Hii ni mbiu ya mgambo kwa upande wa Upinzani, msilegeze kamba katika kuhakikisha madai ya tume huru na iliyobora inapatikana sambamba na Katiba mpya, hayo ya CCM ya kutumbuana kuhamishana, kusifiana kukandiana hayo ni yao na yawachwe kama yao.
Leo mnasema au inasemwa ndani ya CCM kuna wanaosabotaji, wanaokandia na mambo mengi ya kufanya kuonekanwe kama kuna mvutano ndani ya CCM, Kuna mambo ya kitaifa zaidi ambayo yasiachwe kupigiwa kelele hata kama yanaenda vizuri, huo ndio siasa za upinzani.
Inawezekana wengi waliondani ya upinzani haswa ya kisiasa hawaelewi vizuri nembo ya upinzani katika duru za kisiasa, niseme tu ni sumu kwa chama cha upinzani kuisifu serikali ya chama inayoongoza nchi ni mwiko. Unatakiwa uponde hata Rais anavyotembea labda iweke kionjo.
Rais anatembea kwa kujilabu na kutanua mikono yote ni kuonyesha dharau, mmeona hivyo ndivyo inavyotakiwa, kuna waziri anaitwa sijui Jafo amefanya sijui madudu gani, amewajaza wazinifu waliokubuhu katika skendo mbalimbali eti ndio wawe maraisi wa maendelea kisa tu wana followers wengi katika account zao za social media nahisi hicho ndio kigezo. Hapo pekee upinzani wangevalia barakoa na njuga wakapiga makelele ya kila rangi alimuradi Jafo ajute alichokifanya.
Msiingizwe choo cha kike CCM .sisi wananchi tunaijua inatumia mambo mengi kuwapumbaza wapinzani lakini siku za uchaguzi zinapokaribia wote huwa pamoja katika kuhakikisha wanaikandamiza haki na cha haramu kukifanya kwao kuwa halali, mnajua yaliyotokea uchaguzi mkuu uliopita.
Kuweni macho na hila zao hakikisheni msiwape nafasi CCM kufurukuta mnawabana kwa mwendo mdundo mpaka kieleweke, msiiwache serikali ika-relax ni hatari kwenu watawauwa na kuwazima kirahisi na mbaki mkiita vyombo vya habari.