Warioba Kuchafua hali ya Hewa Bungeni

Warioba Kuchafua hali ya Hewa Bungeni

Weston Songoro

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2014
Posts
2,793
Reaction score
1,085
Wadau, mtu akitonywa jambo ambalo lina maslahi ya kitaifa, ni vema akaliweka hadharani ili kupata tafakuri ya pamoja.

Ni kwamba mdau wangu ambaye yupo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo muda si mrefu itamaliza kazi yake, amenitonya kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba atatoa hotuba ambayo kwa maoni yake amesema kuwa huenda ikavuruga maridhiano yanayoendelea Bungeni hivi sana. Kwamba, Warioba kama sheria ya mabadiliko ya Katiba inavyomtaka, atawasilisha kwenye Bunge Maalum nakala za Rasimu ya Pili ya Katiba. Hii ni baada ya Bunge Maalum kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete. Mtonyaji amenifahamisha kuwa Warioba atawasilisha Rasimu hiyo siku hiyo hiyo ambayo Rais atalihutubia Bunge. Aidha, mtonyaji amenidokeza kuwa Kabla ya kukabidhi Rasimu hiyo kwa Bunge Maalum, warioba atahutubia Bunge. Sina hakika kama neno kuhutubia ni mahala pake, pengine ingetosha kusema kuwa atasema machache kabla ya kukabidhi.

Wadau, kilichonifanya nije mbio humu jukwaani ni baada ya kusikia dondooo za yale atakayoongea Warioba ambaye siku zote nilikuwa namheshimu kwa kujali maslahi ya taifa ila katika hili, nina hakika hata wadau wengi watamshangaa.
Miongoni mwa atakayosema warioba ni pamoja na haya yafuatayo

  • Atazungumzia umuhimu wa kura ya Siri kwa wajumbe. Kwamba warioba atatoa maelezo ambayo yana lengo la kuwashawishi wajumbe waunge mkono kura ya Siri. Binafsi sipingi matumizi ya kura hiyo bali hofu yangu ni kuchafuka kwa hali ya hewa. Kama mjuavyo kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Kamati ya Maridhiano ambayo imeundwa na Mwenyekiti wa Muda, mzee Kificho. Pia leo tumepata taarifa kuwa zoezi la kufikia muafaka juu ya namna ya kufanya maamuzi Bungeni linaendelea. Sasa huyu Babu Warioba sijui kitu gani kinamshawishi aende kuzungumza jambo hilo Bungeni?

  • Jambo jingine ambalo Warioba atazungumza ni kuwaeleza wajumbe juu ya umuhimu wa Serikali Tatu. Warioba anataka kulazimisha wajumbe wote waamini kuwa Tume ilikuwa sahihi kupendekeza mfumo wa serikali tatu. Katika hili, pia sina tatizo bali wasiwasi wangu ni namna ya uwasilishaji wake. Ninaamini kuwa wabunge wana akili timamu na hawahitaji mtu kuwasemea uzuri au ubaya wa muundo wa Serikali Tatu. Je wale wanaopendekeza muundo wa serikali moja, mbili, nne na tano nani atawasemea?

Mtonyaji pia amenidokeza kuwa Warioba atatoa hotuba ndefu ambayo itabeba maudhui ya mtazamo wake juu ya mchakato wa Katiba. Binafsi, namshauri Mzee Warioba aangalie upepo unavyoenda. Kwa sasa si wakati wa kushindana. Maridhiano ni jambo muhimu sana. Mwanzo walioanza nao wabunge ni mzuri. Warioba akabidhi tu na asitumie muda mwingi kama ambavyo amepanga kuwachanganya Watanzania na kupandikiza chuki za kuvurugana.

Ni hayo tu wakuu kwa leo. Siku nikitonywa jambo jingine nitakuja fasta kuwatonya.
 
ingetosha tu kusema kuwa nimajungu ya ufipani kwa babu wa gongo:A S thumbs_up::A S thumbs_up:
 
Umejiunga juzi hata mwezi huna na tayari ni Senior Expert Member!!! Tena umejiunga wakati Bunge Maalumu ndio kwanza linaanza na inaonekana unakerwa sana na Warioba. Vipi yakhe, umejiunga kwa malengo maalumu? Just curious!!!
 
Gamba lako lina tofauti kidogo na la Chenge maana la kwako limekwama miguuni!
 
Warioba anaenda kuzungumzia mawazo yake au mawazo ya wananchi wengi waliosema serikali3? Kuhusu kura ya siri au wazi, sheria ya mabadiliko ya katiba inazungumza nini au Warioba anaenda na sheria yake binafsi?
 
Kwa nini warioba anataka kulazimisha matakwa yake aache wajumbe wapime na kuamua kipi chema au kipimhakifai kwenye rasimu yake.
 
Umejiunga juzi hata mwezi huna na tayari ni Senior Expert Member!!! Tena umejiunga wakati Bunge Maalumu ndio kwanza linaanza na inaonekana unakerwa sana na Warioba. Vipi yakhe, umejiunga kwa malengo maalumu? Just curious!!!
Mkuu, katika hili, hakuna cha kujiunga juzi wala jana. Ninapopata taarifa lazima niwatonye. Yasije yakawa yale ya Zitto ndanimya CDM
 
Warioba anaenda kuzungumzia mawazo yake au mawazo ya wananchi wengi waliosema serikali3? Kuhusu kura ya siri au wazi, sheria ya mabadiliko ya katiba inazungumza nini au Warioba anaenda na sheria yake binafsi?
Mkuu, ni dhahiri kuwa anaenda kuzungumzia mawazo yake na si ya wananchi. Wqnanchi hatujapiga kura kuamua aina ya serikali tuitakayo
 
Wadau, mtu akitonywa jambo ambalo lina maslahi ya kitaifa, ni vema akaliweka hadharani ili kupata tafakuri ya pamoja.

