moodykabwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2015
- 625
- 602
WARAKA WA WANACHAMA WA YANGA KWA TFF
TAREHE; 23/02/2019
NA MOODY KABWE
moodykabwe@gmail.com
0715268499
0685188679
Sisi wanachama wa YANGA nchi nzima kwa umoja wetu tuna masikitiko makubwa sana na
mapenzi yetu kwa mpira wan chi hii tunatuma waraka mzito kwa TFF kutokana na vitendo vya
hujuma za wazi dhidi ya timu yetu ya YANGA;
TFF inasimamia mpira katika nchi hii kwa upendeleo mkubwa sana kwa klabu moja tu ya SIMBA
na inaonyesha vilabu vingine havina haki ya kucheza mpira katika nchi hii na kuchukua ubingwa
hivyo basi tunapenda kuufahamisha umma wa wapenda mpira katika nchi sisi kama YANGA
hatukubaliani na mambo yanayofanywa na TFF kwa klabu yetu pendwa ya YANGA
Tunapenda kuwaambia hao viongozi wa TFF waelewe kuwa timu zote zinazoshiriki ligi kuu,
madhumuni ya timu hizo ni kuchukua ubingwa sio vinginevyo ili nazo aiweze kuiwakilisha nchi
katika mashindano ya kimataifa kama ilivyo timu hiyo ya SIMBA wanayoibeba.
Tungependa kuanisha baadhi tu ya mambo ya hovyo yanayofanywa na TFF katika kuihujumu
Yanga ;
1.Asilimia 90 ya uongozi wa juu wa TFF ni wanachama wa SIMBA au watu wenye mapenzi na
SIMBA
2. Asimia 95 wa wajumbe wa bodi ya ligi ni wanachama wa SIMBA au watu wenye mapenzi na
SIMBA
3.Asilimia 90 ya kamati zote za utendaji na uendashaji mpira wa nchi hii ni wanachama wa
SIMBA au watu wenye mapenzi na SIMBA.
Na kuna mambo ya hovyo yanayofanywa TFF katika kutekeleza adhima yao ya kuibeba Simba
ambayo uwezo wao katika mashindano ya kimaifa ni mdogo imepelekea kufungwa mabao kumi
kwa kucheza mechi mbili tu kwa nini wasiache bingwa apatikane kwa uwezo wake uwanjani?
1. Kupanga ratiba ya kuipendelea SIMBA na kuipangia YANGA ratiba ngumu na yenye
kuchosha ili isifanye vizuri katika mechi zake.
2. Kwa kuwapangia waamuzi watakaibeba SIMBA na kuwapa maelekezo waamuzi
wanaochezesha mechi za YANGA na waamuzi wamepelekea kukataa magoli halali ya
YANGA mfano mechi ya YANGA NA COASTAL UNION mshika kibendera kukataa goli
halali la MAKAMBO akidai kaotea,na kukubali goli la kwanza la SIMBA alilofunga
KAGERE dhidi ya MWADUI na pia goli tulilowafunga SINGIDA UNITED limekataliwa
katika mazingira yasiyoeleweka.
3. Kuukalia uchaguzi wa YANGA usifanyike kwa mujibu wa katiba ya YANGA na kutaka
kuuhodhi uchaguzi huo ili watuchagulie viongozi wanaowataka wao TFF badala ya
uchaguzi huo ufanyike na wanayanga wenyewe.
4. Kuwarubuni baadhi ya wanachama wa YANGA wasiokuwa na mapenzi mema na klabu
yetu ili washirikiane nao katika kuihujumu YANGA ili isifanye vizuri katika ligi.
5. TFF inaihujumu YANGA pia isifanye usajili mzuri kwa kupandikiza mamluki kila unapofika
muda wa usajili ili YANGA washindwe kusajili vizuri kwa kutuvuruga.
Sasa kutokana na hujuma zote hizo sisi wana YANGA nchi nzima hatuna imani na TFF
kuendelea kuongoza mpira katika nchi hii.
Hivyo basi sisi wanachama na mashabiki wote wenye mapenzi mema na klabu yetu ya
YANGA nchi nzima tunaazimia kutokuwapa ushirikiano wowote TFF kwa TIMU zote za TAIFA
kwa kutokwenda uwanjani au kuhamasisha ushindi wa timu ya TAIFA na ikibidi tutaingia
mstuni ili kuzifelisha timu zote za TAIFA mpk pale TFF itakapojirekebisha na kutoa haki kwa
timu yetu ya YANGA na vilabu vingine,
Ni mategemeo yangu sisi wanachama na mashabiki wa YANGA tumeeleweka katika kile
tunachokiona kuwa ni hujuma kwa klabu yetu
Wasalaam
-------------------------------------------------------------------------- WANACHAMA NA MASHABIKI WA YANGA NCHI NZIMA
Sent using Jamii Forums mobile app