Amani Msumari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,830
- 972
Wanabodi,
Historia ni somo la muhimu sana kwani linatuonesha ni wapi tulipotoka, tulipo na kutuwezesha kupanga na kutabiri kesho yetu.
Wakoloni walipokuja Afrika hawakuja moja kwa moja. Walikuja kwa hatua, kwa kuwatanguliza wamishionari, wapelelezi na wafanyabiashara. Hawa walipeleleza tabia zetu, utamaduni wetu, uimara na udhaifu wetu. Walipoweka mambo sawa, wakatuvamia.
Katika uvamizi mpaka utawala, wakoloni walishirikiana na waafrika wenzetu. Hata sasa, hatujasahau mateso, dhiki, unyanyasaji, dharau na madhila waliyotufanyia achilia mbali unyonyaji wa rasilimali walioufanya. Kwa taarifa tuu, hata kutupa uhuru ilikuwa ni mbinu ili wasitumie tena nguvu bali akili katika kututawala.
Ukoloni mamboleo ndio unaoutumika kuidumaza Afrika. Leo hii haishangazi kumuona kiongozi mkubwa wa kisiasa akijinasibu kwa kuongea kiingereza fasaha. Tupo kwenye vita ya uchumi na wakubwa wanataka Afrika iendelee kuwa soko na mzalishaji wa rasilimali kwa viwanda vya viranja wa dunia.
Kwa mantiki hiyo, wakubwa hao watafanya kila namna ili tusiendelee maana kuendelea kwetu ni hatari kwa ustawi wa uchumi wao. Angalia kilichowapata marehemu Gaddafi na Mugabe. Libya na Zimbabwe zilikuwa nchi bora kabisa Afrika ila viongozi walipoingilia maslahi ya wakubwa "wakakiona chamtemakuni". Wenyewe hawana adui au rafiki wa kudumu Bali wana maslahi ya kudumu.
Mabeberu ni wajanja sana, hawaingilii nchi yoyote bila kupata vibaraka wao ndani ya nchi husika. Kwa bahati mbaya, sehemu nyingi wametumika "wapinzani uchwara". Sehemu yoyote ambapo wananchi wanakuwa na umoja, basi nchi hizo haziingiliki.
Niwaombe sana watanzania wenzangu kuwa makini sana kipindi hiki cha Uchaguzi kwani ndio msimu wenyewe wa kutumika. Kampeni ziende kwa amani, umoja, staha na ustaarabu.
Amani Msumari
Tanga (kwasasa Arusha kwa kazi maalumu)