Ili waweze kuondoa CCM Madarakani.
Mstahiki:
Waanze na vitu mhimu vya msingi kabisa katika kuleta mabadiliko.
Kwa mfano: Kama kuna mambo yanayowawezesha CCM kuendelea kuwa katika utawala ni mhimu kabisa wapinzani wayaangalie kwa makini kabisa na waanze kampeni kubwa ya kuyaondosha. Kama mambo hayo yamo katika katiba, basi katiba ifanyiwe marekebisho au ibadilishwe kabisa kama inalazimu.
Wapinzani waache kuendelea kuwalaumu tu wananchi kwa kutowachagua wao. Ni mhimu wajiulize, ni kwa nini wao hawachaguliwi. Kuna mambo mengi sana sasa hivi yanayofanywa na CCM ambayo hayawapendezi wananchi, na wengine hawayajui. Ni jukumu la vyama vya upinzani kuwafikishia wananchi mambo hayo.
Bahati waliyo nayo wapinzani wa Kenya, kwa Tanzania hiyo bahati haipo katika baadhi ya mambo hayo. Kwa mfano: Ukabila na kuwa na kabila moja linaloonekana kufaidi zaidi ya mengine. Kama isingekuwa kujiunga kwa Raila, Mudavadi, Ruto, Balala, Nyaga na Ngilu, na kuyategemea makabila yao kuwaunga mkono, ODM isingeweza kuwa na nguvu inazozionyesha hadi sasa.
Tusisahau pia kuwa KANU, hakikuwa chama kilichokuwa kinatetea haki za mwananchi wa kawaida, kama ilivyokuwa CCM kabla hakijawa chama cha mafisadi. Kwa hiyo wakenya wengi walikuwa wanakiona chama cha kanu kama cha kionevu; tofauti kabisa na CCM ya hapo zamani, iliyokuwa inaonekana kupigania haki ya mwananchi wa kawaida. WaTanzania walizoea hivyo kwa muda mrefu, inahitaji pia muda kuwafumbua macho kuwa CCM ya Kawawa ni tofauti kabisa na CCM ya Makamba.
Mwananchi wa Kenya amezoea mfumo wa kuonewa/kunyanyaswa kwa muda mrefu. Anapoona nafasi hii ya upinzani kujikomboa, ni lazima akubali.
Wapinzani wa Tanzania ni lazima wawe na subira na wafanye juhudi zaidi; na hasa sasa kwa kutumia mfano huu wa mabadiliko huko Kenya kuwavutia wananchi.