwa na kushtakiwa.

Watatozwa faini ya mpaka dola 5000, au kifungo cha miezi 18.

Source:BBC


Maoni yangu: Walianza Rwanda,sasa Kenya. Je nyumbani ni lini?
 
Back
Top Bottom