Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Ukiangalia trend za majadiliano mitandaoni utaona dhahiri watanzania wameingia ubaridi toka jana ilipotoka taarifa ya Dr Abbas kukanganya na kufuatiwa na ya Msigwa kufafanua vyombo vipi vya habari vifunguliwe._
Jambo lililovurugika zaidi Waziri mwenye dhamana alipoomba wamiliki wa magazeti wafike wizarani waone vifungu vikivyotumika kuwafungia--Hii iliongeza ubaridi na ganzi kuwa Wizara yenyewe ni kama haijui vifungu vipi vilitumika.
Mbaya zaidi ni kuonekana Magazeti yenye uchafu mwingi na matusi yaitwayo Tanzanites, Fahari na The Observer yakiendelea kutamba bila hata maonyo.
Habari hiyo iliendelezwa na habari mbaya ikionyesha mteule wa Rais DC wa Hai akiendesha operations za uvamizi na utesaji wa raia, wafanyabiashara,wanasiasa wa upinzani hadi wengine kujeruhiwa vibaya na kukatwa viungo vya mwilini.Video nyingine ilionyesha RC wa Kilimanjaro akikemea matendo hayo mkutanoni lakini DC husika akionekana kumtazama RC kwa jicho la dharau kama vile kutokubaliana na alichoambiwa.
Ganzi na ubaridi vimeongezeka leo baada ya ripoti ya CAG kusomwa Bungeni na kuamsha hisia kali kwa wananchi baada ya kujua ni kiasi gani walikuwa wanapigwa fedha za umma na kuhadaiwa katika serikali waliyoaminishwa ni salama na kuwa ina nidhamu na uadilifu kwa watumishi wake.
Haya ni madoa meusi katika kitambaa cheupe! Furaha ya mapokeo ya hotuba ya Mh Raisi siku ya Jumanne wakati wa uapisho wa Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi za umma imeingia dosari.
Yetu macho na masikio kuona uongozi mpya utayakabili vipi haya madoa ili furaha na matumaini ya Watanzania yarejee. Inaweza kuwa ni mapema kupiga vigelegele iwapo dosari hizi zitafumbiwa macho