Waraka wa CCM : ikulu itoe maelezo

Geeky

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2013
Posts
307
Reaction score
179
Dodoma.
Waraka unaodaiwa kuandaliwa na CCM kwa ajili kuwaelekeza wajumbe wake kwenye Bunge Maalumu la Katiba kutetea msimamo wa Serikali mbili umepokewa kwa hisia tofauti huku Rais Jakaya Kikwete akitakiwa kujitokeza hadharani kueleza msimamo wake.

Waraka huo uliibuliwa na gazeti hili jana ukibainisha sura ya Serikali mbili inayotakiwa na CCM, likiwamo pendekezo la kuanzisha Baraza la Wawakilishi la Tanzania Bara.

Hakukuwa na sababu ya kuweka Tume ya Mabadiliko ya Katiba iwapo nao wanakuja na waraka wao, tunatakiwa kuboresha yaliyomo kwenye rasimu ili tuweze kupata Katiba yenye maoni ya watu," alisema.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Gaudence Mpangala alisema iwapo CCM kimesambaza waraka huo, kinafanya makosa kwa kuendeleza misimamo isiyokuwa na hoja za msingi kwa Watanzania... "CCM kusambaza waraka huo ni dalili mbaya za kuleta machafuko miongoni mwa wajumbe..."

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Nicholas Mgaya alisema hatua ya CCM kusambaza waraka huo ni kutapatapa kwa kuwa yaliyomo hayatawezekana kupitishwa na Watanzania.

Mgaya alisema waraka huo umevunja Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inayozuia kusambaza maoni ya makundi katika mchakato huo.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba alisema tatizo siyo kuwa na msimamo wa chama kupitia waraka huo, bali kuusambaza... "Sijaupata waraka huo lakini kitendo cha kuusambaza tu kisheria ni makosa, walitakiwa kutumia nafasi na wajumbe wake kupeleka hoja hizo bungeni," alisema Kibamba.

Wabunge CCM wanena
--------------------------------------
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema katika hali ya kawaida, kila kundi katika jamii lina fikra zake kuhusu mapendekezo yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na haki ya kupendekeza kile ambacho linaona kinafaa kuongezwa au kuondolewa na kwamba kuwa na mtazamo tofauti kuhusu jambo fulani ni kitu ambacho hakizuiliki.

"Binafsi ningependa kupata waraka kutoka kila kundi ili nisome na kujua mawazo mazuri yaliyopendekezwa. Ukipitia ni wazi kuwa utakutana na mambo mazuri tu. Hili ni jambo ambalo lipo wazi kabisa."

Hata hivyo, Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa (CCM) alisema chama hicho hakijagawa rasimu yoyote.

Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi Kigwangalla alisema hana hakika iwapo waraka huo umesambazwa kwa wajumbe.

Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy naye alisema hajauona waraka huo, kauli ambayo iliungwa mkono na Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage.

Jana, gazeti la mwananchi lilichapisha taarifa za kuonekana kwa waraka huo, ambao pamoja na mambo mengine, umetoa mapendekezo katika ibara 42 za Rasimu ya Katiba ya Tume na kupangua hoja mbalimbali ikiwamo ya muundo wa muungano huku ikitaka mfumo wa Serikali mbili uendelee lakini ufanyiwe marekebisho.


source : Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Tunakoelekea tutamtaka Rais Kikwete ajiuzulu.Tunahitaji katiba mpya na bora kuliko tunavyouhitaji utawala wa Rais Kikwete
 
Kama kweli ikibainika waliusambaza, HATUA gani itachukuliwa? Kwakweli wananchi tunawasiwasi sana na huu mchakato wa kupata KATIBA mpya. Kama kweli tutapuuzwa mawazo yetu, basi tutakosa IMANI na hao watakaosababisha maoni yetu kutofanyiwa kazi.
 
Tunakoelekea tutamtaka Rais Kikwete ajiuzulu.Tunahitaji katiba mpya na bora kuliko tunavyouhitaji utawala wa Rais Kikwete

Hahahaa umenikumbusha ya Fr Nyalali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…