Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,380
WARAKA MAALUM KWA WASANII WA BONGOFLEVA.
"MZIKI BILA VINA UNAWEZEKANA"
Kwanza pokeeni salaam zangu za Krismas na mwaka mpya 2018, Mimi ni mwenzenu Deogratius Nalimi Kisandu kwa jina la kisanii "MASQO", Leo nimekuja na matunda ya pwani kutofautisha kati ya ndizi mbivu na ndizi mbichi. Hoja yangu ni kuwa tunaweza kuimba Mziki bila kuweka VINA kwenye mashairi au ngonjera zetu(verse).
MASHAIRI na NGONJERA YA VITABUNI.
Mashairi au Ngonjera kama za Mashairi ya Chekacheka, Wasakatonge sio mashairi yanayotumika kwenye mziki, haya ni mashairi ambayo huandikwa kwa ajili ya kusomea shuleni au vyuoni na pia ni mashairi au ngonjera zinazotumika kufikisha ujumbe usio na mziki, mfumo huu pia huandaa kuunda washairi wa Vitabu na waimbaji wabadae. Mashairi haya lazima yawe na Mizani, Beti na VINA na yanakuwa na mpangilio maalum wa kiufundi. Huwezi ukatumia mfumo huu wa mashairi kuimba Mziki wa HIPHOP au Taarabu au Bolingo au Mchiriku.
MASHAIRI YA MZIKI WA CHIPUKIZI.
Msanii anayeanza kujifunza Mziki ana lazimika kutumia VINA kwenye mashairi yake(verse zake) ili aweze kuimba vizuri kwa kufuata biti na kwa kufuata Mziki wenyewe. Msanii chipukizi anakuwa hana utalaam wa kutambua kuwa huu mziki nifuate key (funguo) gani ili aendane na biti, hivyo huimba mashairi yanayoshabihiana na ngonjera yakiwa na VINA mwanzo mwisho. Na msanii huyu akikomaa na kuujua Mziki huachana na muundo huo maana tayari anajua funguo ya Mziki wake.
MASHAIRI YA MSANII MZOEFU.
Msanii mzoefu tayari anajua key ya kila biti au mziki Fulani na hivyo anaweza kuimba bila kuweka VINA Bali maneno yake yanaambatana na biti au mziki, mfano Freestyle, pia Prodyuza wa Mziki anawajibu wa kupanga wimbo wa Msanii pale ambapo ameenda Offkey (kinyume na mziki), ndio maana kama unajua mziki ukifika studio na kupewa biti unaweza kupanda na biti kwa mashairi kutoka kichwani ambayo umeyapata kulingana na wazo lako jipya. Mziki ni Mziki haijalishi umeimba kwa VINA au hakuna VINA Bali kinachopaswa ni kwenda na Biti na Mziki wenyewe.
HAKUNA ANAYEIMBA MZIKI FLATI.
Kuna aina ya uimbaji ambayo Msanii anaimba wengine husema ni Flati hasa Wasanii wanaoimba kwa Kubana PUA, mfano uimbaji wa 50Cent mwanamziki wa Kimarekani angekuwa Tanzania wange sema anaimba FLATI SANA, kumbe yeye habani pia Bali anatoa Sauti yake kama ilivyo, uimbaji wa Ja Rule yote ni staili ambayo msanii anafikiri inaweza kubamba, Wimbo wa kwanza wa Mez B (Kwanza Fikiria), na wimbo wa Kwanza wa Ney wa Mitego kwa Leo unaweza kusema wameimba FLATI, kumbe ni mtindo tu wa muimbaji. Pia fatilia uimbaji wa Mwanamziki wa zamani wa T.O.T Captain Komba unaweza sema anaimba FLAT kumbe ni mtindo wake tu.
Nawatakia Siku njema na Krismas njema katika Bwana na Mkombozi wetu Yesu Kristu hasa kwa Damu yake Takatifu. Naandika waraka huu nikiwa wilayani Kahama, Shinyanga.
Wasalaaaaam
Deogratius Nalimi Kisandu
24 Desemba 2017.