Warioba awajibu CCM serikali tatu kulinda Muungano

Warioba awajibu CCM serikali tatu kulinda Muungano

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
katiba.jpg

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ametangaza tarehe rasmi ya kuanza kwa mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya wilaya, huku akiwaonya watu wa kada mbalimbali vikiwemo vyama vya siasa kutokuingilia mikutano hiyo. Vilevile Jaji Warioba alieleza sababu za Tume hiyo kupendekeza Serikali tatu, huku akisisitiza kuwa suala hilo lilikuwepo tangu siku nyingi na Tume iliamua kupendekeza Serikali tatu kwa kuwa ndiyo ilikuwa njia pekee ya kuulinda muungano.

Kauli hiyo inaonekana kama kukijibu Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimependekeza kuwepo kwa Serikali mbili, ikiwa ni siku chache baada ya kutolewa kwa Rasimu ya Katiba. Mikutano hiyo inafanyika baada ya Juni 3 mwaka huu, Tume hiyo kutoa rasimu ya Katiba na kusambaza katika vijiji, mitaa na shehia kwa ajili ya kujadiliwa na wananchi, ambao nao watachangia mawazo yao kwa wawakilishi wao waliowachagua kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana, inaeleza kuwa mikutano hiyo itaanza Julai 12 hadi Septemba 2 mwaka huu na kutakuwa na jumla ya Mabaraza 177, Tanzania Bara 164 na Zanzibar 13.

Tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) kipo katika mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa mapendekezo yake yanapitishwa huku kikitumia wajumbe wa Mabaraza ya Katiba wakiwemo wa ngazi ya mtaa, huku Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye akiwaeleza wajumbe wa mabaraza ya Katiba jijini Dar es Salaam juzi azma ya chama hicho kuwa na rasimu mbadala.

Wakati CCM wakieleza hayo, Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inakutana leo na kesho katika kikao cha dharura jijini Dar es Salaam ili kujadili pamoja na mambo mengine Rasimu ya Katiba Mpya.

Naye Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, anayemaliza muda wake, Profesa Issa Shivji, Juni 21 mwaka huu alisema kama Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano ikikubaliwa bila mabadiliko makubwa itasababisha kuvunjika kwa Muungano.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Jaji Warioba alisema hairuhusiwi kwa makundi, vyama vya siasa au mtu yeyote kuingia katika mabaraza hayo kwa lengo la kushawishi kukubaliwa na maoni ya aina fulani. Alitoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa swali na gazeti hili, juu ya taarifa zilizopo kwamba baadhi ya vyama vya siasa nchini vimeandaa rasimu zao kwa lengo la kuwashawishi wajumbe wa mabaraza kupitisha maoni yao.

“Mikutano na Mabaraza ya Katiba siyo ya kupiga kura bali ni kujadili na kutoa hoja ambazo zitakuwa na msingi kwa masilahi ya taifa na siyo kutetea masilahi ya kundi au watu fulani,” alisema Jaji Warioba na kuongeza;

“Hilo la vyama kuandaa rasimu zao kwa lengo la kuingilia utaratibu huu sijalisikia, ila kikubwa ni kwamba si ruhusa kuingilia mchakato huu kwa sababu utafanyika kwa mujibu wa taratibu zilizopo,” alisema Warioba na kusisitiza; “Wananchi watoe maoni ambayo yatasaidia kuiboresha rasimu iliyotolewa kwa kuweka mbele masilahi ya taifa na kuepuka ubinafsi wa mtu mmojammoja au makundi ya aina yeyote.”

Alisema Tume yake itapokea maoni na mapendekezo yote ambayo yatakuwa na lengo la kuiboresha rasimu ambayo itaweka umoja wa kitaifa na siyo kuwagawa Watanzania.
“Tunazidi kuwaomba wasiishie kutoa maoni na hofu zao, bali wasaidie tume kutoa mapendekezo ambayo yataisaidia tume katika kazi yake ya kuwapatia Watanzania katiba iliyokuwa bora,” alisema.

Akizungumzia sababu za kupendekeza Serikali tatu, Warioba alisema kama wangependekeza Serikali ya mkataba ilikuwa lazima kuvunjwa kwa muungano na kuwepo kwa Serikali mbili ambazo baadaye zingekaa na kuamua kushirikiana ama laa, jambo ambalo lingekuwa gumu.

