Wapigeni wanaokaidi/kiuka sheria halali, alisema Pinda wiki iliyopita. Tuitafakari kauli ya Pinda kisheria.
1. Kwanza, sheria mama inasema watu wote wako sawa mbele ya sheria na wanalindwa na sheria: Ibara 13(1) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (kama ilivyorekebishwa 2005). Na ili kuhakikisha usawa mbele ya sheria, mamlaka ya nchi itahakikisha inaweka utaratibu unaozingatia haya yafuatayo kama ilivyoainishwa katika ibara ndogo ya 6(a-e), ambayo ni:
(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kingenecho kinachohusika;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa l a jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo;
(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo chohote ambacho alipokitenda hakikuwa ni kosa chini ya sheria, na pia kwamba ni marufuku kwa adhabu kutolewa ambayo ni kubwa kuliko adhabu iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendwa;
(d) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu, heshima ya mtu itatunzwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi na uendeshaji wa mambo ya jinai na katika shughuli nyinginezo ambazo mtu anakuwa chini ya ulinzi bila uhuru, au katika kuhakikisha utekelezaji wa adhabu;
(e) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.
2. Sasa hii ya Pinda ya "piga tu... na mimi nasema pigeni..." ameitoa wapi?
3. Nani anayetafsiri kuwa kitu fulani kikitendeka ni kukaidi amri halali: ni polisi au mahakama? Ninavyojua ni kwamba raia au polisi wakihisi kuna uhalifu unatendeka wana wajibu wa kumkamata wanayemhisi na kumpeleka mahakamani ambako ndiko kesi yake itakapoamriwa na ama kuachiwa huru au kupewa adhabu.
4. Kama kila wanachofanya/tenda polisi ni halali, mbona wakienda mahakamani huwa pia wanabwagwa chini? Zipo kesi nyingi ambazo wamekuwa wakishindwa kwa sababu ya kutokuwa na ushahidi au ushahidi hafifu au wenyewe tu kutojua sheria husika.
5. Je, kwa yeyote atayepigwa vibaya, tafsiri haitakuwa kwamba ni kutekeleza kauli ya Pinda (serikali) ya kuvunja sheria?
6. Serikali lazima ioneshe mfano mzuri ili raia waweze kujifunza na kufuata: Je, kwa kauli hii ya Pinda haitazidisha pia uhalifu wa kujichukulia sheria mkononi miongoni mwa raia kwa kuiga/kujifunza wanachokifanya polisi cha "kupiga tu" wakihisi mtu amekaidi amri yao? Maana sidhani kwama polisi kuwaambiwa raia wasijichukulie sheria mkononi (kutoa kipigo au kuua wakihisi mtu fulani ni mhalifu) itafanya kazi kama polisi wenyewe wana uhalali wa kufanya hivyo. Hili fundisho ni gumu kulichukua. Naomba tujadili.