Waraka wa kwanza kwa utopolo

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
UNAAMBIWA

1. Na ilikuwa siku ya pili ya juma, wachezaji walipojiandaa kwenda kana ya Nigeria kupindua meza kibabe.

2. Nao walipofika katika kijiji kile kinachowakabili, ndipo wakamuona Manara akiwa pamoja na Senzo wakiimbia kwa sauti kuu:

3. "Tumelala yooo, Wananchii tumelala yeeeee," nao walipowasogelea ili wawakemee wakaanza kunena kwa Ki Nigeria wakisema:
"Akieeee and pawpaw, Akii na Ukwaa".

4. Wakawanyamazisha na tazama, zikaja taarifa kuwa wachezaji wao wanne wana uviko na saba wana utapiamlo.

5. Miongoni mwao alikuwemo Fei toto, Diara, Mukoko na Makambo yule anayetoa ulimi kama nyoka wa kibisa.

6. Nawakishakuyajua hayo, wakapaza sauti wakisema "Hatuchesiiiii hatuchesiiiiii" na akasikika yule Yuda akinena kwa sauti "One hour before match, one hour before match" na baada ya kutia huruma sana wakaambiwa waingize timu.

7. Na Katika kipindi cha pili, yapata dakika ya 78 lilipigwa shuti lililolenga lango urefu kimo cha Zakayo mtoza ushuru, kikigusa mtambaa wa Panya upande wa mashariki mwa Lagos, sentimita chache kutoka usawa wa bahari ya Sham walipopita Wayahudi wakimtoroka Farao.

8. Na tazama golini alikuwepo Diara, yule waliyemnadi anadaka mpaka mishale, naye akijua kwamba akilifuata shuti lile atateguka nyonga, akaliacha likaenda zake nyavuni.

9. Ndipo waandishi wa habari wakina Maulidi kitenge na wenzake, wakasambaza taarifa kote Tanzania kuwa "The Return of Champion wa Mapinduzi is Dead."

10. Taarifa zilizambaa kote na kufika mpaka kwa Mamajusi wa Jangwani Mzee Mpilipili hoho na wenzie, nao walikuwa kwenye Vidimbwi wakiwatega Vyura. Na tazama:

11. Ikasikika sauti ya mtu aliye nyikani akanena nao akisema,

12. Enyi utopolo mnaoishi katika kizazi cha Chura, hivi ni nani aliyewaloga?.

13. "Amin amin nawaambia, mkiwaona Yanga wametinga kwenye makundi, ujue hayo ni makundi ya Whatsapp, Telegram ama Facebook."

14. Naye akiisha kunena hayo akajitokeza mbele yao, akapita katikati yao akaenda zake Unyamani.

UTOPOLO 16: 1-14.
 
Dah wakikukamata utajua hujui
 
Halafu usikute wewe ni mtu mzima, na una watoto kabisa! Lakini unakuja kuandika vitu vya kitoto kama hivi!!

Ndiyo maana Dr. Mwigulu Nchemba akiona utumbo kama huu, anatuchukulia Watanzania wote kama hatuna akili vile! Na hivyo anajiongezea tu tozo kadiri apendavyo.
 
Utopolo wewe pumbavu nenda jukwaa la siasa,mpira ni utoto we watu 22kukimbiza mpira mmoja huoni ni utoto,kenge we yaani huyo mwigulu ndio umeona genius wako
 
Utopolo wewe pumbavu nenda jukwaa la siasa,mpira ni utoto we watu 22kukimbiza mpira mmoja huoni ni utoto,kenge we yaani huyo mwigulu ndio umeona genius wako
Wazazi wako bila shaka wanajutia sana kuzaa POOZA kama wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…