Pre GE2025 Waraka wa Mbunge Luhaga Mpina kwa Watanzania: Tumeonewa kiasi cha kutosha sasa tunataka Mapinduzi ili tusionewe tena

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tatizo lako Mpina akizungumza mambo yake hupendi kumsikiliza kwa makini, umeshamuhukumu zamani sana kwako hana jema, ndio maana unakuwa negative always dhidi yake.

Hata kama akiwa CCM ni haki yake kuzungumza na asikilizwe, kuwa CCM hakumuondolei hiyo haki yake, usihukumu mtu kwa sababu ya u CCM wake.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Huyu jamaa ni mnafiki sana, akiwa waziri alikua mkatili kwa wananchi leo kakosa uwaziri ndio anajifanya ana uchungu na wananchi!!

Huyu ni failure tu, nawapongeza sana CCM kwa kumuangusha kwenye ujumbe wa NEC mkoa na taifa.
This is your problem, makosa ya beyond 2020 unayatumia kumhukumu leo!.

Tena unawapongeza CCM kwa tabia yao ya kukumbatia maovu, na kuwaadhibu wafichua maovu, ajabu sana.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Yetu macho!
 
Hakuna mtanzania ana time na huyo mnafiki. Pia alikatawa ujumbe wa NEC taifa na mkoa na wala sikuona kelele yoyote means watu wamempuuza rasmi.
Kuna kitu hakiko sawa kichwani kwako!! Tulioingia darasani huwa tunajipa muda wa kusoma na kutafakari.

Comments zako zote zinakuondolea sifai ya usomi na ustaarabu. Kama nilivyosema, ama Kuna shida kubwa kichwani au ni mhusika wa upumbavu unaozungumzwa na Mpina!!
 
Oooh wewe ambaye kichwa kipo sawa nisaidie.
1. Mpina anasema Trillion 30 zilifanyiwa ufisadi mwaka 2021/22. Sasa bajeti ya mwaka husika ilikua ni Trillion 40 hivi, je ina maana mishahara haikulipwa mwaka mzima?

2. Mpina anasema Miamala shuku hapa Tanzania kwa mwaka 2021/22 ilikua Tsh Trillion 280 sasa GDP ya Tanzania ni Tsh 150 Trillion. Sasa kama miamala shuku ni Trillion 280 ina maana ukiichanganya na miamala halali utakuta kuna miamala ya Tsh zaidi Trillion 1000. Sasa basi ina maana Tanzania tuna miamala mingi mara 10 ya pato la taifa tena kwa mwaka mmoja pekee?

Naomba usikimbie hili swali ujibu kwa takwimu maana umesema "umeingia darasani".
 
Bongo nyoso..ukikosoa mfumo na kuelezea changamoto na jinsi ya kuzitatua wanakuona ni mpinzani wanakubagua
Ukitumia akili yako bila kutumia unafiki na akili ya kushikiwa wanakupunguzia ulaji wanakutoa kwenye mfumo wao wa kidhalimu na kifisadi

CCM inataka wazandiki , wahafidhina wenye itikadi wa kusemea vizuri tuu ina uadui na uongo
 
vipi angekuwa anaabudu hao mitume wako napo angekuwa kwenye kuchanganyikiwa?
 
Waziri wa Fedha Mchumi daraja la kwanza alishindwa kujibu hizo hoja bungeni, akaitwa kwenye mdahalo akashindwa wewe ndio utaweza kuzijibu hizo hoja kwa kutumia hisia zako binafsi
 
Waziri wa Fedha Mchumi daraja la kwanza alishindwa kujibu hizo hoja bungeni, akaitwa kwenye mdahalo akashindwa wewe ndio utaweza kuzijibu hizo hoja kwa kutumia hisia zako binafsi
Mbona alijibu bungeni kwamba Trillion 25 ni mishahara out of bajeti ya Trillion 40, ndio akahoji sasa kivipi Trillion 30 iibwe ilihali mishahara imelipwa?

View: https://youtu.be/B_XR2NBGHAk?si=U3kyTJVDDssQv-Ai
Tatizo lenu hamfuatilii mambo mmejaa ujuaji tu.
 
Kwamba kumbe baada ya kuwapindua wakoloni,

Tumerudi tena kutawaliwa na weusi wenzetu,

Ninajaribu kumuelewa Ndugu Mpina mwanamapinduzi.
 
"Tunataka mapinduzi ili tusionewe tena"kauli kubwa sana hii!!

Halafu kigogo media name inaandika hashtag"jeshi limetawala"!!

Mpina unasadifu Nini ndugu yangu!!?

Naongeza hili

"wakati wanajeshi wakilinda mipaka ya nchi yetu,wanasiasa walipaswa kulinda rasilimali zetu,je ulinzi wa rasilimali zetu unaridhisha"!!?
 
Aliyesoma anipe summary Jamaa hasa anasemaje?

Hayo mapinduzi aanzishe Sasa yeye aende Barabarani na familia yake ndio na sisi tutafuata.
 
duuuu kumbe luhaga ni kirusi hatari sana kwa nchi yet ameshasahau dhuruma zoote hizo alizofanya kweli anakuja kujifanya mtetezi kwa sukari
 
duuuu kumbe luhaga ni kirusi hatari sana kwa nchi yet ameshasahau dhuruma zoote hizo alizofanya kweli anakuja kujifanya mtetezi kwa sukari
Hana jipya luhaga,awasumbue dodoma tu,huku jimboni kwake hawamtako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…