Sasa hiyo mitinga-tinga ina urembo gani? wa-kujikobowa kutaka weupe wasio nao na kujitia nywele za kuji fanya wahindi ambazo sio (natural) yao kabisa.
Mimi kananifurahisha kale ka model ketu kako south africa, hakajikorogi wala hakajitii hizi nywele za maiti. Kako natural na kanapendeza kweli! Tena kwa kuonyesha kuwa uzuri si nywele kanazipiga kipara kabisaaa.
Siku hizi mie nashangaa hawa madada, majority weupe na majority wana nywele za kichina, na nasikia hata makalio wanayaongeza kwa kutumia dawa za kichina? hivi maumbile aliyotupa/wapa Mwenyeezi Mungu tunayasuta? yaani alitukosea kutuweka hivi tulivyo?
Nakumbuka enzi za kawawa alipiga marufuku pasi zote za kuchomea nywele! naona sasa ma-chemical ya kuchomea hizo nywele ndio mabaya kuliko hizo pasi.