Waraka wa wazi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Waraka wa wazi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Joined
Aug 15, 2023
Posts
1
Reaction score
0
WARAKA WA WAZI KWA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA KUUNGANO WA TANZANIA DKT SAMIA SULUHU HASSAN.

Mheshimiwa Rais Awali ya yote ninakusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Rais kupitia kipande hiki cha maandishi napenda kuongea na wewe mambo machache yanayolikumba taifa letu na ambayo yameanza kushamiri siku za Karibuni.

Mheshimiwa Rais,

Katika kipindi Cha miezi mitano katika taifa letu kumetokea Matendo mabaya sana ambayo yanaichafua sana nchi yetu na ambayo yanatamausha sana mioyo yetu kama sio kututia shaka sio tu kutembea barabarani bali pia hata kiza kinapotanda na hata kututia wasiwasi kulala majumbani mwetu.

Mheshimiwa Rais,Vitendo vya utekaji kwa makada wa kisiasa,Kupotea kwa watoto wetu pamoja mauaji vimekuwa gumzo sio ndani ya nchi yetu pekee bali pia nje ya mipaka ya nchi yetu kwani,kwa kipindi hicho ambacho matendo haya yameshamiri,Dunia na jamii inakuwa na ukakasi kidogo kuzitafsiri falsafa zako za 4R.

Mheshimiwa Rais,Mimi binafsi na jamii tunaamini Utekaji wa kisiasa ambao ulianza kama utani na ambapo miongoni mwetu tulitegemea ungekoma baada ya kipindi kifupi umegeuka kuwa shubiri na badala yake umefungua fursa ya utekaji wa kifamilia na kijamii.

Mheshimiwa Rais,Ninajua unafahamu tukio la mauaji ya mtoto albino kule Bukoba,Kutekwa kwa Akina Soka,Mauaji ya Mzee Ali Kibao pamoja na matukio mengine mengi yasiyoridhisha yaliyotukia kwa kipindi kifupi.
Mheshimiwa Rais;Sina lengo la kukumbusha tena kuyabusu matukio hayo kwakuwa ninayojua unayafahanu ila ninataka kuyatumia kama reference ya WARAKA Wangu kwako kuhusu matukio hayo ya aibu.

Mheshimiwa Rais panapo wiki hii kumetokea mauaji msituni huko Korogwe Tanga ,katikati ya oparesheni kubwa sana ya jeshi la polisi kote nchini na baada ya wewe kukutana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ikulu.
Ni tukio la mauaji ya Dada mmoja aliyejulikana kwa jina Jonais mzaliwa wa Mwika Kilimanjaro sambamba na mtoto wake ambaye pia alichomwa moto kwenye tukio hilo hilo,ambapo kadhia hiyo haikumsaza binti wake wa kazi😭.

Mheshimiwa Rais sio hayo tu Kuna matukio mengi mno ya kuogofya ambayo yametokea katika sehemu mbalimbali katika nchi yetu ambayo yanaogofya sana.

Kwa niaba ya Watanzania nimekuandika WARAKA huu kukuomba utafakari matendo haya ambayo yanatokea chini ya Utawala wako na ambayo yanatia doa Uongozi wako na ambayo yanafanywa na watu wasiokupenda wewe,wasiolipenda taifa letu na watu ambao wanazikwamisha 4R zako.

Mheshimiwa Rais,ninakuandika WARAKA huu kukuomba japo kidogo utafakari tena na uone umuhimu wa kulifumua jeshi la polisi,ikiwa ni pamoja na kumsimamisha kazi waziri wa mambo ya ndani Eng Msauni kazi kwasababu ya utepetevu huu mkubwa unaendelea kukua kila kuchwapo.

Mheshimiwa Rais,
Asha kumsi Matusi,Pamoja na kuwa Umma ulifedheheshwa na kauli yako uliyoitoa ulipokuwa hapa mkoani Kilimanjaro kwamba kifo ni kifo tunajaribu kuwaza je mathalani kama ingekua haya yameikuta familia yako ungefedheka kwa kiasi gani na kuumia kwa namna ipi,na ndiyo Maana ninakuandika malalamiko yetu uone namna ambavyo watu uliowaamini wanakufelisha na kukukosanisha na wananchi.

MHESHIMIWA Raisi,Na amiri jeshi mkuu na mama kwetu sote tuoneshe upendo wa kimama kwa;

1-Kutoa kauli nzito juu ya matukio haya,(Presidential and as Commander in Chief)

2-Kufanya mabadiliko katika jeshi la Polisi,

3- Anayewajibika kisiasa katika mambo yote ya ndani awajibishwe.

4-Kuunda tume huru ya kimahakama kuchunguza matukio haya ya kupotea kwa watu na kuuwawa.

5-Kufanyike National Dialogue itakayohusisha Makundi yote Wakiongozwa na viongozi wa kidini.

Asante Mheshimiwa Rais.

Wako katika ujenzi wa Taifa.

Revocatus James Ng'oja
Activist,politician and Human Rights Defender
Reha-Rombo-kilimanjaro.
(255764689409 jamesrevocatus0@gmail.com)
26Sep,2024.
 
Back
Top Bottom