Pre GE2025 Wapinzani ogopeni wanachama walionunuliwa bila kuchukuliwa

Pre GE2025 Wapinzani ogopeni wanachama walionunuliwa bila kuchukuliwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Wapo wanachama ndani ya vyama vya siasa wanaoshikilia misimamo ya kupinga agenda zitakazokiimarisha chama. Ndani ya vyama wamo wanachama ambao wamenunuliwa bila kuchukuliwa. Unaweza kumnunua mbuzi wako halafu ukamuacha palepale kwa mfugaji kwa muda au milele aendelee kuzaa kutokana na sababu zako maalum.

Akina Nassari na Msigwa ni mfano wa watu walionunuliwa na kuchukuliwa na mnunuzi, lakini wako wengine wengi tu ambao wamenunuliwa lakini wakabakizwa humohumo ndani ya chama kwa kazi maalumu kama hizo. Wako ndani kupinga na kuchochea kila kitu kitakachoonekana kukiimarisha chama. Na watu hawa walionunuliwa bila kuchukuliwa ni hatari sana kwa chama kuliko wale waliochukuliwa na mnunuzi.

Kuweni macho, tizamaneni usoni mtawagundua tu. Dalili kuu za watu hawa ni:

1. Wanapinga reconciliations (kusameheana)- jino kwa jino.
2. Wanapinga negotiations (majadiliano)
3. Wanavujisha siri za vikao/chama
4. Wanajifanya bila wao chama hakiendi, wakati mwingine wanajitolea (fedha) kufanikisha vikao, ofisi, stationery, chakula/vinywaji kutoka mifukoni mwao (pesa za master wake anazolipwa)
5. Lazima awe na cheo kitakachomuwezesha kushiriki mipango na siri za chama.

Kuweni macho.
 
Back
Top Bottom