Waraka wa Marehemu Chacha Wangwe na Hatma ya Siasa za CHADEMA

ALICHOKIPINGA MAREHEMU HORACE KOLIMBA ni CCM kuwanyima wanachama nafasi ya kupambana katika nafasi ya mwenyekiti wa Taifa. Mwenyekiti wa Taifa ccm huwa hapingwi? Na makamu wake naye huwa hapingwi? Mwanachama akionyesha nia ya kutaka kugombea nafasi za uongozi Nape anasema katiba haimruhusu kuanza kampeni mapema huko ni kuvuruga chama. CCM inawazuia wanachama wake kuanza kutangaza nia za kugombea nafasi ndani ya chama kabla hazijatangazwa? Kumbuka majuzi tu Sumaye aligoma kuwaambia waandishi wa habari kama atagombea urais au lah kwa vile taratibu za ccm haziruhusu? Sasa iweje leo kitendo hicho hicho walichokifanya Zitto, Kitila na Mwigamba kionekane sawa kwa chadema? Nani anayehoji matumizi mabaya ya hela za ccm? Lini ccm walipata kutoa ripoti ya mapato na matumizi hadharani tangu kizaliwe 1977? Kwanza ccm wamejimilikisha mali bila ridhaa ya watanzania ambazo watu wote walizichangia chini ya mfumo wa chama kimoja.
 
Zzk akishakosa cha kusema
anaanza kusingizia uenyekiti

msalit hana tofaut na shwetan
 

Duh...kumbe Chacha Wangwe alikuwa sahihi japo hatukumuelewa wakati ule,maana ukiisoma huu waraka ni kama vile umeandikwa jana, RIP Kamanda Chacha Wangwe.
 
Aisee.......!

Bila kuondoa mzizi wa tatizo, Chadema itaendelea kushuhudia migogoro hii inayosababishwa na baadhi ya viongozi wakuu kuhodhi chama kama mali yao binafsi.

Juzi alikuwa Chacha Wangwe lakini leo yaleyale tunayasikia kwa akina Zitto na sterring bado ni yuleyule (Mbowe) akitumia mbinu zilezile alizozitumia wakati ule (Kuita Msaliti) na hawa wanaoitwa wasaliti wakiendelea kuyalalamikiua yaleyale yaliyolalamikiwa na Kamanda Chacha Wangwe na historia itaendelea kujirudia.
 


Mkuu kumbuka watu wanapoteza maisha yao, kuna watu wanapata ulemavu katika harakati za kuiondoa CCM madarakani. Inauma sana kuona mnaetaka kumuweka madarakani anafanya yale yale ya mnaetaka kumtoa madarakani, kuna haja gani ya watu kufa/kupata ulemavu wakipambana na CCM wakati CDM inafanya yele yale ya CCM.
 
muacheni chacha wangwe apumzike

sawa kamanda, lakini tunajaribu kuoanisha na alichokuwa anasimamia marehemu kiongozi wetu nyakati hizo ajabu ni kwamba kinafanana na 'wasaliti' wa kipindi cha sasa!!! wanachadema tuache upofu kisa tu baadhi yetu tuna mahaba na viongozi.....tupende tusipende mbowe ana tatizo!!!
 
Na walakini wa miaka 50 uliopo kwenyeuongozi wa CCM unauzungumziaje?au wao ndiyo miungu mtu?safisheni macho muweze kuona waTZ hiyo rangi ya kijani inawapumbaza kiasi cha kushindwa kupembua mambo? Tuwafikirie sana watoto wetu na vizazi vijavyo,tuache ushabiki unaotunufaisha kwa siku mbili tatu.Wanatuvuruga ili waendelee kula mikate na asali wakati sisi na watoto wetu tuna ganga njaa nasi tuna kubali?
 

chadema mna akili za kukodi kweli. kwann usijikite kwenye mada unajaribu kupindisha mjadala?? chacha wangwe alisema wazi chadema kuna wizi wa ruzuku, soma huu waraka kwa utulivu
 
Mwanzo niliona kama Vita nyepesi kwa ZZK ni kumbe ni ngumu kama kuiondoa CCM madarakani.
Pole sana ZZK nawe pia utapita kama wapigania Democracia wengine walivyopita.
Nimeshakata tamaa ya wewe kushinda vita hii,RIP Chacha Wangwe sasa hivi ruzuku imeongezeka karibu mara tatu ya uliyokua unapigania ila mikoani bila bila.
 
Mbowe kama unamganga endelea nae usimuachie maana haya mambo unayoyafanya watu hawayaoni wanaona ya wengine wanafukuzwa na kusimamishwa na kuvuliwa vyeo vyao du...!!!

Yaaani hata mie nashangaa,,,sielewi kabisa watu wamelishwa nini. Wanashindwa hata kufocus kwenye makosa ya Mwenyekiti na Katibu ambayo tayari yana uthibitisho wanabaki kung'ang'ana na vitu vya kufikirika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…