Waraka wa John Bocco kuhusu timu ya Taifa

Waraka wa John Bocco kuhusu timu ya Taifa

Keng'oni

Senior Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
183
Reaction score
147
JOHN%2BBOCCO.jpg


"Nikiwa kama mchezaji waki TANZANIA ninaecheza ligi ya hapa nyumbani na nikiwa mmoja wa wachezaji katika Timu ya Taifa ya kizazi hiki cha sasa wa Mudamrefu. Naandika hivi nikiwa na huzuni na masikitiko makubwa juu ya mpira wetu wa TANZANIA kwa ujumla kuanzia club zetu, ligi yetu na mpaka kwenye Timu ya TAIFA 'TAIFA STARS'.

Sijaandika ivi kwania ya kufundisha wala kukosoa MSHABIKI, KIONGOZI WA MPIRA, VILABU VYA TANZANIA, SHIRIKISHO LA MPIRA WA TANZANIA na wala TIMU YETU YA TAIFA YA MPIRA WA MIGUU.

Toka nilipopata akili ya kuutambua mpira wa TANZANIA kwa kuusikiliza kwenye redio na pia kuona bahazi ya mechi kwenye Tv za vilabu pamoja na Timu ya TAIFA nilikuta ukiwa na lawama upande wa Wachezaji pamoja na Uongozi wa uendeshaji wa mpira wa VILABU pamoja na TIMU YA TAIFA mpaka nilisikia timu yetu ya TAIFA IKIITWA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU.

Mimi nikiwa kama Mtanzania pia nikiwa miongoni mwafamilia ya mpira wa tanzania pia inaniuma sana nikiiona mioyo ya watanzania wa penda soka mamilioni ikiteseka kutopata furaha ya mpira.

Wewe kama mtanzania mpenda soka, Unahisi furaha inakoseshwa na Wachezaji wa kitanzania, Uongozi na uendeshaji mpira wa kitanzani, Mashabiki wa kitanzania au TATIZO NI NINI?

Kwafikra zangu mimi nahisi mpira wa tanzania unaasiriwa 1. Kutokuwa na program za kuendesha mpira kisasa 2. Kutokuwa na misingi endelevu ya kuendesha wachezaji wa dogo kisasa 3.kutokua na ligi kuu bora nchini 4.Kuwa na huaba wa wachezaji wachache wanachezesha njee ya nchi ndani ya Timu ya TAIFA 5.Kutothamini na kueshimu wachezaji wakitanzania walio ndani ya ligi yetu na njee ya ligi yetu etc.

1. PROGRAM ZA KISASA ZA KUENDESHA MPIRA WETU.

Tanzania tupo nyuma sana yani tunaongoza mpira kizamani sana kwa upeo wangu mimi wa sasa mpira hauchezwi na kipaji tu Bali pamoja na elimu ya mpira Ndio maana wenzetu wanakuwa na shule za mpira, mfano' sisi watanzania tunaleta makocha wa kisasa kwenye club zetu pamoja na timu yetu ya taifa, ila mnasahau kuwa wachezaji wenu hawajaandaliwa kisasa pia hata makocha wanaowafundisha sio wa kisasa.

Tunatakiwa sasa tuamke kuwapeleka makocha wetu wakajue mpira wakisasa unavofundishwa ili waje kuwafundisha wachezaji mpira huo ili hata tukileta makocha wakigeni ambao ni wakisasa wawe wanatuongezea kipya sio kuanza tena moja. Pia na shirikisho la mpira liongoze mpira kisasa hata kwakuiga basi nchi zilizoendelea zaidi yetu kimiprira kuwa walianzaje na wamewezaje sio kwa mifumo yetu hii yakizamani na mawazo yetu ya mtu mmoja mmoja.

KUTOKUWA NA MISINGI ENDELEVU YA KUENDESHA WACHEZAJI WADOGO KISASA.

Tanzania tuna uhaba wa vituo vya kuendesha soka na kutengeneza vipaji vya vijana wadogo pia tuna utamaduni ambao sio wakisasa wa kuinua na kutengeneza vipaji hapa nchini, sisi watanzania club na shirikisho letu huwa wanainua vipaji sio kutengeneza vipaji kama kwa nchi za wenzetu. Kutengeneza kipaji ni nini?

Kutengeneza kipaji katika soka nikumchukua Mtoto asiejua hata maana ya kupiga pasi, krosi shuti na kuanza kumfundisha moja baada ya moja mpaka kufikia kugeuka na mpira na kupiga chenga. Kuinua kipaji ni nini?

