Wana JF, sometimes tuwe tunatoa maoni kulingana na hali halisi sio siasa za chuki tu. hi barua kwa mtu makini inaonyesha wazi kwamba ilichongwa, na seems na wanachadema wenzetu kitu ambacho kinaharibu tu jina la chama. Ingekuwa kweli, kwa barua ya siri kama hio, hawangeweka majina, na cha kushangaza wakaweka majina ya JK, Ridhi, EL, Rostam eti na wengineo, kiserikali ilikuwa either waweke majina yote au wasiweke.
Lowasa ana alama na popote atakapokatisha ataonekana, leo aende mwanza aisionekane, na alisema hajawahi kwenda mwanza miaka zaidi ya 2!. na Pia JK ni Rais, eti aende tu Mwanza kwa ajili ya Kupanga kuchakachua kura, haiji akilini. na wachangiaji wanachangia tu bila kupima. tuongee facts tuache matusi yasiojenga ni uppuzi mtupu
Jwagu, ili ku-balance habari nakubaliana nawe kuwa yaweza kuwa barua si ya kweli, lakini barua kama hii iliyowazi kwa umma inachafua majiana ya watu. Dr Slaa siku zote amesema kama lipo jambo linatatiza yeye yupo tayari kwenda mahakamani, na kwa mantiki hiyo wote waliotajwa na kuhisi wamechafuliwa majina njia muafaka ni kwenda mahakamani ili mahakama iwasafishe na si kutuma habari katika vyombo vya habari kama wanavyofanya. Ni mahakama pekee itakayotuambia ukweli, vinginevyo tutabaki kuamaini kuwa barua ni ya kweli.
Historia inaonyesha kuwa hata Slaa alipotaja orodha mwembe chai walisema ni mzushi na muongo, lakini walipoombwa kwenda mahakamani hata mmoja hakutokea. Mheshimiwa Bomani akatahadharisha kuwa kwenda mahakamani kungezua mambo makubwa zaidi.
Kwa EL, amani ya nchi haivunjwi kwa taarifa za barua,huvunjwa kwa uonevu ikiwa ni pamoja na kukusanya kodi za masikini wa Tanzania na kuingia mikataba yenye manufaa kwa kikundi cha watu wasiozidi 10. Genge hili la mafisadi ndilo limeitikisa nchi na wananchi kuhisi kuwa wanaonewa kwa kulipa kodi ili hali wake zao wakizalia juu ya matenga, na keki ya taifa kutafunwa na walafi wachache wakisaidiana na raia wenye asili za kigeni. Rais alisema pale diamond jubilee kuwa kujiuzulu kwako nchi imetetereka, pengine ni kwa kashfa maana tuna PM wengi waliopita na nchi haikutetereka, kwa hiyo ni wajibu wako kuelewa kuwa katika kipindi fulani cha uongozi wa nchi, uliwahi kusababisha mtetereko wa nchi. Hiyo ndiyo kuvunja amani kwa mtazamo wangu.Kabla huja sota kidole kwa Dr Slaa ulipaswa kutuomba radhi kwa kuteteresha nchi na amani halafu ndiyo usote kidole kwa wengine. Rejea hotuba ya JK Diamond.
Ni kweli mwalimu alituachia amani, nasi sote tunaitunza kwani ni wajibu wetu. Ikumbukwe kuwa hoja iliyopo mbele yetu ni kikao na kama hakikuwepo, basi wewe kama raia mwema na uliwahi kushika uongozi wa juu wa taifa unawajibika kukomesha uvumi wowote utakaovunja amani,hii ni pamoja na kumfikisha Dr Slaa mahakamani, kwa hiyo changamoto iliyo mbele yako si kumhukumu Dr Slaa mbele ya vyombo vya habari bali kuchukua hatua. Tunajua wazi kuwa ni viongozi waliokosa uadilifu walitumia vyombo vya habari kuvunja amani Rwanda, na kwahiyo wewe hupaswi kufuata njia hiyo bali njia sahihi ya mahakama.
Mhe El, mbona wakati taifa linaporwa ukiwa PM kwa mikataba feki hukugusia wosia wa mwalimu wala madhara ya uvunjifu wa amani? Katika kadhia iliyopelekea wewe kujiuzulu hata siku moja hukuwahi kumnukuu mwalimu, vipi leo imekuwaje? Kama unapenda amani kwa dhati ya moyo wako tuambie ninini EPA, Richmondul, Green.., meremeta, n.k. Vinginevyo wapi unapata
moral authority ya kumkemea Dr Slaa ambaye kwa kiwango chochote kiwacho ameonyesha mapenzi na uchungu na taifa hili.?
Mwisho, suala lililopo mbele ni barua, sijui wingi wa watu katika mikutano ya Dr Slaa vinawiana vipi na hoja iliyo mbele yetu. Mrema anapenda kubebwa na hajawahi kuvunja amani kwa kubebwa na wala si
issue kwa watanzania. Kama Dr Slaa anapenda
crowd ili mradi havunji sheria kuna kosa gani. Mheshimiwa, jibu hoja ya barua na si
personal attack. Huu ni udhaifu mkubwa wa kujieleza kama ulivyofanya pale bungeni.
Napenda kukushauri kuwa kwa siasa za Tanzania ni bora utulie monduli na kuendeleza watu wako, kama ipo ndoto ya kurejea madarakani hiyo ni yako binafsi, lakini kuendelea kuwasiliana na umma ukiwa bado na makovu ya kashafa haikusaidii. Kama unapenda amani na chama chako, basi kaa kando kwani nguvu ya umma
''people's power'' imeonekana, na ni ushahidi kuwa kashfa zilizozuka nyakati zako za uongozi zinaweza kuwa zimechangia kuwatia hasira wananchi na wakaamu kutoa adhabu kwa kupitia sanduku la kura. Pengine huu ni mwanzo ipo siku yote yaliyofichwa chini ya kapeti yatawekwa hadharani na wahusika watawajibika. Kamuzu Banda analijua hili vema huko aliko.