Pre GE2025 Wapinzani wataishinda CCM 2025 endapo yatafanyika yafuatayo

Pre GE2025 Wapinzani wataishinda CCM 2025 endapo yatafanyika yafuatayo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
Kuishinda CCM ,sio jambo dogo sababu kwanza wameshikilia dola , wana wanachama watiifu wengi ,na pesa pia .lakini wakifanya yafuatayo kwa katiba hii wanaweza shinda :-

1.Wawa hamasishe na kuwahimiza wananchi kupiga kura ,Wana CCM kwenye mitaa wanajuana na hupitiana kuhakikisha wanapiga kura .

2.Kuwatoa hofu wananchi kwamba kura haibadili matokea , kura yako inaongeza idadi na inazuia wizi , kituoni mkijiandisha 200 watu 100 wakapiga kura ni Rahisi kura 50 kuongezwa wao na kura 15 zikapewa Upinzani.

3.Kusimamisha wagombea wenye ushawishi sio watu wenye nguvu chamani , vyama vitoke vitafute watu wanaokubalika katika jamii husika .

4.Mawakala wawe wenye misimamo na motivated , wakala apewe fungu na ajue kituo chake akishinda atapata fungu lipi la ziada .

5.Vyama vifanye mabadiliko ya uongozi, kwa sasa hakuna Mwenyekiti wa Chama ambae yuko pale kwa ajili ya chama zaidi ya CCM na Maslahi tubadilike mapema kabla ya 2025 .
 
Hapa ndio umemaliza Kiongozi?

Ngoja nami nijazilizie

1. Chama kianzishe RUNINGA na RADIO yake, ndani or hata nje ya nchi hasa hizi nchi jirani kama Kenya kwa ajili ya kuibua ufisadi ,changamoto na kutoa njia mbadala ya kutatua changamoto hizo bila kusahau kueneza SERA na ITIKADI za Chama

2. Ipigwe movement ya nguvu ya KUDAI KATIBA MPYA NA ILIYO BORA pamoja na TUME HURU NA SHIRIKISHI YA UCHAGUZI .Chama kipeleke vijana kujifunza mbinu zaidi ya kufanikisha haya. Kuna mengi ya kujifunza nchi jirani ya Msumbiji na hata Kenya hasa kipindi cha Hayati MOI

3.Iendeshwe kampeni kali nje ya nchi hasa haya Mataifa yanayotufadhili bajeti zetu za Maendeleo,ili waelewe kwamba hakuna demokrasia ya kweli nchini. Kusanyani EVIDENCES za KUTOSHA na kuziwasilisha kwa wafadhili. Njia hii aliitumia sana Hayati Maalim seif na Mh Lissu kuonyesha dunia ufedhuli wa Serikali hii ya CCM

4.Elimu ya Uraia izidi kutolewa hasa vijijini

5.Kuwe na mikakakti ya kutafuta vyanzo endelevu vya FEDHA,na hizi kanda ziongezewe nguvu

6. Mikutano ya hadhara ya kutosha bila kusahau maandamano ya kupingika mambo yote yasiyofaaa
N.B
Kuiondoa CCM sio kazi rahisi,kwa kuwa wanajua siku wakitolewa madarakani basi wengi wao watafikishwa Mahakamani kwa UFISADI
 
Hapa ndio umemaliza Kiongozi?
Ngoja nami nijazilizie

1. Chama kianzishe RUNINGA na RADIO yake, ndani or hata nje ya nchi hasa hizi nchi jirani kama Kenya kwa ajili ya kuibua ufisadi ,changamoto na kutoa njia mbadala ya kutatua changamoto hizo bila kusahau kueneza SERA na ITIKADI za Chama

2. Ipigwe movement ya nguvu ya KUDAI KATIBA MPYA NA ILIYO BORA pamoja na TUME HURU NA SHIRIKISHI UCHAGUZI .Chama kipeleke vijana kujifunza mbinu zaidi ya kufanikisha haya. Kuna mengi ya kujifunza nchi jirani ya Msumbiji na hata Kenya hasa kipindi cha Hayati MOI

3.Iendeshwe kampeni kali nje ya nchi hasa haya Mataifa yanayotufadhili bajeji zetu za Maendeleo,i li waelewe kwamba hakuna demokrasia ya kweli nchi. Kusanyani EVIDENCES za KUTOSHA na kuziwasilisha kwa wafadhili. Njia hii aliitumia sana Hayati Maalim seif na Mh Lissu kuonyesha duna ufedhuli wa Serikali hii ya CCM

4.Elimu ya Uraia izidi kutolewa hasa vijijini

5.Kuwe na mikakakti ya kutafuta vyanzo endelevu vya FEDHA,na hizi kanda ziongezewe nguvu

6. Mikutano ya hadhara ya kutosha bila kusahau maandamano ya kupingika mambo yote yasiyofaaa
N.B
Kuiondoa CCM sio kazi rahisi,kwa kuwa wanajua siku wakitolewa madarakani basi wengi wao watafikishwa Mahakamani kwa UFISADI
Uko sahihi
 
Back
Top Bottom