“Wapo waliotaka Serikali mbili, lakini katika hilo wapo waliosema kuwa Zanzibar wana wimbo wao wa taifa na bendera, pia wamejiunga na OIC na hata Katiba yao inasema kuwa Zanzibar ni nchi, Watanganyika nao wangeanza kuhoji Tanganyika iko wapi,” alisema.

Alisema ndiyo maana walipendekeza Serikali tatu na kwamba kama wangeamua kuvunja muungano operesheni za sheria tulizonazo zingewatenganisha wananchi, kama soko la pamoja, sheria ya ardhi, mwingiliano wa pande mbili, biashara, matibabu na shule.

Alisema Serikali tatu ndiyo suluhisho la kudumisha muungano kuliko Serikali moja au mbili, na kwamba katika kura ya maoni jambo la uwepo wa Serikali tatu linategemea uamuzi wa viongozi.

Akizungumzia idadi ya wajumbe wa mabaraza hayo alisema Tanzania Bara kutakuwa na wajumbe 18,174 na Zanzibar 1159 na kwamba tume itatumia siku 54 kuendesha Mabaraza ya Katiba nchi nzima.

“Ili kuweza kufika sehemu zote za nchi, tume imejigawa katika makundi 14 na kila kundi litaendesha mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya wilaya katika Mamlaka za Serikali za mitaa 12 au 13 na mikutano itafanyika kwa siku tatu,” alisema.

Alisema mikutano ya kwanza itafanyika katika mikoa ya Kagera, Shinyanga, Mara, Kigoma, Tabora, Lindi, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mkoa wa Kusini Unguja, Mbeya, Rukwa, Mtwara na Njombe.

 
Ahsante warioba chapa kazi tulokutuma wavuja jasho wa nchi hii pale ulipo tusimamisha mchana tena jua likiwa kali tukikusubiri uje tukupe mawazo achana na hao wavuruga nchi
 
Ahsante warioba chapa kazi tulokutuma wavuja jasho wa nchi hii pale ulipo tusimamisha mchana tena jua likiwa kali tukikusubiri uje tukupe mawazo achana na hao wavuruga nchi

Na imani hata wazenj wanakubalaina na serikali tatu ingawa viongozi wa CCM wako kinyume chake.
 
Na imani hata wazenj wanakubalaina na serikali tatu ingawa viongozi wa CCM wako kinyume chake.


Tatizo viongozi wengi wa CCM huwa wanafanya kazi kwa maslahi yao binafsi na CCM. Wananchi baadaye!!

Kwa sasa jamaa wanaangalia beyond 2015 .......... ni namna gani watalinda vyeo vyao!!
 
Chapa kazi mzee wariaba kuna watanzania milion 44 wako nyuma yako na wenzako.Kwa taarifa yako mzee kama ulikuwaq unasubiri kuwa utaacha legacy gani duniani na hasa tanzania ni kukubalui serikali tatu. Kaza buti baba achana na ma-ccm YAMECHANGANYIKWA KITUMBUA CHAO KWISA CHAFUKA MCHANGA
 
Serikali tatu ni nzuri Warioba kaza buti. Ila nina wazo jingine kama serikali tatu hazikubaliki ni heri tuwe na Serikali moja ya muungano kuliko kuwa na serikali mbili kama ilivyo sasa au kama mapendekezo ya CCM.
Heri wote tukose Tangayika tukose Serikali na Zanzibar wakose tuwe nayo ya muungano. Otherwise naunga mkono hoja ya Serikali TATU.
 
CCM wameshateka mchakato mzima wa katiba mpya. Juzi bwana mdogo Jerry Slaa alikuwa Mkoani Simiyu katika wilaya ya Bariadi na waliwaita wajumbe wote wa mabaraza ya kata walio wanachama wa ccm na kuwapatia maagizo, maazimio na msimamo wa ccm na kuwalazimisha hao wajumbe kuwa ni lazima watetee serikali mbili, makuu wa wilaya na mkoa na mambo mengine ya limagamba.. Cha kutisha zaidi ni kuwa anasema hayo ndo maagizo kutoka kwa Mwenyekiti wa chama Taifa
 
Hii idea ya serikali tatu naipenda.
Ni njia rahisi na isiyohitaji nguvu kuachana na wapemba na waunguja.
 
