Waraka wa Maaskofu unabagua mambo

Nyerere alikuwa bado mwenyekiti wa CCM
Aliwezaje kuleta 'azimio la Zanzibar' kuja kudhohofisha azimio la Arusha wakati Nyerere yupo?
Note: Azimio la Zanzibar siyo rasmi.
 
Waraka wa tisha nyau, watu wakina nani hao huko duniani? kumbe waraka ni kwaajili ya watu walioko nje ya nchi? tulilijua hilo zamaaaani. Tanzania inaongozwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania sio Ubelgiji, canada wala sweden, mnajisumbua sana wazee wangu na waraka hafifu. Mama anajua tulipokuwa tumekwama, wachunga ng'ombe, makuwadi wa neo-colonialism na wapenda sifa na maslahi binafsi ndio waliotufikisha hapa tulipo leo
 
Ukisikia kuzidiwa na nguvu ya hoja ndiyo huko ulikokuonesha wewe.

Kauliza maswali mengine kabisa, wewe umejibu mengine kabisa. Mbingu na ardhi.


Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Mimi ni mkatoliki na kwa sasa ni mwanachama wa ushirika wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, lakini huwa nakereka sana ninapoona ukatoliki ukitaka kuunyanyapa uongozi wa nchi wenye rais muislam.

Umenikumbusha mbali sana awamu ya pili ya Mzee Mwinyi, wakatoliki walipotaka kumuendesha na yeye akafanya kazi kwa upole lakini kwa msimamo thabiti.
 
Kwa hiyo, ulitaka baada ya kuwa umetoka ufichwe uvunguni? Kama jambo ni jema kwa nini hata wengine wasijue? Hata unachoandika humu si kinasomwa na watu wengi duniani pia au unadhani umejificha chumbani?
 
Watawala waanguke tuu, ... ila wasianguke na Tanzania yetu!
😅
 
Sasa utaacha kubagua wakati ni wa kitapeli?
 
Tukosoe serikali zetu kama raia huru sio kama waumini wa dini na dhehebu fulani. Kule Rwanda dini zilihusika sana kuchochea vurugu zao, kule DR Congo makanisa ni sehemu ya shida zao. Watanzania tumeshavuka level ya dini, makabila na kanda zetu. Kwa hili tumshukuru sana Baba wa taifa Mwl Nyerere. Tushirikiane wote kuzisigina cheche zote za udini, ukabila na ukanda kwa nguvu zetu zote. Tumekubaliana kama nchi kwamba wawakilishi wetu sisi wananchi ni wabunge wetu, hatuna mwakilishi mwingine zaidi ya hapo.
 
Baada ya kusoma comment nimejilidhisha kuwa 2025 wapo ambao Hawata mchagua Samia kwasababu ya Dini yake na wapo watakaomchagua sababu ya dini yake! yaani wao kwao DIni ndiyo itakuwa sababu ya msingi kuliko mengine.
Mungu anijalie uhai na siha njema, katu sitamchagua Samia liwake jua au inyeshe mvua. Sababu: mkataba mbovu wa kumpa mwarabu(Dpworld) rasilimali zetu..azimiliki milele.
 
Kwa hiyo, ulitaka baada ya kuwa umetoka ufichwe uvunguni? Kama jambo ni jema kwa nini hata wengine wasijue? Hata unachoandika humu si kinasomwa na watu wengi duniani pia au unadhani umejificha chumbani?
Shida ni pale mwanasheria uchwara anaposema mahakama tumeshindwa lakini tutahamia kwenye mahakama ya wananchi, hapo maana yake anataka kuyaharisha maisha ya watu wengine dhidi ya vyombo vya dola kwa maslahi yake. Hawawaonei huruma wananchi ambao hawana pakwenda zaidi ya hapa Tanzania.
 
Mungu anijalie uhai na siha njema, katu sitamchagua Samia liwake jua au inyeshe mvua. Sababu: mkataba mbovu wa kumpa mwarabu(Dpworld) rasilimali zetu..azimiliki milele.
TICTS alikuwepo hapo bandarini miaka 22 na leo hii ameondoka, hakuna anayeweza kuuza bandari katika miaka hii ya sasa.

Ni biashara tu ya upangishaji wa magati ya bandarini. Mwenye nyumba ambaye ni TPA anayo haki ya kumpangisha yoyote anayemtaka.

Kusema kwamba tunampa bandari mwarabu milele ni uoga wetu usio hata na sababu za msingi.
 
ANDIKA NA WEWE WA KWAKO USIOPOTOSHA
 
Kwanini waraka haukutoka wakati serikali inaruhusu vyama vingi 1992 wakati 80% wa wananchi walikataa?
Mtatafuta sana vijisababu, lakini mambo yashageuka..!!! Muswada wa kubadili sheria haupo tena
 
Sasa utaacha kubagua wakati ni wa kitapeli?
Ungeonekana una akili sana kama ungetaja huo utapeli. Vinginevyo ni ujinga kuzua mambo. Ukizingatia wengi tumesoma tamko la TEC na lipo sawa kabisa. Limewakamata papaya hadi mnahaha. Kila uchwao TEC hivi, TEC vile
 
Mungu anijalie uhai na siha njema, katu sitamchagua Samia liwake jua au inyeshe mvua. Sababu: mkataba mbovu wa kumpa mwarabu(Dpworld) rasilimali zetu..azimiliki milele.
Kwani Nyerere, Mzee Mwinyi, Mkapa, Jakaya, na Magufuli walikuwa wakichaguliwa? Kura zilikuwa Ndiyo au Hapana. Muulize Ali Karume akwambie. Usipomchagua ni kama umemchangua na ukimchagua umemchangua.
 
Unalinganishaje mambo hayo na mkataba wa dp world na bandari, pana ufanano? Naona kama povu la udini linakutoka
 
Nionyeshe haya yameandikwa kwenye waraka wa TEC ukurasa gani? Umesema hapo juu kwamba TEC wanapingana na mahakama na mimi nikakuuliza kama ruling ikitoka huwa watu wanazuiwa kutoa maoni na kueleza mawazo yao? Na nikakuuliza kama kuna hiyo sheria na wewe unarukaruka tu. Naona napoteza tu muda wangu bure kujadili na wewe maana siyo size yangu kabisa!
 
Utapeli uliopo kwenye huo mkataba ni upi haswa?
Waumini nao Wanao Uhuru na akili zao kamili, hawahitaji waraka kana kwamba wao hawajui kinachoendelea nchini kwao. Waraka ni matuzi mabaya ya taasisi iliyosajiliwa kuabudu. Ni kuwafanya waumini mazuzu, kwani hata dk mpango ni muumini mzuri kama mkataba ungekuwa na kasoro angeshauri mapema sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…