Bwana MaxShimba,(Nimekupa rangi ya kijani kama heshima kwani mimi ni mwana mazingira- Environmentalist)
Asante sana kwa kutukumbushia historia ya baba wa taifa, nafikiri kwa yeyote atakae angalia hiyo picha ya nyerere, kama alikuwa na mtizamo hasi, atarudi nyuma na kujipambambanua.
Lakini na mimi kama mwana JF nitoe mawazo yangu, nafikiri watanzania tusiogope kuona yale yanayokwenda kutokea katika nchi muda si mrefu,(kupatikana kwa UKOMBOZI au UHURU), ingawa nasikitika kusema kuwa lazima tutapitia wakati mugumu kidogo, na pengine wako ambao wanaweza poteza maisha kama ambavyo tayari tulivyokwisha poteza baadhi ya ndugu zetu waliosimama kwa ujasiri kutetea maslahi ya watanzania sina haja ya kuwataja maana badhi yao tunawakumbuka. Ila damu zao zitaendelea kuwapa ujasiri watu wengine kupinga ufisadi au fikra za kidini kama ambavyo serikali hii ya kikwete ilivyojitahidi kupalilia haya mambo.
Ni historia pekee ndio itatufanya aidha tupate ukombozi kwa amani au kwa gharama ya juu(watu kupoteza maisha), Amerika ina misingi yake hivyo hatuwezi kujilinganisha nayo na pia South Afrika nao wanahistoria yao na tunapoona leo hii wanafurahia matunda kuna gharama iliyowahi kulipwa huko nyuma.
Viongozi wetu wa sasa katika serikali hii, nawashukuru sana maana kwa upofu walionao, ndio utakuwa mwanzo wa Tanzania, au Tanganyika mpya kwa yale waliopalilia na sasa yamekomaa. Mimi naona hayo yote yanayotokea katika nchi yetu, zikiwemo nyalaka za wakatoliki au waislamu, au na mambo mengine mengi tu ambayo yametokea katika nchi yetu na tutashuudia mengi yakitokea ni harakati za ukombozi. Ila naomba niweke angalizo kwa wanaotetea dini zao, Mungu hana dini, watu wote wana thamani mbele zake, tena kifo cha mwenye dhambi Mungu hafurahii kabisa, lakini kama mtapenda kuendeleza mijadala ya dini, na nyie pie mjue mnafanya gharama ya kupata uhuru kuzidi kuwa kubwa kwa yale yatakayo tokea hapo mbele. Siwalaumu lakini, ingawa mnachochea mafuta na kuongeza ukali na ugumu wa njia tutakayoipitia na mwisho wa yote, watanzania walio wengi watashinda vita hii.