Wapinzani ni dhaifu mno katika Bunge la Katiba!

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Wapimzani wanaburuzwa na mwenyekiti wa Bunge pamoja na wana-CCM kwasababu wameonyesha udhaifu mkubwa!Kila siku mnaburuzwa na nyie mpo tu bila kuchukua hatua zozote.

Nawaonya msipobadilika na kuwa na msimamo thabiti, mtaburuzwa kila siku na mwisho wa siku itapatikana katiba ya CCM alafu muanze kulialia na kuitisha maandamano.

Ni bora mkajitoa sasa katika mchakato huo haramu kuliko kuja kulaumu baadae wakati na nyinyi mmeshiriki.
 
Mimi natofautiana na wewe kwa hili !

Udhaifu au uimara wa upinzani ni matokeo, sio katika kupigana au kuleta fujo !

Sasa hivi hakuna kanunu zozote zinazotumika hivyo ni busara ya Mwenyekiti tu ndio inayotumika. Unapoonewa katika mazingira hayo, unachoweza kufanya ni kueleza ukweli kwamba unaonewa hapo hapo Bungeni na unaweza kufanya hivyo hata nje ya Bunge unapopata nafasi...Wapinzani wamekuwa wakifanya hivyo.....Zaidi ya hapo labda wasusie na sioni namna nyingine labda uiseme wewe. Na wakisusia utungaji wa kanuni kwa sababu hiyo watakuwa ni wapuuzi wa hali ya juu...

Wapinzani walikuwa wanataka vitu viwili vikubwa katika kanunu hizi na ambavyo CCM wamevipinga kwa nguvu zote !.

1.Moja walitaka hoja zao ziwekwe bayana na wao waweze kuzitetea hizo hoja zao. Katika hili, ingawa report yao haitakuwa separate, imeamuliwa kwamba itakuwa sehemu ya report kuu na wao watapata nafasi kwa kumchagua mtu mmoja ambaye atazitolea ufafanuzi...Kwa hili wamefanikiwa sana, ninawapa kama 90% kwenye hili ! CCM walichofanikiwa hapa ni kuiunganisha report yao na report kubwa lakini wameshindwa kuiondoa report yao na kuzuia mtu wa upinzani kutetea hoja zao, hapa nawapa CCM 10%

2. Jambo la pili ni kura ya siri au kura ya wazi. Kitendo kwamba CCM pamoja na wingi wao, wameshindwa kupitisha kura ya wazi mpaka sasa hivi inaonyesha jinsi gani wapinzani walivyo imara ! Ilifika mahali mpaka CCM wakakubali hii kura ya siri ila wakageuzwa na machozi ya mmoja wa wabunge wao !. Na leo wameamua rasimu ya kanuni ipitishwe bila kusema kura gani itapigwa (wazi au siri) ili kamati ya mashauriano iendelee kufanya kazi !. Na siamini kama watawashinda wapinzani kwa hili !

Nadhani utakubaliana na mimi hizo ndio hoja mbili ambazo zimeleta kutofautiana kwa kiwango kikubwa kati wa CCM na wapinzani kwenye rasimu ya kanuni.

Ya kwanza wapinzani wameshinda, ya pili ngoma bado mbichi na wanaelekea kushinda vile vile.....Hivi unawezaje kuwaita waliopata mafanikio kama haya wadhaifu ?

Hawa ni majasiri na wajenga hoja wazuri sana, kwani pamoja na uchache wao wamefanikiwa kupata mafanikio makubwa kama ambavyo nimeeleza hapo juu....


 
Huko mbeleni ndio utakuja kuamini ninayosema.
 
Naunga mkono wazo lako kwa asilimia mia moja
 

Salary Slip, wewe kama mtanganyika au mzanzibar umefanya nini nje ya bunge maalumu kushinikiza yale unayoona hayaendi vizuri mjengoni! Katiba ya nchi ni yetu wote. Katiba sio ya ccm wala vyama vya upinzani! Katiba sio ya wanasiasa wala wanaharakati ni yetu sote. Ikishindikana jua tumekosa wote. Wako wapi wasomi ya nchi hii wapinge wazi wazi madudu yanayotokea hadharani ndani ya bunge maalumu. Nchi hii kama tumelaani!
 
Hii ni moja ya thread ambayo kila mchangiaji ana point. Kasoro mimi.
 
Km maantiki yako kuburuzwa ni ile ile zomea zomea inayofanywa na ccm,hapo kweli upinzani wanaburuzwa! Lkn kwa maana ya hoja nzito mpaka sasa bunge bado limedhibitiwa na upinzani. Ule mgawanyiko unaosikika upo ndani ya ccm na si upinzani. Upinzani wameweza kupenyeza nguvu yao hadi ndani ya ccm. Lkn wameweza kuwateka hata wateule wa rais kwa kiwango kikubwa.
 
Ni kwamba, sifikiri sana kama hata inabidi kusema upinzani unaburuzwa, utakuwa hufikirii vema. Nafikiri unatakiwa kulia na hoja zinazopitishwa zinamsaidia mtanzania huyu na ajae. Ukizungumza hivyo da, Napata taabu sana. Tuangalie hoja zina maslahi kwa Taifa ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…