Elections 2010 Waraka wa Lowassa kwa vyombo vya habari


Siku moja ina masaa 24. Kampeni zinaisha saa 12 jioni. Barua inasema kikao cha kuchakachua kiliendeshwa hadi usiku. Kwa nini tumwamini Lowasa na siyo barua iliyosainiwa na Kabwe. Kwani kinachoshindikana ni nini kwa Lowasa kusafiri baada ya kampeni na kwenda Mwanza na kurudi Monduli. Dr. Slaa amefanya mikutano mingapi sehemu tofauti kwa siku kwa kutumia helkopita?. Taarifa ya Lowasa haikubaliki.
 
Hivi ni kweli kwamba Nyerere alimkataa Lowasa? Hivi kwa nini alimkataa?

Nyerere alisema " Huyu kijana ni mchafu" kwa maneno mengine alikwisha kupata taarifa zake kuwa alikuwa FISADI toka enzi hizo!!
 
UKWELI NI KWAMBA NYERERE ALIWAKATAA WOTE YEYE NA HUYU RAFIKI YAKE, TATIZO HATUKUMUELEWA. ALIJUA KABLA AKIINGIA HUYU JAMAA ATAKUWA DIKTETA... SASA YAMETOKEA, SASA TUJIANDAE KUANZA MAISHA MAPYA CHINI YA DIKTETA NA SIJUI YATAKUWAJE.... :rip:TZ YA NYERERE!!!!
 
Mhh
nasubiri kwa hamu kubwa kuona Rich Man of Monduli atapata au kupewa position gani kwenye Chama.

Je kisheria inawezekana mtu aliyejiuzuru kupewa tena postion kwenye cabinet au bunge?

The more JK atavyomzogeza karibu na uongozi wa serilai au chama Huyu fisadi na mafisadi wengine the more naona 2015 Chadema wana viti 75 bungeni.

kwa hii Kauli Lowasa kumjibu Dr slaa nakubaliana naye inawezekana hakushiriki.Amekuwa mwepesi kujibu.Mbona hakua na kasi hii ya kutoa majibu kama haya kuhusu Richmond.
 
Hawa waj....umbe mbona wanataka kutudanganya, mbona kila mtu anakimbilia amani!!! hivi kuna utulivu au amani???
 
itakuwa huyu lowasa ameanza ufisadi tangu kjana......................dizaini hizi usijekushangaa hata elimu aliyoipata pia aliichakachua
 
Ampeleke mahakamani huko zitajulikana mbivu na mbichi..zama za kudanganyika zimeisha, hatudanganyiki tena.
 



We Jibu tuhuma zako hayo mengine hayana uhusiano na unavyotuhumiwa. Usitumie jina la mwalimu kujisafisha. Kwanza yeye mwenyewe alikuuliza utajiri umepata wapi mpaka leo hujajibu.

Pili kama unaimani hujaenda mwanza na Arusha kwa muda tajwa, mahakama ndo msema kweli. Nenda mahakamani nao watakuja na utabiri wao.
 
Kwakweli hapakuwa na sababu tena ya hawa miungu watu kurudi tena bungeni safari hii, kunasehemu ambazo wananchi aidha walizidiwa ujanja sana. Ndiyo yale ya Karagwe mbunge mteule anasindikizwa na maninja kusafiri eneo lake kelekea nyumbani.
 
Wote wanao mlalamikia Dr.Slaa wanaonekana kupoteza lengo, maana majina yao yalitajwa kwenye barua inayosemekana iliandikwa na Mkurugenzi wa jiji la Mwanza. Kwakuwa Mkugenzi huyo hajaikana barua hiyo, basi shutuma zingelikuwa zinaelekezwa kwake na wala siyo kwa Dr Slaa ambaye inawezekana aliiona barua hiyo kwenye mtandao kama ilivyotokea kwa wengi wetu.
 


- Mnyonge mnyongeni, he makes a lot of sense na utetezi wake namba moja, lakini namba mbili ni nyepesi nyepesi mno!

- Vipi hana more evidence kama namba one, maana nikiwa Judge nitamnasa kwenye namba mbili!


William.
 
Mheshimiwa Lowassa - usitufanye hamnazo.....tumevumilia saana sasa mnatufanya mabwege!

Jamani nawaomba at least hapa JF tusimuite huyu fisadi kuwa mheshimiwa!!! hawezi kuheshimika katu. mwizi ni mwizi tu hata akishinda ubunge!!!!
 

Kama ni kweli kuwa Lowasa anazungumzia tarehe 19 Oktoba iliyotajwa hapo juu ndiyo tarehe aliyotaja Dr. Slaa kwamba ni tarehe ya kikao cha Mwanza basi Lowasa ni mwongo. Waraka wa Msimamzi wa uchaguzi wa Jiji la Mwanza (Kabwe) ulitaja tarehe 16/10/2010 kuwa ndiyo tarehe ya kikao. Barua yenyewe iliandikwa tarehe 18 Oktoba, hiyo tarehe 19 Oktoba anayoitaja Lowasa anaitoa wapi na ni tukio gani anahusisha na tarehe hiyo?
 
Na huyu EL kaibukia wapi tena kuchafua hewa? aaaaaaaaaaagrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!!
 
Hana lolote mwongo mkubwa huyo...ni yeye alidiriki kusema ni bora alipoteze jimbo la monduli kuliko kuipoteza arusha... Alikuja kuchakachua akakutana na people's power ikabidi ageuze gari...alikuwa na mpango wa kununua kiwanda cha general tyre hapa arusha....na nyumba za manispaa...mwanakharamu we...
 
- Mnyonge mnyongeni, he makes a lot of sense na utetezi wake namba moja, lakini namba mbili ni nyepesi nyepesi mno!

- Vipi hana more evidence kama namba one, maana nikiwa Judge nitamnasa kwenye namba mbili!


William.

Mkuu hata ukiwa jaji wa ovyo ovyo unaweza kumnasa kwenye namba moja pia. Ansema "siku aliyoitaja ya Oktoba 19, nilikuwa katika vijiji vya Mfereji na Enguiki nikifanya kampeni siku nzima." Moja, kwa maana nyingine alikuwa anafanya kampeni masaa 24?. Atasema confotablyhapana, alikuwa akimaanisha siku nzima kama masaa 12 kuanzia asubuhi mpaka jioni. Pili, barua inasema kikao kilifanyika tarehe Octoba, 16, sio Octoba 19. Hapo sijui atajibu nini
 
Hawa waongo, Lowasa ni kweli alienda kumsaidia Batilda kujaribu kuchakachua matokeo lakini pia tunajua hawezi kukubali hadharani kuwa alienda hata aliposhutumiwa na ufisadi na kujifanya kuzira haijawa njia ya yeye kujisafisha. Sasa jimbo limechukuliwa na Chadema wajiandae ufisadi wa ardhi mpaka kwa viwanja vya wananchi wa kawaida. Hivi wanategemea watanzia wengine hawana ridhaa ya makazi bora???? Mi sielewi huu wimbo wa amani wanaoutumia wanafikiri bado tumelala sio. they have to wait and see!!! Their property which they have accumulated is at our disposal regardless of whoever they have registered as the owner
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…