Pre GE2025 Waraka wa Mbunge Luhaga Mpina kwa Watanzania: Tumeonewa kiasi cha kutosha sasa tunataka Mapinduzi ili tusionewe tena

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Waziri pekee aliefanya Wizara ya Mifugo kutambulika na kuingiza pato kubwa hadi kutunukiwa cheti cha hongera na IKULU
 
Umejigeuza waziri wetu wa fedha!.

Mpe Mwigulu haya majibu yako, kisha atupe yeye, halafu tutaangalia tunayachambua vipi..

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
You are part of the problem,
Kwanini unayasema haya leo? Unafikiri watu wamesahau uliyowafanyia wakati ule ulipokuwa na madaraka? Tangu umeshika na kupoteza madaraka ulipaswa uwe 'consistency all the way' sio kubadilika badilika kutokana na matuko. Huna 'moral authority' ya kuongea unachoongea
 
Umejigeuza waziri wetu wa fedha!.

Mpe Mwigulu haya majibu yako, kisha atupe yeye, halafu tutaangalia tunayachambua vipi..

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Mwigulu na Mpina wote ni CCM usitarajie watakua na nia njema kwa maslahi ya nchi. So Mwigulu ku underperform hakumfanyi Mpina kuwa mzalendo kisa kuongea mambo asiyo na utaalamu nayo.

Ndio maana nimekuuliza Trillion 40 ndio bajeti alafu Trillion 30 imeporwa kwa mwaka mmoja pekee!! Sasa mishahara ililipwaje?

Unajua we ni great thinker mkuu nashangaa unavyobebwa na upepo wa walaghai.
 
Huyu jamaa ni mnafiki sana, akiwa waziri alikua mkatili kwa wananchi leo kakosa uwaziri ndio anajifanya ana uchungu na wananchi!!

Huyu ni failure tu, nawapongeza sana CCM kwa kumuangusha kwenye ujumbe wa NEC mkoa na taifa.
 
Majina ya zito ni tumbo na maslah yao kwanza
 
Wajumbe wanamtuzima Mpina wanamsubiria 25,ila tatizo la siasa zetu hatujazoea kuambiana ukweli sababu viongozi hawana mioyo na uvumilivu wa kuubeba ukweli na kuufanyia kazi.
 
Naona kitengo kimejipambanua vilivyo kupitia mpina!!

Huyu ni game changer wakimuandaa kimkakati,nadhani ni mgombea urais ndani ya chama atakaefukuzwa na kwenda upinzani kuchukua dola!!

Naamini hata wanaccm wenzangu watampa kura za kutosha hasa kama ccm ikimpitisha mama kama mgombea!!
 
Majina ya zito ni tumbo na maslah yao kwanza
Jibu hoja, GDP ya Tanzania ni almost Tshs 150 Trillion sasa kivipi miamala shuku iwe 280 Trillion let alone hujahesabu miamala isiyo na shuku, so ni kusema Tanzania kuna miamala ya zaidi ya Trillion 1000?

Ukijibu hilo basi nitakubali mimi ni mchumia tumbo.
 
Pamoja b
Hakuna mtanzania ana time na huyo mnafiki. Pia alikatawa ujumbe wa NEC taifa na mkoa na wala sikuona kelele yoyote means watu wamempuuza rasmi.
Acha upuuzi ndugu Zitto junior. Mpina ni mbunge anayejitambua sana na anaonyesha uzalendo sana kwa taifa lake tofauti na nyinyi ambao mko tayari kuuza utu wenu kwa vipande thelathini vya fedha. Angalia hata comment zako hazina likes means wewe ndo watu wanakupuuza kama wanavyopuuza wapuuzi wengine
 
Hahahaha kwamba natafuta likes za ID feki? Ili nipate nini kwa mfano? Mimi huwa msema ukweli na mpenda facts.

Huyo mpina kapotosha hapo sasa kama wewe unasema ni muongo jibu hizo hoja zangu nilizouliza.

1. Bajeti ya Trillion 40 kivipi aseme zimefisadiwa Trillion 30 ilihali mishahara ililipwa ambayo ni zaidi ya 40% ya bajeti!! Au hakuna mtumishi alilipwa 2022?

2. Anadai miamala shuku ina thamani ya 280 Trillion sasa najiuliza kama shuku ni 280 je ukijumlisha na isiyo na shuku ina maana kuna miamala zaidi ya Trilion 1000 ilihali pato la taifa ni 150 Trillion pekee!!

Embu jibu hapa kwanza ndio tuone mimi na wewe nani hajui anachotetea.
 
Safi sana !
Ufisadi = ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa !
 
Naomba kumuuliza Mpina kwamba pamoja na maneno yake mazuri tena ya maana, hivi kipindi kile anachoma nyavu makokoro mitumbwi kutaifisha mifugo kuomba rushwa Ili nyavu na makokoro visichomwe ulikuwa ni wewe Mpina? Hizi akili unazozitumia sasa hivi na kipindi kile zilikuwepo?
 
Chuki binafsi
 
Kwa waraka huu, ninategemea Mpina ajitokeze akiwa mstari wa mbele kwenye MAANDAMANO ya 24 January. 2024.

Tofauti na hapo, apuuzwe tu.
 
Mbona sisi huku kilwa hajawahi kutufanyia hivyo?nilichogundua ni kwamba una chuki nae kisa kaongea uhalisia kwenye utawala huu wa bibi yako
 
Mbona sisi huku kilwa hajawahi kutufanyia hivyo?nilichogundua ni kwamba una chuki nae kisa kaongea uhalisia kwenye utawala huu wa bibi yako
Mkuu fika kanda ya ziwa kuhusu mtu anayeitwa Luhaga Mpina,watakuambia huyu anasitahiri kuwa kuzimu kabisa,mama kajitenga naye hicho ndo kinamuumiza,kauwa watu wengi sana huyu mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…