warioba kuchafua hali ya hewa bungeni

warioba kuchafua hali ya hewa bungeni

hugochavez

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2013
Posts
1,907
Reaction score
1,009
Warioba Kuchafua hali ya Hewa Bungeni

Wadau, mtu akitonywa jambo ambalo lina maslahi ya kitaifa, ni vema akaliweka hadharani ili kupata tafakuri ya pamoja.

Ni kwamba mdau wangu ambaye yupo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo muda si mrefu itamaliza kazi yake, amenitonya kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba atatoa hotuba ambayo kwa maoni yake amesema kuwa huenda ikavuruga maridhiano yanayoendelea Bungeni hivi sasa. Kwamba, Warioba kama sheria ya mabadiliko ya Katiba inavyomtaka, atawasilisha kwenye Bunge Maalum nakala za Rasimu ya Pili ya Katiba. Hii ni baada ya Bunge Maalum kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete. Mtonyaji amenifahamisha kuwa Warioba atawasilisha Rasimu hiyo siku hiyo hiyo ambayo Rais atalihutubia Bunge. Aidha, mtonyaji amenidokeza kuwa Kabla ya kukabidhi Rasimu hiyo kwa Bunge Maalum, warioba atahutubia Bunge. Sina hakika kama neno kuhutubia ni mahala pake, pengine ingetosha kusema kuwa atasema machache kabla ya kukabidhi.

Wadau, kilichonifanya nije mbio humu jukwaani ni baada ya kusikia dondooo za yale atakayoongea Warioba ambaye siku zote nilikuwa namheshimu kwa kujali maslahi ya taifa ila katika hili, nina hakika hata wadau wengi watamshangaa.
Miongoni mwa atakayosema warioba ni pamoja na haya yafuatayo
Atazungumzia umuhimu wa kura ya Siri kwa wajumbe. Kwamba warioba atatoa maelezo ambayo yana lengo la kuwashawishi wajumbe waunge mkono kura ya Siri. Binafsi sipingi matumizi ya kura hiyo bali hofu yangu ni kuchafuka kwa hali ya hewa. Kama mjuavyo kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Kamati ya Maridhiano ambayo imeundwa na Mwenyekiti wa Muda, mzee Kificho. Pia leo tumepata taarifa kuwa zoezi la kufikia muafaka juu ya namna ya kufanya maamuzi Bungeni linaendelea. Sasa huyu Babu Warioba sijui kitu gani kinamshawishi aende kuzungumza jambo hilo Bungeni?

Jambo jingine ambalo Warioba atazungumza ni kuwaeleza wajumbe juu ya umuhimu wa Serikali Tatu. Warioba anataka kulazimisha wajumbe wote waamini kuwa Tume ilikuwa sahihi kupendekeza mfumo wa serikali tatu. Katika hili, pia sina tatizo bali wasiwasi wangu ni namna ya uwasilishaji wake. Ninaamini kuwa wabunge wana akili timamu na hawahitaji mtu kuwasemea uzuri au ubaya wa muundo wa Serikali Tatu. Je wale wanaopendekeza muundo wa serikali moja, mbili, nne na tano nani atawasemea?

Mtonyaji pia amenidokeza kuwa Warioba atatoa hotuba ndefu ambayo itabeba maudhui ya mtazamo wake juu ya mchakato wa Katiba. Binafsi, namshauri Mzee Warioba aangalie upepo unavyoenda. Kwa sasa si wakati wa kushindana. Maridhiano ni jambo muhimu sana. Mwanzo walioanza nao wabunge ni mzuri. Warioba akabidhi tu na asitumie muda mwingi kama ambavyo amepanga kuwachanganya Watanzania na kupandikiza chuki za kuvurugana.

Ni hayo tu wakuu kwa leo. Siku nikitonywa jambo jingine nitakuja fasta kuwatonya.
 
Warioba ni mtoa hoja ambayo ndio rasimu ya pili ya katiba ambayo ndio maoni ya wananchi.....Hicho ndio atakachopresent na ofcourse ni lazima akifafanue kwa kadri ya uwezo wake ili wajumbea waelewe, kabla ya kuijadili hiyo rasimu. Hawezi kukabidhi tu halafu akaondoka ! Lazima afanye presentation pia ! Hilo liko kisheria ndugu yangu na vile vile kwenye kanuni imeshapitishwa kwamba atapresent na hakuna mtu atakayeruhusiwa kumkatiza wakati anafanya presentation !

