expirience man
JF-Expert Member
- Nov 16, 2013
- 214
- 104
Kama inavyofahamika kuwa uchaguzi ni mchakato wenye hatua mbalimbali na huitimishwa na upigaji wa kura na utangazaji wa matokeo.
Inafahamika pia aina ya tume ya uchaguzi tuliyonayo haiko on favor ya wapiga kura ambao ndio wananchi, tume ipo kwa ajili ya kuhakikisha CCM inabakia madarakani.
Hili limejionesha wazi zaidi mwaka huu pengine kuliko chaguzi zilizopita na kuufanya uchaguzi wa mwaka huu kuwa tofauti sana na chaguzi zilizopita.
Tumeona matendo ya NEC kupitia kwa mkurugenzi wake Dkt. Wilson Mahera ni ya kutilia mashaka sana.
Pia matendo ya vyombo vya usalama wakiongozwa na polisi yanatia shaka sana.
Pamekuwepo na matamko toka NEC na jeshi la Polisi kuelekea kwa upande mmoja tu wa wapinzani kwa aina ya matendo yanatofanywa na wagombea wa vyama vyote lakini wanakemea upande mmoja tu.
Usiku wa Jana zipo taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuvamiwa kwa ngome za wagombea wa ubunge mkoa wa Mara na Arusha na watu wanaodaiwa kuwa ni Jeshi la Polisi. Inaripotiwa kuwa vifaa mbalimbali vya kampeni za wagombea hao. Mambo hayo hapo juu yananisukuma kuandika taadhari zinazopaswa kuchukuliwa na wapinzani kulinda ngome zao na vituo vya kijumlisha matokeo Kila Jimbo.
1. Waweke vituo vyao kwa siri kubwa sana na viwe zaidi ya kimoja kwenye Jimbo.
2. Kuandaa vituo hewa ili kupoteza maboya.
3. Nyakati Kama hizi waweke vijana kwenye kambi za siri kwa ajili ya kazi hiyo ya ujumlishaji matokeo yao na ikibidi wasitoke hata nje wiki mbili kabla ya uchaguzi mpaka kutangazwa kwa matokeo. Hii itasaidia kupunguza mamluki wa kuchomekewa. Kuteuwa mawakala wanaoaminika kuwawezesha pia kuwa na timu itakayoratibu kuhakikisha kila wakala anaapishwa na anaingia kwenye kituo, asipoingia kituo husika muhakikishe hakuna upigaji kura hapo unafanyika by any means necessary.
4. Ku-rise awareness ya jamii kuwa tayari ikiwa hujuma zitafanyika, hili linapaswa kusisitizwa na kila mgombea katika Kila ngazi ili kuweka msisitizo wa kauli ya Mbowe na Lissu kuhusu hujuma za uchaguzi.
Kuhitimisha hili nisisitize tu huu uchaguzi wapinzani wakitembea na nguvu ya umma watafanikiwa zaidi.