Kuinua kipaji ni kumkuta Mtoto wa umri wamiaka 15, 16 mpaka 17 na kuendelea akiwa anajua nn maana ya kupiga pasi, krosi, kugeuka na mpira na mpaka kupiga chenga, kwa maana hiyo sasa ukifatilia club zetu hata shirikisho letu la mpira hawana malengo na watoto wenye umri wa miaka 8, 9, 10, 11, 12, 13, 14 na 15 kuwaandaa ambao hawa unaweza kuwapa msingi wowote wa soka unaoutaka.

Bali tunaanza na watoto wa umri wa miaka 17, 18, 19 na 20 na kuendelea ambao washapitia kwenye misingi ya kizamani ambayo yamitaani ya kupiga pasi,krosi na chenga, ambao umri huo nchi za wenzetu zilizo endelea umri huo wa miaka 17 - 20 unawakuta wakiwa tayari na wekicheza Timu kubwa pamoja na timu ya taifa kwa mafanikio sio kwakupata uzoefu.

Tuamke watanzania pamoja na shirikisho letu na vilabu vyetu tusitake mafanikio ya haraka ambayo yanazidi kutupotezea muda kumchukua mchezaji wa umri wa miaka 17 nakuendelea aliepitia misingi mibovu ya mpira ndio ukataka umbadilishe na kocha wa kisasa wakigeni wa u17 wa timu ya taifa bali tuchukue Mtoto wa miaka 8 mpaka 12 tumpe kocha wa kisasa, madocta wa kisasa, elimu ya kisasa na malezi ya soka la kisasa alfu tuone kama hatutoweza shiriki kombe la Afrika.

3. KUTOKUWA NA LIGI KUU BORA NCHINI.

Kkuwa na Ligi Kuu bora chini ni kioo kwa kuinua mpira wa nchi yetu, kwa mfano kama kwa sisi Tanzania naweza kusema asilimia 90% ya wachezaji wa Timu ya taifa wanatoka katika ligi yetu ya nyumbani lakini kiukweli ligi yetu haina ubora kuanzia kwa maandalizi ya wachezaji toka walipoanzia soka (mafunzo ya soka waliyoyapata) pili uendeshaji wa club zetu hapa nchini miundombinu inayotumiwa kuendesha ligi yetu hapa nchini mfano viwanja tunavotumia vibovu, mipira tunayotumia mibovyu kwenye ligi, jezi mbovu waamuzi sio wazuri ni waamuzi wanachezesha kizamani.

Kwa sababu tukija kucheza mechi zakimataifa tunakutana na mipira mizuri viwanja vizuri waamuzi wazuri wakisasa na ndio mana timu za tanzania kwenye mashindano ya kimataifa tunapata kadi nyingi ofsaidi nyingi mwisho tunafungwa kumbe tatizo tulizoeshwa vibaya na marefa wa ligi yetu.

Kwa maana iyo basi huwezi kumpata mchezaji wa Timu ya taifa mzuri kutoka kwenyeligi yetu mbovu isiyo na viwanja bora mipira bora uongozi bora marefa bora wala mashabiki bora, hiyo nichangamoto kwetu watanzania wote wapenda soka tushtuke na tubadilike ili mpira wetu uinuke bilaivo mtalaumu wachezaji tu mpaka Somalia watashiriki world cup sisi hata Afican cup hatutagusa.

Waandishi wa habari na mashabiki wa MPIRA WA TANZANIA muamke na mbadilike kunavitu muhimu sana vya kusema ili soka la tanzania libadilike kunavitu Vingi sana vya kusema ili vibadilishwe ili tanzania tusiwe tena vipofu kwenye ulimwengu huu wa soka la kisasa sio soka la mdomoni wala magazetini sio soka lakupanga Timu ya TAIFA kwenye gazeti au kwenye vijiwe jioni tukikaa ila imefikia wakati wa kupanga timu au kuchagua timu kwa mtu husika sio kwamawazo ya mtu mmoja mmoja.

Kwa kufanya mabadiliko ya kuwa na ligi bora ili tupate wachezaji bora kwa ubora wao utatengeneza Timu ya taifa bora na tutapata wachezaji wengi watakao fikia kiwango chakucheza mpaka njee ya nchi ambao tukifikia hatua hiyo tutakua na Timu ya TAIFA bora zaidi kwa badae ambayo tukija kupangwa tena na NIGERIA miaka ya badae tutakua na uwakika wakuwafunga ila kwa hivi tunavoenda hatatukiwafunga tumewabahatisha tu kiukweli TANZANIA tulipo sasa na soka la ulimwengu huu lilivofikia bado sana.