Hii ikipita naona njia ni nyeupe kwa 'uhuru' wa waznz mwanzo wa mwisho wa Muungano.
 
KWELI CCM Wameishiwa kweli wanaanza kupuuza wananchi na maoni yao na hii mimi nimeipenda maana wanajiandalia kaburi lefu sana kwa ajili yao wenyewe maana nipo hapa Ngaramtoni-Arusha wenyeviti wa vijiji na vitongoji wanahangahika wako kwenye vikao vya kamati ya siasa ili kuwaelekeza wajumbe wa mabaraza cha kusema kwenye rasimu. Warioba komaa na hawa jamaa ni wepesi mno,
 
Yan CCM kweli noma. Hapa ilibidi kuwepo na kupiga kura za maoni. Yan kila mwananchi apige kura kama anautaka Muungano au hautaki. Zoezi hilo likikamilika ndio tuletewe Rasimu ya katiba ya Tanganyika. Pasipo na hvyo Tutaendelea kudanganywa na CCM hadi MUNGU atakaporudi kuihukumu Dunia na CCM. Mm nashangaa mtu aliyeuleta Muungano amekufa tayari leo hii Viongozi wanajiumauma.
 
Li-ccm ni mauzauza tu hawana lolote. Wazanzibar kamwe hawatakubali serikali mbili au moja, wao wanataka serikali tatu tu vinginevyo muungano uvunjike. Huku Tz bara bado kuna vibaraka vingi sana vya liccm tofauti na Zenj ambako watu walishaacha ujinga ujinga wa liccm.
 
katiba.jpg


Vilevile Jaji Warioba alieleza sababu za Tume hiyo kupendekeza Serikali tatu, huku akisisitiza kuwa suala hilo lilikuwepo tangu siku nyingi na Tume iliamua kupendekeza Serikali tatu kwa kuwa ndiyo ilikuwa njia pekee ya kuulinda muungano.



Shida ninayoiona Warioba na Tume yake wanataka kutuingizia hasara ya mabilioni ya Pesa iliwapate kuifanya kazi hii mara ya Pili maana kwa jinsi Rasimu hii ilivyo (Serikali Tatu) huhitaji kuwa Profesa kunga'mua kitakachotokea mbele ya safari na haitapita Mwaka .

Hebu namshauri Warioba na Tume yake wapitie Ibara hii na waje na majibu maana nimejaribu kupitia maeneo mengi katika Rasimu na sijaona taasisi au mamlaka itakayolinda kiapo hii pale Raisi wa Tanganyika au Zanzibar atakapokaidi kutekeleza/kushiriki shughuli za Muungano.

Mifano hii ipo wazi hadi dakika hii naandika maneno haya Zanzibar wamekwisha funja Katiba iliyopo.

Wajibu wa

kulinda
Muungano
66.-(1) Bila ya kuathiri wajibu wa kila raia kwa mujibu wa Katiba
hii, viongozi wakuu wenye mamlaka ya utendaji katika Jamhuri ya
Muungano waliotajwa katika Ibara ndogo ya (3) watawajibika, kila mmoja
wao katika kutekeleza madaraka waliyopewa kwa mujibu wa Katiba hii au
Katiba za Washirika wa Muungano kuhakikisha kuwa analinda, kuimarisha
na kudumisha Muungano.
(2) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara ndogo ya (1), kila
mmojawapo wa viongozi wakuu waliotajwa katika Ibara ndogo ya (3),
kabla ya kushika madaraka yake ataapa kuutetea na kuudumisha
Muungano kwa mujibu wa Katiba hii.
(3) Viongozi Wakuu wanaohusika na masharti ya Ibara hii ni:
(a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(b) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(c) Rais wa Tanzania Bara; na
(d) Rais wa Zanzibar.
 
Hii katiba sijui itafika kweli ...maaana kila mtu kulalamika...mkuu analalamika....waziri analalamika, wa mkoa analalamika, wa wilaya analalamika, mwenyekiti analalamika,katibu vilevile, mweka hazina ndo usiseme, naibu katibu analia, wajumbe wameshikwa butwaa, wananchi wamechanganykiwa! sasa kweli katiba itafika.....????
 
Back
Top Bottom