Uchaguzi 2020 Wapinzani fanyeni kampeni za kisayansi Oktoba, 2020, tambueni CCM ni Constant namba

Uchaguzi 2020 Wapinzani fanyeni kampeni za kisayansi Oktoba, 2020, tambueni CCM ni Constant namba

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,291
Mada inahusika.

Wapinzani wanalazimika kufanya kampeni za kisayansi sana. Tayari CCM ina mtaji wa NEC, ZEC, Polisi, Wasiri wetu na makada kadhaa.

Mfumo wa nchi unawapendelea zaidi wao na ule uharibifu uliofanywa wa kutumiwa makada kuajiriwa kwenye sehemu nyeti.

Makada hao si watiifu wa sheria na katiba ya nchi yetu bali kwa CCM. Hilo liko wazi.

Wapinzani tambueni hizi code.

X + Y = CCM

Tambueni hata mshinde maeneo mengi ya ubunge, uwakilishi, udiwani na hata Urais bado CCM ina nyenzo na mbinu za kushinda.

Mbinu hiyo kwa jina lengine ni " JECHA STYLE"

Fikirieni mbinu za kisayansi Kuiondowa CCM kwenye "Constant" namba.

Sayansi haijawahi kufeli na hutumika kupata majawabu ya hesabu ngumu na kutatuwa matatizo sugu.

Njoni na " Formula" ya kuondowa "Constant" namba yaani CCM kwenye hii hesabu.

Tunawatakia Prepo njema.

Kishada
 
Kabla ya kuwashauri kuja na mbinu za kisayansi ungeanza kuwashauri kuacha mihemuko ya kisiasa kwanza.
Sayansi haiwezi pelekwa kwa mihemuko ya kisiasa kamwe.

Mfano Mzuri Ni yule jamaa ambae ashaanza kuishambulia NEC juu ya mchakato wa mwisho angali hata haijamaliza mchakato wake wa mwanzo wa kuwagawia fomu Wagombea.
Huu Ni mhemuko Tena mbaya Sana.
 
Pengine ndio wameanza "ku - apply" hio sayansi, kunyamaza kwao wakati wanajua kinachoendelea ni kufanya makosa. TUMEWASHAURI WASIACHE MWANYA.
 
Back
Top Bottom