Tubadilikeni watanzania hii niaibu si kwa wachezaji tu ila ni kwanchi nzima mtawalaumu wachezaji tu ila wachezaji sio tatizo tatizo tunamifumo ya kizamani alafu bado tunailazimisha iendelee.

TULISHAFELI, TUMEFELI NA TUSIPOAMKA TUTAFELI KABISA yani tutakua wa mwisho KABISA duniani. Ebu jiulize wewe mwenyewe uliviona vizazi vingapi tanzania vilivyopita na vilikua na wachezaji wazuri?

Ukipata jibu jiulize tena vilietea mafanikio gani kwenye timu ya taifa au vilabu vyetu ambayo tunajivunia sasa?

Kwa mimi toka nivisikie na kuadisiwa mpaka leo nacheza sijao mafanikio zaidi ya kuwa na sifa zisizofaidisha nchi. Tubadilikeni jamani hayo nimawazo yangu tu kama nimewakosea nisameeni ila hata sisi wachezaji mnaotutukana mais kutuona sio wazalendo inatuumapia kwasababu tunatumia nguvu zetu bilamafanikio nakinachouma zaidi hatupendi kufeli ila tunafelishwa inauma kwa kweli ila nyumbani ni nyumbani TUNAIPENDA NCHI YETU NA TUTAIPENDA MILELE ila tusikubali kupelekwa tubadilikeni watanzania,".


CHANZO: Bin Zubeiry
 
Hayo maneno yapo miaka nenda rudi na wala sio mapya. Suluhisho ni Serikali kuingilia kati ivunje TFF yote ili Fifa watufungie hata miaka 3 tuanze upya kabisa. Maana tukisema tunaanza upya kwa muundo na watu wale wale waliopo kwanye uongozi wa mpira wa sasa ni kazi bure tuu. Na nadiriki kusema hadharani kabisa hakuna Kiongozi wa kada zote alieniangusha na kunitia hasira sana kama Jamal Malinzi,tulimtegemea sana kama Msomi na pengine kijana akili inachangamka na anaishi kisasa kumbe ndio bomu kubwa kuliko yote yaliyowahi kutokea kwenye uongozi wa Soka la Bongo,tena heri ya akina Alhaji Ndolanga na pengine hata Mzee Dalali wa Simba na Marehemu Mzee Matunda wa Yanga. Poor you Malinzi!
 
Acha uongo, nyie wachezaji ndio tatizo, mfano timu ya azam ilimfunga mwarabu hapa nyumbani bao 2 mkaenda kule mkapigwa tatu! hapo unamlaumu kocha? je wewe tangu uanze kucheza timu ya taifa umewahi kuifungia magoli mangapi? Mbona yanga walipo cheza na mwarabu hapa walizidiwa lakini walipo kwenda kwao ndy walicheza mpira mzuri sana.
 
Acha uongo, nyie wachezaji ndio tatizo, mfano timu ya azam ilimfunga mwarabu hapa nyumbani bao 2 mkaenda kule mkapigwa tatu! hapo unamlaumu kocha? je wewe tangu uanze kucheza timu ya taifa umewahi kuifungia magoli mangapi? Mbona yanga walipo cheza na mwarabu hapa walizidiwa lakini walipo kwenda kwao ndy walicheza mpira mzuri sana.

Hilo ndio tatizo letu kubwa wabongo,hatutaki kukubali kuwa tumekosea na kwa hatua ile tumeshindwa. Yeye ni sehemu ya tatizo but anatengeneza mazingira ya kuonekana yeye kuwa sio sehemu pana ya tatizo husika. Hapa suluhisho ni hilo nililolitoa hapo juu,kuwa tukubali kuwa tumefeli tuanze upya kabisa na Waswahili wanakwambia kuwa kuanza upya sio ujinga bali ni ushujaa.
 
Kaka umechemsha huo ushauri ungeutoa kabla hujaukubali unahodha wala kabla hujapanda pipa kwenda S.A, si mlijitamba kuwa mmejiandaa vya kutosha
 
Kwenye uongozi wa Mpira nako wameingia waganga njaa. Tusishangae. Tunavuna tunayopanda
 
kwanza kaandika kiswahili kibovu wakati kapewa u captain wa timu ya taifa,yeye mwenyewe anaonyesha dhahiri hajitambui anatakuwa mwanasiasa sasa na yeye,maana mpira ushaisha hapo madhani anafikiria kustahafu awekiongozi wa TFF
 
Nilifikiri anaomba msamaha kwa upuuzi wanaendelea nao hulo SA na kwamba yeye ameamua kuachia ngazi?!
 