Kwa hiyo kama wewe au wengine hampendi Warioba apresent, itabidi mvumilie tu, kwa sababu option ya kumzuia haipo !. Option pekee mliyonayo nyie binafsi ni kutomsikiliza kama mtapenda kufanya hivyo !

Issue ya kura ya siri au wazi sidhani kama ataongelea hilo, kwa sababu hilo halimhusu na anajua na vile vile na nina amini ana busara ya kutokuingilia mambo yasiyomhusu !

Warioba Kuchafua hali ya Hewa Bungeni

Wadau, mtu akitonywa jambo ambalo lina maslahi ya kitaifa, ni vema akaliweka hadharani ili kupata tafakuri ya pamoja.

Ni kwamba mdau wangu ambaye yupo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo muda si mrefu itamaliza kazi yake, amenitonya kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba atatoa hotuba ambayo kwa maoni yake amesema kuwa huenda ikavuruga maridhiano yanayoendelea Bungeni hivi sana. Kwamba, Warioba kama sheria ya mabadiliko ya Katiba inavyomtaka, atawasilisha kwenye Bunge Maalum nakala za Rasimu ya Pili ya Katiba. Hii ni baada ya Bunge Maalum kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete. Mtonyaji amenifahamisha kuwa Warioba atawasilisha Rasimu hiyo siku hiyo hiyo ambayo Rais atalihutubia Bunge. Aidha, mtonyaji amenidokeza kuwa Kabla ya kukabidhi Rasimu hiyo kwa Bunge Maalum, warioba atahutubia Bunge. Sina hakika kama neno kuhutubia ni mahala pake, pengine ingetosha kusema kuwa atasema machache kabla ya kukabidhi.

Wadau, kilichonifanya nije mbio humu jukwaani ni baada ya kusikia dondooo za yale atakayoongea Warioba ambaye siku zote nilikuwa namheshimu kwa kujali maslahi ya taifa ila katika hili, nina hakika hata wadau wengi watamshangaa.
Miongoni mwa atakayosema warioba ni pamoja na haya yafuatayo
Atazungumzia umuhimu wa kura ya Siri kwa wajumbe. Kwamba warioba atatoa maelezo ambayo yana lengo la kuwashawishi wajumbe waunge mkono kura ya Siri. Binafsi sipingi matumizi ya kura hiyo bali hofu yangu ni kuchafuka kwa hali ya hewa. Kama mjuavyo kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Kamati ya Maridhiano ambayo imeundwa na Mwenyekiti wa Muda, mzee Kificho. Pia leo tumepata taarifa kuwa zoezi la kufikia muafaka juu ya namna ya kufanya maamuzi Bungeni linaendelea. Sasa huyu Babu Warioba sijui kitu gani kinamshawishi aende kuzungumza jambo hilo Bungeni?

Jambo jingine ambalo Warioba atazungumza ni kuwaeleza wajumbe juu ya umuhimu wa Serikali Tatu. Warioba anataka kulazimisha wajumbe wote waamini kuwa Tume ilikuwa sahihi kupendekeza mfumo wa serikali tatu. Katika hili, pia sina tatizo bali wasiwasi wangu ni namna ya uwasilishaji wake. Ninaamini kuwa wabunge wana akili timamu na hawahitaji mtu kuwasemea uzuri au ubaya wa muundo wa Serikali Tatu. Je wale wanaopendekeza muundo wa serikali moja, mbili, nne na tano nani atawasemea?

Mtonyaji pia amenidokeza kuwa Warioba atatoa hotuba ndefu ambayo itabeba maudhui ya mtazamo wake juu ya mchakato wa Katiba. Binafsi, namshauri Mzee Warioba aangalie upepo unavyoenda. Kwa sasa si wakati wa kushindana. Maridhiano ni jambo muhimu sana. Mwanzo walioanza nao wabunge ni mzuri. Warioba akabidhi tu na asitumie muda mwingi kama ambavyo amepanga kuwachanganya Watanzania na kupandikiza chuki za kuvurugana.

Ni hayo tu wakuu kwa leo. Siku nikitonywa jambo jingine nitakuja fasta kuwatonya.
 
hata wewe hueleweki-maana unasema unatutonya halafu hapohapo unaanza kupinga hata ambacho mzee Warioba hajazungumza-
Nenda kwa Nnape mkadanganyane.
 
