Mambo ya Walawi 20:27Hakuna uchawi naishi kwetu miaka kibao ,nimesoma mpaka nimepata kazi hapa Sijaonw huo ujinga.
Wewe bado hujarogwa, ukirogwa ndo utajua uchawi upo au haupoHiyo ni imani ya hovyo ,hakuna anayeweza kukurudisha nyuma ...Hakuna ndugu Yako anayekuroga ..
Ukishaanza kuamini hayo mambo basi unakuwa kama zombie.
Kwa hiyo nguvu ni za kuroga watu waliofanikiwa na sio kuwapita kimafanikio?Wewe bado hujarogwa, ukirogwa ndo utajua uchawi upo au haupo
Uchawi ni sanaa ,Rudi ukasome ...Vitabu vya kichawi vipo kibao hata wazungu wanatumia.Mambo ya Walawi 20:27
[27]Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.
A man also or woman that hath a familiar spirit, or that is a wizard, shall surely be put to death: they shall stone them with stones: their blood shall be upon them.
Mtoa mada katoa mifano ya watu walioanza kufanya maendeleo huko kwao wote walirogwa wakafaKwa hiyo nguvu ni za kuroga watu walioganikiwa na sio kuwapita kimafanikio?
Havijawakuta hao mkuu lazima watabisha.Hujui kitu , tulia.
Uchawi huwezi kuushinda kwa kutokuamini kuwa upo
Si kweli😅😅😅...Nauliza huo uchawi una nguvu ya kurudisha watu nyuma tu ila sio mafanikio.Mtoa mada katoa mifano ya watu walioanza kufanya maendeleo huko kwao wote walirogwa wakafa
Hizo ni hadithi tu za kufikirikaMambo ya Walawi 20:27
[27]Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.
A man also or woman that hath a familiar spirit, or that is a wizard, shall surely be put to death: they shall stone them with stones: their blood shall be upon them.
Hakuna uchawi naishi Tanga tangu miaka ya 90's ,stori zenu ni za kutunga 😅😅.
Uchawi ni sanaa ya kiini macho ila haiko serious mpaka kuua mtu.
Ili kutoboa katika jamii za Watanzania usisahu kuzingatia jadi. Nafikiri imeeleweka. Kuna watu ni komesha, wamefuata jadi wapo maofisi makubwa yenye hela, hata uweke sumu kwenye chakula hali na anashtukia. Hao ndio wanadumu katika ulimwengu huu!Sijafanya utafiti wa kutosha kuhusu mikoa mingine, lakini karibu nimetembea mikoa yote ya Tanganyika. Hali zinafanana—utofauti ni mdogo sana.
Turudi mkoani kwangu, Lindi. Kule, ndugu wa damu kabisa ndiye mchawi wako namba moja. Ni kama Yesu alivyosema: "Adui wa mtu ni wa nyumbani mwake".
Nakumbuka mwaka fulani huko Kilwa Kipatimwa, watoto wengi wa shule ya msingi walifaulu na kwenda sekondari. Miaka hiyo, ukienda sekondari ilikuwa kama umeenda Ulaya. Wanafunzi wa kidato cha nne walifaulu, wa kidato cha sita pia wakafaulu—karibu wote wakaenda UDSM wakitokea shule tofauti.
Miaka hiyo, kazi za kuokota ziliwaleta wote katika ajira nzuri, wakaanza kujenga vijijini kwao. Thubutu! Ndoto zao zilikatishwa ghafla—misiba tu ndiyo iliyotawala. Kwa muda mfupi, wote walifariki kwa hali za kushangaza. Mchezo ukaisha hapo.
Mfano mwingine:
Jamaa mmoja aliyekuwa polisi Dar es Salaam kwa miaka mingi hakuwa anarudi likizo. Mwaka mmoja akakopa pesa na kuamua kujenga nyumbani kwao. Nyumba ilipokamilika, akaja likizo ili afaidi matunda ya kazi yake. Siku ya kwanza tu, asubuhi wakaamka wakimuita—hakuamka. Alikuwa tayari maiti.
Hata ndugu wa damu hawaachi. Brother wangu, ambaye tumezaliwa baba mmoja na mama mmoja, alikuwa na ramani nzuri sana ya maisha. Sasa hivi amechoka kama mzee, ilhali ana miaka 46 tu. Sasa anajichomea mkaa ili apate mkate wa kila siku. Amepigwa na kitu kizito kisichoeleweka, hata akilima hekari tano, mavuno yake hayazidi debe moja au mbili.
Mimi mwenyewe niliwahi kufungua duka la bidhaa mchanganyiko, nikawekeza mamilioni. Lakini cha kushangaza, mauzo kwa siku yalikuwa shilingi elfu 20, elfu 30, mara chache elfu 40. Watanzania wana wivu na uchawi mwingi sana. Kama hujui namna ya kuwakabili, hutafanikiwa hata uwe na juhudi na ubunifu kiasi gani.
Nimeona watu wakiacha kazi nzuri bila sababu za maana baada ya kurogwa.
Watu wana wivu mwingi sana—wanaokuchekea mdomoni, moyoni hawamaanishi hivyo.