Maneno kuntu haya.

Ushauri huu aliutoa Jenerali Ulimwengu kipindi kile akiwa Mwenyekiti wa BMT pengine zaidi ya miaka kumi iliyopita, na kipindi hicho tukiwa na mzozo na FIFA kuingilia mambo ya TFF ya zamani (FAT) kutoka Serikalini. Jenerali alishaur wacha tufungiwe tusafishe nyumba yetu, tuweke mifumo mizuri ya uendeshaji na mambo yote ya mpira wa miguu angalau kwa miaka mitatu, tukitoka hapo tuombe tena kujiunga na FIFA.

Looh!, lakini siasa zetu za Simba na Yanga halikuwezekana, haya tumeshiriki mashindano ya kimataifa kwa hiyo miaka zaidi ya kumi tumepata NINI?

Kipindi kile angalau hata utandawazi wa soka ulikuwa siyo juu namna ile kama ilivyo leo, ambapo utandawazi wa soka umetamalaki na soka sasa imeshakuwa biashara rasmi.

Yanga na Simba na ni kwa upande mmoja ni mtaji kama mazingira ya uendeshaji wa mpira unakuwa huru na haki bila rushwa lakini kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa na jinsi vile vile vinavyotumika siyo tu kwenye siasa za mpira mpaka kwenye siasa kuu inahitaji nguvu na msukumo mkubwa na kujitoa kweli kweli kuleta mabadiliko chanya ya soka letu.
 
Maneno kuntu haya. Ushauri huu aliutoa Jenerali Ulimwengu kipindi kile akiwa Mwenyekiti wa BMT pengine zaidi ya miaka kumi iliyopita, na kipindi hicho tukiwa na mzozo na FIFA kuingilia mambo ya TFF ya zamani (FAT) kutoka Serikalini. Jenerali alishaur wacha tufungiwe tusafishe nyumba yetu, tuweke mifumo mizuri ya uendeshaji na mambo yote ya mpira wa miguu angalau kwa miaka mitatu, tukitoka hapo tuombe tena kujiunga na FIFA.

Looh!, lakini siasa zetu za Simba na Yanga halikuwezekana, haya tumeshiriki mashindano ya kimataifa kwa hiyo miaka zaidi ya kumi tumepata NINI?

Kipindi kile angalau hata utandawazi wa soka ulikuwa siyo juu namna ile kama ilivyo leo, ambapo utandawazi wa soka umetamalaki na soka sasa imeshakuwa biashara rasmi.

Yanga na Simba na ni kwa upande mmoja ni mtaji kama mazingira ya uendeshaji wa mpira unakuwa huru na haki bila rushwa lakini kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa na jinsi vile vile vinavyotumika siyo tu kwenye siasa za mpira mpaka kwenye siasa kuu inahitaji nguvu na msukumo mkubwa na kujitoa kweli kweli kuleta mabadiliko chanya ya soka letu.

Hivi Mkuu BMT bado ipo siku hizi?nadhani ilikufa alipoondoka Mzee Said El Mamry.
 
Naomba leo mfungwe pia ili akili ikae sawa,
halafu nitafurahi kweli mkifungwa.
Unaleta utetezi yote hayo hukuyajua?
 
Kaka umechemsha huo ushauri ungeutoa kabla hujaukubali unahodha wala kabla hujapanda pipa kwenda S.A, si mlijitamba kuwa mmejiandaa vya kutosha