Una ufinyu wa fikra kama wabunge wa chama tawala. Kwani serikalu tatu ni dhambi?? Anza zomeazomea kama mluvyo zowea.
 
Nadhani umesema vema kuwa sheria inamtaka awasilishe rasimu bungeni. Sasa nakushangaa unapotaka kumfunga mdomo. Ana wajibu wa kisheria lakini pia ana wajibu kama mtanzania. Sioni shida akizungumzia lolote ktk hayo uliyoyasema
 
Warioba si mmoja washiriki wa hilo Bunge.....Yeye analeta rasimu kama wananchi walivyoonyesha msimamo....

Baada ya hapo, hao waliopo hapo Bungeni, ndio watakaomua, kukubali maoni ya wananchi au kuridhiana na kuyaacha na kuweka ya kwao !

Warioba anafanya presentation ya mawazo ya wananchi na kuondoka. Kuridhiana au kutokuridhiana kwa wabunge wa bunge maalumu, hakumhusu !

Mkuu, karika hili suala la Katiba, maridhiano ni jambo la msingi. Si kama anavyofanya huyu babu
 
Warioba Kuchafua hali ya Hewa Bungeni

Wadau, mtu akitonywa jambo ambalo lina maslahi ya kitaifa, ni vema akaliweka hadharani ili kupata tafakuri ya pamoja.

Ni kwamba mdau wangu ambaye yupo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo muda si mrefu itamaliza kazi yake, amenitonya kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba atatoa hotuba ambayo kwa maoni yake amesema kuwa huenda ikavuruga maridhiano yanayoendelea Bungeni hivi sasa. Kwamba, Warioba kama sheria ya mabadiliko ya Katiba inavyomtaka, atawasilisha kwenye Bunge Maalum nakala za Rasimu ya Pili ya Katiba. Hii ni baada ya Bunge Maalum kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete. Mtonyaji amenifahamisha kuwa Warioba atawasilisha Rasimu hiyo siku hiyo hiyo ambayo Rais atalihutubia Bunge. Aidha, mtonyaji amenidokeza kuwa Kabla ya kukabidhi Rasimu hiyo kwa Bunge Maalum, warioba atahutubia Bunge. Sina hakika kama neno kuhutubia ni mahala pake, pengine ingetosha kusema kuwa atasema machache kabla ya kukabidhi.

Wadau, kilichonifanya nije mbio humu jukwaani ni baada ya kusikia dondooo za yale atakayoongea Warioba ambaye siku zote nilikuwa namheshimu kwa kujali maslahi ya taifa ila katika hili, nina hakika hata wadau wengi watamshangaa.
Miongoni mwa atakayosema warioba ni pamoja na haya yafuatayo
Atazungumzia umuhimu wa kura ya Siri kwa wajumbe. Kwamba warioba atatoa maelezo ambayo yana lengo la kuwashawishi wajumbe waunge mkono kura ya Siri. Binafsi sipingi matumizi ya kura hiyo bali hofu yangu ni kuchafuka kwa hali ya hewa. Kama mjuavyo kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Kamati ya Maridhiano ambayo imeundwa na Mwenyekiti wa Muda, mzee Kificho. Pia leo tumepata taarifa kuwa zoezi la kufikia muafaka juu ya namna ya kufanya maamuzi Bungeni linaendelea. Sasa huyu Babu Warioba sijui kitu gani kinamshawishi aende kuzungumza jambo hilo Bungeni?

Jambo jingine ambalo Warioba atazungumza ni kuwaeleza wajumbe juu ya umuhimu wa Serikali Tatu. Warioba anataka kulazimisha wajumbe wote waamini kuwa Tume ilikuwa sahihi kupendekeza mfumo wa serikali tatu. Katika hili, pia sina tatizo bali wasiwasi wangu ni namna ya uwasilishaji wake. Ninaamini kuwa wabunge wana akili timamu na hawahitaji mtu kuwasemea uzuri au ubaya wa muundo wa Serikali Tatu. Je wale wanaopendekeza muundo wa serikali moja, mbili, nne na tano nani atawasemea?