Ni kwamba mdau wangu ambaye yupo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo muda si mrefu itamaliza kazi yake, amenitonya kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba atatoa hotuba ambayo kwa maoni yake amesema kuwa huenda ikavuruga maridhiano yanayoendelea Bungeni hivi sana. Kwamba, Warioba kama sheria ya mabadiliko ya Katiba inavyomtaka, atawasilisha kwenye Bunge Maalum nakala za Rasimu ya Pili ya Katiba. Hii ni baada ya Bunge Maalum kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete. Mtonyaji amenifahamisha kuwa Warioba atawasilisha Rasimu hiyo siku hiyo hiyo ambayo Rais atalihutubia Bunge. Aidha, mtonyaji amenidokeza kuwa Kabla ya kukabidhi Rasimu hiyo kwa Bunge Maalum, warioba atahutubia Bunge. Sina hakika kama neno kuhutubia ni mahala pake, pengine ingetosha kusema kuwa atasema machache kabla ya kukabidhi.

Wadau, kilichonifanya nije mbio humu jukwaani ni baada ya kusikia dondooo za yale atakayoongea Warioba ambaye siku zote nilikuwa namheshimu kwa kujali maslahi ya taifa ila katika hili, nina hakika hata wadau wengi watamshangaa.
Miongoni mwa atakayosema warioba ni pamoja na haya yafuatayo

  • Atazungumzia umuhimu wa kura ya Siri kwa wajumbe. Kwamba warioba atatoa maelezo ambayo yana lengo la kuwashawishi wajumbe waunge mkono kura ya Siri. Binafsi sipingi matumizi ya kura hiyo bali hofu yangu ni kuchafuka kwa hali ya hewa. Kama mjuavyo kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Kamati ya Maridhiano ambayo imeundwa na Mwenyekiti wa Muda, mzee Kificho. Pia leo tumepata taarifa kuwa zoezi la kufikia muafaka juu ya namna ya kufanya maamuzi Bungeni linaendelea. Sasa huyu Babu Warioba sijui kitu gani kinamshawishi aende kuzungumza jambo hilo Bungeni?

  • Jambo jingine ambalo Warioba atazungumza ni kuwaeleza wajumbe juu ya umuhimu wa Serikali Tatu. Warioba anataka kulazimisha wajumbe wote waamini kuwa Tume ilikuwa sahihi kupendekeza mfumo wa serikali tatu. Katika hili, pia sina tatizo bali wasiwasi wangu ni namna ya uwasilishaji wake. Ninaamini kuwa wabunge wana akili timamu na hawahitaji mtu kuwasemea uzuri au ubaya wa muundo wa Serikali Tatu. Je wale wanaopendekeza muundo wa serikali moja, mbili, nne na tano nani atawasemea?

Mtonyaji pia amenidokeza kuwa Warioba atatoa hotuba ndefu ambayo itabeba maudhui ya mtazamo wake juu ya mchakato wa Katiba. Binafsi, namshauri Mzee Warioba aangalie upepo unavyoenda. Kwa sasa si wakati wa kushindana. Maridhiano ni jambo muhimu sana. Mwanzo walioanza nao wabunge ni mzuri. Warioba akabidhi tu na asitumie muda mwingi kama ambavyo amepanga kuwachanganya Watanzania na kupandikiza chuki za kuvurugana.

Ni hayo tu wakuu kwa leo. Siku nikitonywa jambo jingine nitakuja fasta kuwatonya.
Mimi nimesikia kuwa hotuba yake itakuwa na page zaidi ya 80 ambayo amepanga kuisoma kwa mda wa masaa 8.
 
Kuna kingine? Kubwa hapa ww ni Gamba tu basi...
 
Mtoa mada nimekupata vizuri, nahisi kama mzee walioba atakwenda kuwakilisha maoni ya wananchi na sio ya kwake hivyo sio busara kumfunga mdomo.
ukweli unaujua serekali moja haiwezekani na mbili ndo matatizo tinayaona na kama hawapendi tatu basi kila mtu aende kwake tukae kwa amani na ushilokiano bola.
 
Kwa nini warioba anataka kulazimisha matakwa yake aache wajumbe wapime na kuamua kipi chema au kipimhakifai kwenye rasimu yake.

Asante kwa kuwa muwazi leo, ya kwamba wewe sio mmoja wa wajumbe wa bunge maalumu la katiba.
 
ccm iache kutapatapa. na iache kutulqzimishia mawazo.
wa tanzania tunahitaji katiba nzuri isiyokuwa na makandokando hususani kwenye muundo wa serikali.
mimi binafsi ni muumini wa serikali moja tu ya tanganyika. wazanzibari waachwe huru wajitegemee
 
Jamani watanzania imefika wakati sasa hatuoni wala hatusikii, hivi SERIKALI TATU ni maoni ya tume au wananchi? Tume ilienda kwa wananchi na wananchi wakasema kilicholetwa na tume na kama ni kutetea ni haki yake kama mwenyekiti maana ni nani asiyeipenda kazi aliyotumwa?
 
Mbona una panic...acha atoe maoni na watu wachambue...okay mie napendekeza kura ya siri.
Serikali mbili kwa sasa.. ingawa ningependa iwe moja sema tu hali hairuhusu kwa sasa kutokana na uchu wa madaraka.
 
Back
Top Bottom