Waraka kwa tume ya mabadiliko ya katiba: Mabaraza ya katiba ya wilaya yawe hivi!

Waraka kwa tume ya mabadiliko ya katiba: Mabaraza ya katiba ya wilaya yawe hivi!

Mhoja

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2010
Posts
207
Reaction score
24
MABARAZA YA KATIBA YA WILAYA YAWE HIVI
Tume ya mabadiliko ya katiba imetoa mwongozo wa jinsi ya uundwaji wa mabaraza ya katiba ya wilaya. Mie sina shida sana na uendeshaji wake, bali nina matatizo kuhusu muundo na utaratibu wa kuwapata wajumbe watakaounda mabaraza hayo.

Kwa mujibu wa Tume ya marekebisho ya katiba, mabaraza hayo yataundwa na wajumbe wa aina mbili, wajumbe wanne kutoka kila kata ambao watachaguliwa na kamati za maendeleo za kata (WDCs) kutoka miongoni mwa wajumbe waliochaguliwa na wananchi kutoka kila mtaa au kijiji pamoja na madiwani wa kuchaguliwa, viti maalumu au wa kuteuliwa na waziri ambao wapo katika kata husika.
Ningependa niungane na mwandishi wa makala wa gazeti la Tanzania Daima Jumatano Ndugu George Maziku katika makala yake ya tarehe 27/02/2013 iliyokuwa na kichwa cha habari "MWONGOZO MABARAZA YA KATIBA UNA KASORO KUBWA" mwandishi huyu amejitahidi sana kuelezea mapungufu yaliyomo kwenye mwongozo huo.

Kwa kuanzia na muundo wake, naona una matatizo makubwa, tatizo kubwa lipo kwa kulazimisha madiwani kuwa wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya kwa kutumia nyadhifa zao, jambo hili halikubaliki kabisa kwanza kwa kuzingatia sifa za watakaokuwa wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya kama yalivyoainishwa katika kifungu namba 4.0 vifungu vidogo namba 4.5 na 4.6

Tukianza na kifungu namba 4.5 ambacho kinasema, "Awe ni mtu mwenye hekima, busara, na uadilifu" Katika sifa za kumchagua mtu kuwa diwani hiyo sifa haipo, kwa kuwaingiza madiwani kuingia moja kwa moja kwenye mabaraza hayo ni kasoro kubwa, kwa sababu siyo kila diwani ana hekima, busara na uadilifu, anaweza kipindi alipochaguliwa kuwa diwani mwaka 2010 alikuwa na busara, lakini mpaka kufikia leo ameshapungukiwa busara, na kwa kuzingatia sheria zetu hata kama wananchi wataona diwani wao hana hekima, busara na uadilifu hawana jinsi ya kumtoa tofauti na kusubiri uchaguzi mkuu kwa ajili ya kumtoa, kwa hiyo wataingia watu kwenye mabaraza ya katiba ya wilaya ambao hawana busara, hekima na uadilifu. Napendekeza muda bado upo unaruhusu kubadilisha mwongozo huo na kuwataka madiwani nao wagombee kwenye mikutano ya mitaa au vijiji kwenye nafasi za kila mitaa na baadaye nafasi kwa kila kata badala ya kuingia moja kwa moja.

Katika kifungu namba 4.6 ambacho kinasema, "Awe ni mtu mwenye uwezo wa kujieleza na kupambanua mambo" Siyo kila diwani ana uwezo wa kujieleza na kupambanua mambo na hasa mambo yanahusu katiba, kuna mwingine anauwezo wa kupambanua mambo ya mpira au bongo movie, utakapomleta huku kwenye kupambanua mambo na hasa yanayohusu mambo ya msingi kama katiba ya nchi atashiriki tu kama ni msindikizaji na siyo mshiriki mchangiaji. Kwa hiyo kwenye eneo hili bado diwani hana nafasi ya kushiriki moja kwa moja kwenye mabaraza hayo, kwa mfano unakuta diwani, kipindi cha mchakato wapambe wake wanenda kumchukulia fomu, wanamjazia, wanarubuni watu wengine waliochukua fomu ndani ya chama chake wajitoe, pamoja na kurubuni watu wengine ambao watakuwa wamechukua fomu kwa ajili ya kugombea udiwani kwenye kata husika kupitia vyama vingine wajitoe ili kutoa nafasi kwa mtu wao kuwa mgombea pekee na ambaye kwa kwa mujibu wa sheria zetu anakuwa amepita bila kupingwa, je huyu uwezo wake wa kupambanua mambo utajulikana vipi? Kwa sababu mtu akipita bila kupingwa hata kampeni hafanyi. Kwa wanasheria kuna msemo unaitwa (to test the validity of the witness).