Mtonyaji pia amenidokeza kuwa Warioba atatoa hotuba ndefu ambayo itabeba maudhui ya mtazamo wake juu ya mchakato wa Katiba. Binafsi, namshauri Mzee Warioba aangalie upepo unavyoenda. Kwa sasa si wakati wa kushindana. Maridhiano ni jambo muhimu sana. Mwanzo walioanza nao wabunge ni mzuri. Warioba akabidhi tu na asitumie muda mwingi kama ambavyo amepanga kuwachanganya Watanzania na kupandikiza chuki za kuvurugana.

Ni hayo tu wakuu kwa leo. Siku nikitonywa jambo jingine nitakuja fasta kuwatonya.
Mbona umeandika unajizungusha na kujikanyaga kanyaga?
Utaratibu upo hivyo ni lazma atazungumza,

Hali ya hewa ipi itabadilika?
Serikali 3 ipo kwenye rasimu aliyokabiziwa Jk na ushahidi wa video na maandiko ya watannzania wanaopenda serikali tatu.
Mfano baraza la wawakilishi barua ipo

Tatizo lenu ni nini maccm?
 
Hiv vijana wa ccm kama hugochavez mnakuwaga darasa la ngapi, maana upeo wenu wa kufikiri huwa mdogo sana
 
Last edited by a moderator:
Kwani Kura ya siri inamapungufu gani?Tusifanyane mazuzu.
CCM wanaelewa dhamira ya wabunge wake ni tofauti na mahitaji ya chama.
Wazanzibari hawapo tayari kuupoteza Uzazibari wao kwenye serikali moja kama Wadanganyika tulivoupoteza.
Serikali mbili ndiyo hii iliyotufikisha hapa tulipo (Kero zisizoisha).
Iliyobakia ni serikali Tatu na kundelea.CCM wajiandae kwa mabadiliko hayo.
Hata hivyo M/kiti wao alisha watahadharisha wajiandae Kisaikologia.
 
Mbona umeandika unajizungusha na kujikanyaga kanyaga?
Utaratibu upo hivyo ni lazma atazungumza,

Hali ya hewa ipi itabadilika?
Serikali 3 ipo kwenye rasimu aliyokabiziwa Jk na ushahidi wa video na maandiko ya watannzania wanaopenda serikali tatu.
Mfano baraza la wawakilishi barua ipo

Tatizo lenu ni nini maccm?

Mkuu usikurupuke, Hiyo ndio fasihi andishi.
 
Mkuu, karika hili suala la Katiba, maridhiano ni jambo la msingi. Si kama anavyofanya huyu babu

kipi bora,maridhiano au UKWELI?kwa maoni yangu Ukweli ndio Bora siku zote kuliko maridhiano ambayo kuna upande utakubaliana kwa shingo upande na litakapotokea la kutokea ataanza kulaumu.Halafu tujiulize, kwa nini hili suala lilete mvutano kiasi hicho hadi tufikie kwenye maridhiano?Je kwenye Maridhiano je napo patapatikana muafaka?Usipopatikana nini kitatokea, na nini kifanyike?

Mchakato mzima ulishakosewa tangu mwanzo, na tuliporuhusu wabunge wa Bunge la JMT na Wawakilishi kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba hapo ndipo tumeruhusu mvua ya magoli katika mchakato huu!
 
Mkuu, karika hili suala la Katiba, maridhiano ni jambo la msingi. Si kama anavyofanya huyu babu

Tatizo lake babu liko wapi? Yeye atawakilisha mawazo ya wananchi ambayo ccm wanataka kuyapotosha hata kumuona mzee WARIOBA hafai. Tatizo la serikari ya ccm haiutaki ukweli na kamwe hawataweza kusema ukweli mpaka walazimishwe.
 
Warioba wa ajabu sana pale wilayani kwetu bariad wamehoji kata si zaidi ya tano halafu anasema watanzania wengi wametoa maoni yao sijui kayatoa wapi.
 
warioba anazeeka vibaya kama slaa
 
Tatizo lake babu liko wapi? Yeye atawakilisha mawazo ya wananchi ambayo ccm wanataka kuyapotosha hata kumuona mzee WARIOBA hafai. Tatizo la serikari ya ccm haiutaki ukweli na kamwe hawataweza kusema ukweli mpaka walazimishwe.
Nini kinachotaka kupotoshwa kwa maoni yako wewe pengine unazungumza vitu bila kuwa na uhakika wenye uthibitisho wa kutosha.
 
Back
Top Bottom