Waraka wa wazi kwa waajiriwa wote wanaotamani kufanikiwa kwenye ujasiriamali

Eliah Geofrey Kamwela

Senior Member
Joined
Dec 30, 2018
Posts
184
Reaction score
507
Nimekutana na watu kadhaa wanao anza biashara au miradi, haswa waajiriwa wanao taka kuongeza kipato nje ya ajira zao, wakikata tamaa na kuachana na hab ari ya miradi pale zinapo ibuka changamoto kama Kuibiwa na wafanyakazi wao, hasara na misala mingine.

Wemgi hapa huishia kusema, "Chaaaaa!!! Kama ujasiriamali wenyewe Ndio huu, bora tu Nile mshahara inatosha", na hufikia huu uamuzi si kwamba inatosha kweli, Bali ni kwa kuchoshwa na misala isiyo isha.

Hebu nikupe machache hapa yanayo weza kukusaidia:

1: Kazi unayo ifanya unaisomea kwa wastani wa miaka isiyo pungua 12 hadi 16(ukihesabu toka elimu ya msingi) na huko na huko kote unalipa Ada.
Katika kujiajiri pia kuna ada unayo paswa kulipa, na moja ya aina ya ada ni 'misala' ya hapa na pale!!

2. Matatizo na chqngamoto katika ujasiriamali ndizo zinajenga 'misuli' ya ujasiriamali. Kujenga misuli kunahitaji kunyanyua chuma au vitu vizito, ni kitu kisicho vutia sana, ila Ndio kinampa 'Siksi paki' mbeba vyuma. Vyuma vya ujasiriamali ni Chang a moto ambavyo kadri unazitatua misuli yako inajengeka na unakua na uwezo wa kukabili Mengi magumu.

3. Kama unavyo jifunza kwa bidii ili ufanye kazi ya kuajiriwa, ni muhimu pia kujifunza kwa bidii ili utoboe pia upande huu. Sasa wengi wanataka kuchukua tu Mkopo na kuwekeza , wakipigwa wanaishia kuutukana ujasiriamali kuwa ni ufala wakati wao hawajataka kujifunza.
Ndio maana kwa mfano, nimekuandikia Kitabu cha 'NGUVU YA KUANZA KUELEKEA UHURU WA KIUCHUMI' ambapo nimeeleza namna unavyo weza kuanza na kuendelea na ujasiriamali ukiwa na ajira yako kwa mafanikio. Hutakiwi kuacha kujifunza!!!

3. Katika shule, mwanafunzi mtukutu hukimbia mitihani na werevu hupambana na mitihani hadi wafaulu.
Hata katika miradi, kuzira miradi badala ya kusaka suluhu ni sawa kabisa na mwanafunzi anaye kimbia mitihani!! Huyu hata alalamike vipi, atadharauliwa tu! Wakati unalalamika kwamba mshahara hautoshi, kuna mwingine analipwa kidogo kuliko wewe na anaishi maisha ya utoshelevu kwa kuwa anazalisha!!

4. Mwisho kwa leo, ingawa si kwa umuhimu, ni kuwa upende au usipende, ujasiriamali haukwepeki! Usipo ufanya kwa hiari sasa ukiwa kazini, utalazimika kufanya kwa lazima pale utakapo staafu!!
Huu wa lazima ni hatari kwa kuwa risk ya kufeli kwa ujasiriamali kipindi hicho ni stress zinazo weza hata kufupisha uhai wako.

Wito wangu ni kuwa usiache kujifunza na kufanya na kurekebisha makosa hadi kieleweke, hasa sasa ukiwa na nguvu zako zote.
Kwa leo hebu niishie hapa, nitaendelea wakati mwingine.
#Divine_Solutions_Carrier.
Fb: Eliah Geofrey Kamwela
IG: Eliahkamwela.
 
Mkuu ujumbe wako unanikera kweli. maana ndiyo nimeanza ujasiriamali huku mkoani nikitokea dar(Nimeajiriwa)lakini.

Basi siuzi mpaka mwenyeji wangu amalize.Ndiyo na Mimi niuze. A see huwa nakufa sana moyo. Naomba uvae viatu vyangu unipe ushauri. Ungekuwa Mimi ungefanyaje?? maana hayo uliyoyaandika ukija kwenye uhalisia wake si lelemama.
 
...Ni kweli, ujasiriamali haukwepeki, lakini kwa mwajiriwa ni too risky. Why? Kwasababu anatafuta underkibano. Anawaza asiharibu aliko ajiriwa at the same time aendeshe hiyo miradi yake. Halafu wasichokifahamu wengi katika harakati za kujitafutia sio tu misala wapatayo as individuals, bali hata serikali. Je, serikali inaandaa mazingira gani wezeshi kwa wananchi wake ili wasianguke kizembe kiuchumi. A regime paves the way too.... Misala.... Hii tuichambue upya pia. Rejea sakata la mahindi, na mazao mengine.
 
Hongera sana kwa changamoto mkuu wangu. Tumia muda kutafiti kwanini Wateja wanapenda vya mwenyeji kuliko kwako . Baadhi ya maeneo kuna issue ya kujuana au ukabila, ila ukiboresha Huduma&bidhaa utauza tu.
Pia m train kijana wako kama umemweka, juu ya customer care nzuri kwa Wateja.
 
Ndugu hili andiko nimeliewa vizuri sana kati yamahali ambapo wanadamu hatupapendi ni changamoto, mtu akipata changamoto hukata tamaa vibaya sana hasa kwenye huu ujasiria mali, nakibaya zaidi huwa tunawatisha hata wale wanaotaka kuingia ktk ujasiria mali, naamini ktkt kuto kukata tamaa ndipo mafanikio huja hata kama yakiwa madogo kiasi gani lakini ndiyo hayo uliyo jaaliwa.
 
Kwa sakata la mahindi nafikiri kuna mtu wakushika hilo maana kama mazoea yalikuwa ya njia hii sasa njia ikibadilishwa ghafla nini kitafwata?ni anguko kubwa , hata la mwaka juzi kama sikosei nyanya morogoro ilikuwa hivyo hivyo,shida kubwa serekali zetu zinaanda maelezo mengi lakini yanabakia kwenye makalabrasha na makabati masijala msala unabakia kwetu tuliokopa sasa.
 
Ni kweli kabisa ndugu
 
Kawaida tuu watakuzoea na ww utapata usikute huko wanapenda coz wanakopa sana ndio changamoto hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sawa
 
Ushauri mzuri tena sana

Td mkali
 
Customer care ni muhimu sana unaweza ukawa na bidhaa nzuri ila ukaanguka kwenye customer care
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…