Jambo jingine linaonyesha ubaguzi katika hiki kifungu, unaposema huyo mtu awe na uwezo wa kujieleza, lazima ufafanue, kuna ndugu zetu hawana uwezo wa kuongea vizuri, mabubu, wasiosikia, wasioona nk, ambao huwa wanahitaji usaidizi wa ziada ili ujumbe uweze kuifikia jamii husika, naona kwa mwongozo huu watakuwa wameachwa nje, mi naona sifa hii inahitaji marekebisho au ufafanuzi ili tusiwatenge wenzetu wenye ulemavu ambao utawasababishia wasiweze kuchaguliwa kuingia kwenye mabaraza hayo.

Tatizo la pili kwenye mwongozo wa Tume ya marekebisho ya katiba ni namna ya kuwapata wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya. Hatua ya kwanza ya kuwapata wajumbe kwa ngazi ya kijiji au mtaa haina tatizo kubwa, tatizo lipo jinsi ya kupata wajumbe kwa ngazi ya kata, utaratibu wa kutumia wajumbe wa kamati za maendeleo za kata kuchagua wajumbe wataoingia baraza la katiba la wilaya haukubaliki, hili litakuwa ni baraza la katiba la wilaya kuwa la kiitikadi zaidi kuliko kuwa la kijamii zaidi, tutajikuta makada wa vyama vya siasa ndiyo wameteka mabaraza ya katiba ya wilaya badala ya wananchi. Tutafanya baada ya uchaguzi wa wajumbe kwa ngazi ya mitaa au vijiji watu waanze kufanya kampeni ya kuchaguliwa kuwa wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya, na hii itafanya hata vyama vya siasa navyo viingilie kati kuhakikisha watu wake wanashinda kwenye kamati za maendeleo za kata kitu ambacho ni hatari sana kwa mustakabali wa Taifa kwa kuruhusu wanasiasa kuteka mabaraza ya katiba ya wilaya.

Ushauri, nashauri baada ya uchaguzi wa wajumbe kwa ngazi ya mitaa na vijiji kumalizika, watu wote wataokuwa wamechaguliwa na majina yao kupelekwa kwa Afisa mtendaji wa Kata badala ya wajumbe wa kamati ya maendeleo ya kata kuwachagua wajumbe wa baraza la katiba la wilaya itumike njia ya kuandaa vikaratasi vya aina nne, ambavyo wagombea wa kila kundi watagawanywa kila mmoja anagombea kupitia kundi lipi ambapo kwa mfano kundi la mjumbe mmoja kutoka vijana, kama kata ina vijiji vitano, kutakuwa na vikaratasi vitano, moja itakuwa na alama ya vema (V) na nyingine nne zitakuwa na kosa (X), vikaratasi hivyo vitawekwa ndani ya sanduku ambapo mtu atakayetoa kikaratasi cha V ndiye atakayejiunga na katika baraza la katiba la wilaya, utaratibu huu utasaidia kuondoa manung'uniko na uchaguzi uliogubikwa na mazingira ya rushwa, udini, ukabila, kujuana, uitikadi, mizengwe nk. Mi naamini kuwa wajumbe wote watakaokuwa wamechaguliwa na mikutano ya vijiji na mitaa watakuwa na sifa zote na pindi mmoja wao akichaguliwa kwa kwa njia ya karatasi bila kampeni haitaleta mtafaruku katika jamii.

Kasoro nyingine katika muundo wa mabaraza ya katiba ya wilaya ni kukosekana nafasi za jamii wenye ulemavu, Tume katika mwongozo wake ingeweka hata nafasi kumi kwa kila baraza la katiba la wilaya kwa watanzania wenye ulemavu ili kuleta usawa.
Ushauri wa mwisho ninaisihi Tume ya Marekebisho ya Katiba kuwa na uzalendo wa kuchukua maoni ya wadau yanayolenga kuboresha mchakato wa kupata katiba safi, na wakati mwingine kabla haijatoa mwongozo iwe inatoa kama rasimu ya mwongozo inaotaka kuutoa ili wadau nao waweze kuweka mawazo yao kwa lengo la kuboresha mchakato mzima, na kuondoa mtazamo kuwa mtu anapotoa maoni yake anaionea wivu Tume.
 
Hongera mkuu, una akili sana, hoja yako imekaa vyema, tatizo viongozi wetu wanasoma? Nawaomba wasome ili tupate wajumbe bila kuingiliwa na wanasiasa.
 
Ni vigumu sana kutenganisha siasa ktk uandaaji wa katiba kwani wanasiasa wamo miongoni mwa jamii. Muhimu ni kutia shime ili watu wa kada nyingine ktk jamii washiriki hasa ukizingatia ushiriki ni hiari ya mtu. Unaweza kuwatoa wanasiasa kisha ukakosa akidi ya watu kwenye hayo mabaraza, nini kitafuata. Sina maana kuwa akidi ni muhimu kwenye mchakato wa katiba, lkn kila jambo linahitaji watu, na penye watu alihalibiki neno.

Mtoa hoja pia akumbuke wabunge wote wanaingia kwenye bunge la katiba kwa nafasi zao, hapo napo vipi ilhali sheria ya tume imeshatamka hivyo?
 
Back
Top Bottom