Tena Ktk Chezaji Linalonitia Kichefuchefu Ni Hili Hili Lilitoa Huu Waraka POPOMA Wake. Ni Huyu Huyu Mchezaji Siku Azam Ikicheza Tu Na Simba ANAKOMAA, ANAGANGAMALA Na Kuzunguka Uwanja Mzima Na Kutufunga Simba Sasa Ngoja Azam Hiyo Hiyo Angalia Jinsi Mchezaji Huyu ANAVYOCHEZA Kwani Hukimbia Hovyo na Kizembe Uwanjani Na Kivivu Utadhani Kachomekewa Bua La Mhindi Ktk NYELEO ( Nduku ) Lake. Na Mkae Mkijua Hata Kama Mmefanya Mbinu Eti Mrudi Leo Usiku Ili Kukwepa Mashabiki Wenye Hasira ( Gentamycine Inclusive ) Tusiwachape Ila Nakupa Salamu Kuwa Wenye Uchungu Na Timu Yetu Leo Tunakesha JNIA Kuwasubirini TUWAPENI KIPONDO Kidogo Ili Mtie Adabu. Mtafungwaje Na Wavuvi? Nyie Kweli Ni MAPOPOMA Na Haswa Wewe Captain Boko Ndiyo POPOMA Uliyetukuka Na Nimekuona Mechi Zote Mbili Ulizocheza Dhidi Ya Swaziland Na Madagascar Na Kwa Utaalam Wangu Mkubwa Wa Mpira Na Kwa Mpira Niliokuwa Nikicheza Kipindi Changu Mimi Ningekuwa Ndiyo Kocha Wa Taifa Stars UNGEITWA Ktk Labda Baada Ya Mimi KUFUKUZWA au KUFA GHAFLA Kwani Hujui Mpira Na Unabahatisha Bahatisha Tu. Na Salamu Hizi Mfikishie Pia Na POPOMA Mwenzio Abubakary Salum Sure Boy Kwani NYIE Kwa Pamoja Ndiyo Huwa Kila Mechi Yenu Na Waume Zenu Yanga IKIKARIBIA Tu Huwa Mnaenda Kukinga ( Kuchukua Pesa ) Kwa Seif Magali Kisha Mnacheza Chini Ya Kiwango au Mnazitafuta Yellow Na Red Cards Kwa Makusudi ILI Mdhoofishe Timu Yenu. Tena Ndiyo Nime Just Log In Na Kukutana Na Uzi Unaokuhusu Na Ndiyo Umenipandisha Mzuka Wa Kizanaki na Kiyao Na Kusababisha Hadi Kuondoa Mood Yangu Ya Siku Nzima.
 
Haya ayasemayo bocco yangekuwa na mashiko kama timu yetu ingekuwa inafungwa na timu za ulaya au hayo mashindano inayoshiriki na kuvurunda yangeshirikisha timu za ulaya. Timu za ulaya ndo zina mazingira ayasemayo Boco. Kwa Africa (ukiondoa SA na arabic countries) ndo zinaanza anza kuiwe hiyo miundombinu, so hata hazijaanza kuvuna matunda yake, ndo maana nasema nchi zinazoshiriki hayo mashindano tunafanana mazingira na matatizo. Unafungwa na timu ambayo unafanana nayo almost kwa kila kitu, tena yenyewe iko chini ktk fifa ranking halafu unaleta utetezi wa ajabu namna hii.

Kuvurunda kwa timu yetu kumetokana na sababu kuu mbili:
1) uteuzi wa kucopy na kupaste
Unamchukuaje mtu kama Kiembe, Dida na Boco mwenyewe amabao siyo regular players kwenye timu yake

2) mbinu mbovu za ufundishaji
Timu inacheza unaona wazi hakuna formation, kila mchezaji anacheza kivyake, no team work, hapo utashindaje sasa. Hapa ni wazi kocha kaishiwa mbinu au hafanyi kazi yake impasavyo, hata benchi la ufundi ni uozo mtupu
 
Mimi nakushangaa wewe Boko ambaye hata jina linakusadifu... unapiga maboko tupu uwanjani. Hujui mpira na sijui kwa nini umekuwa captain. captain unatakiwa umshauri pia kocha na benchi Zima la ufundi dogo. mpira hujui afu hata kujieleza hujui na pia Kiswahili hujui, boya wewe. sasa hivi kilichobaki ni kususia mechi zote za taifa stars,,,, mpe taarifa Malinzi.. msomi mzima na rais wa TFF unajisifu kwa kuonyesha mechi live??? ndo tulokutuma???? nakuuliza wewe Malinzi??? Mnatukera sana. Malinzi kawapa nafasi wahaya tupu hadi soka la wanawake wanapewa wahaya.......no progress, sio kwamba nawachukia wahaya ila tunataka watu wanaoweza kututoa hapa to the next level. Tuombe msamaha wewe boko haramu na wewe Mainzi.
 
Mi binafsi naona maneno aliyosema si sahihi.. na hakupaswa kuongea kwa kipindi hichi ambacho yeye ni captain na isitoshe watanzania bado tunamachungu ya kufungwa na timu ya mia sabini na .. kwenye viwango vya FIFA.. kwa uzembe wao hao wachezaji hizi lawama hawezi kuzikwepa timu za Africa karibia zote zinafanana mifumo..
 
Kwanza hana weredi,huu waraka alitakiwa autoe baada ya kumaliza idadi ya mechi walizotakiwa kucheza
 
Mechi ya Tanzania kukamilisha ratiba iko saa ngap wadau?
 
Back
Top Bottom