Warioba Kuchafua hali ya Hewa Bungeni

mleta mada hujielewi mbona jaji Warioba ataongea vitu vya msingi kwa taifa ulitaka aseme nini
 
Kura ya Siri + serikali tatu = Wananchi

Kura ya Wazi + serikali 2 = CCM

So, hoja iliyoletwa na mleta mada hii ni kumpinga warioba na umuhimu wa kupiga kura ya Siri na kuwa na serikali tatu, ambapo sio hoja binafsi
ya Warioba bali ni matakwa na maoni ya WANANCHI walio wengi!

Aisee masisiem mtalia mwaka huu wallah..
 
Mtoa mada unamchecheto. Mkurupuko.na pia hueleweki lengo lako. Hotuba ya warioba nani kakupa?
 
Kiherere cha nini! au anataka kumhujumu Warioba? Yeye kukabidhi nakala ya rasimu ya pili ya katiba ipo kisheria, na kuhutubia ni lazima kwani hataifanya kazi hiyo kibubu. Katika hotuba yake ni dhahri kuwa atazungumzia kwa ufupi kuhusu mambo muhimu yaliyomo katika rasimu hiyo. Na atakayozungumza ndiyo muhtasari wa matakwa ya raia wengi waliochangia. Kama matakwa ya wananchi yatakinzana na mahitaji ya wajumbe wa bunge la katiba, ama yatasigana na matakwa ya baadhi ya vyama vya siasa ama makundi mengine, hiyo haimuhusu yeye wala tume yake.

Ila nitalishangaa bunge hilo maalum ya kutunga katiba km litakiuka mambo muhimu yaliyopendekezwa na wananchi kwa ujumla wao, hususan kuhusu upigwaji wa kura za siri, muundo wa serikali tatu, na wabunge kutokuwa mawaziri.
 
Mkuu, kwani suala la upigaji kura ni moja ya mapendekezo ya wananchi? Na je wale wanaopendekeza kinyume chake si wananchi? Naona kuna watu wanatumia vibaya neno mwananchi
 
Watu wengine huwa najiuliza sana, mleta post Nina hakika ukimuona barabarani anatembea Ni ngumu kubaini jinsia Yake, Kama asivyoeleweka mwilini mwake Nahisi HATA anachokiandika anakijua Yeye mwenyewe
 
Hii thread mbona imerudiwa na watu wawili tofauti Halafu the same content! Au neo multiple ID!??
 

Kwenye maneno hayo yenye RED sijakuelewa kabisa.....yawezekana hukumnukuu vizuri mtonyaji
 
Hii ni habari ya kutunga haina ukweli hata chembe
 
Haya uliyoandika hapa (tazama maandishi ya blue) inaonyesha huna akili, Warioba hajapendekeza rasmu, haya ni matakwa ya wananchi, acha ujinga wa ccm hapa, ccm itakwisha ila taifa litaendelea na watu wake, tena nasisitiza uache utaahira wako


Warioba anataka kulazimisha wajumbe wote waamini kuwa Tume ilikuwa sahihi kupendekeza mfumo wa serikali tatu. Katika hili, pia sina tatizo bali wasiwasi wangu ni namna ya uwasilishaji wake. Ninaamini kuwa wabunge wana akili timamu na hawahitaji mtu kuwasemea uzuri au ubaya wa muundo wa Serikali Tatu. Je wale wanaopendekeza muundo wa serikali moja, mbili, nne na tano nani atawasemea?
 

Watanzania tuna maneno maneno sana, na kupeana hofu kusikokuwa na msingi. Suala la uthubutu hatuna kabisa! Huu woga wa kinafiki utaisha lini?
 
Mkuu nadhani aliyekutonya alidhani anakabidhi siri kwenye mikono salama kumbe
ni sawa na mbuzi kumkabidhi chui mtoto wake.
Binafsi naamini Walioba kama m/kiti wa tume ana wajibu wa kutetea hoja za tume vinginevyo ataonekana ametuma fedha za umma kufanya vitu visivyo na tija kwa taifa.
Pia Walioba kama mzalendo wa nchi hii lazima atoe onyo juu ya maafa ambayo yatatokea endapo bunge litapuuza
maoni ya tume ambayo ndio ilipewa dhamana ya kuwahoji watanzania kuhusu mchakato wa katiba.
Namuunga mkono Walioba coz Wajumbe wa bunge maalum siyo vyombo vya udongo kwamba akiwashika vibaya watapasuka,
Ni heri awape ukweli,kama katiba mpya itashindikana tutaendelea na ya zamani kama alivyotangulia kusema rais.
 
Kwa nini warioba anataka kulazimisha matakwa yake aache wajumbe wapime na kuamua kipi chema au kipimhakifai kwenye rasimu yake.

Na mawazo kama haya naskia na wewe ni mjumbe mmojawao pale mjengoni..!uso umeumbwa na aibu jamani hebu jitendeeni haki japo kidogo.
 

From time immemorial kura ya siri katika masuala nyeti ndio huwa inatumika. CCM wana wasiwasi gani? JIBU: Wanajua kuwa wabunge na waumini wao hawataki kura ya wazi. Hivyo wanataka kura ya wazi kuwa-spoti watakao kwenda na kinyume na msimamo wa JK, Wasira, and a few others.

Erd ya pilki, Warioba alichokusanya ni matakwa/maoni ya wananchi, hivyo humtendei haki kuwa anataka ku-impose serikali tatu. Ni hato.
 

Wasiwasi wako tuuuuuuu
 
Yeye km Mwenyekiti ana haki ya kutetea kile kilichomo ndani ya Rasimu....!!hata km watanzania wangesema wanataka Serikali moja yy angeenda kulitete hilo.....kwa hiyo hapo hakutakuwa na tatizo kwa Warioba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…