mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,151
Katika kipindi cha dakika 45 jana cha ITV Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba amewaomba wananchi hasa katika mabaraza ya katiba watoe maoni mapya ya kuboresha kile kilichopo tayari na wasirudie maoni ambayo tayari yameshatolewa kwa tume na yenyewe kuyatolea mapendekezo kwa sababu hilo litakuwa kama kuanza upya. Mfano hakuna sababu watu kuja tena na mapendekezo ya Muungano kwa sababu watu wameshatoa maoni yamechambuliwa na tume imetoa mapendekezo. Lakini nionavyo ni kama CCM wanajiandaa kutoa mapendekezo mapay kwa kutumia wanachama wake ili kuilazimisha tume kufuata mapendekezo yao. Itakumbukwa kuwa mapendekezo mengi ya CCM hayajakubaliwa na mengi ya upinzani, wananharakati na wasomi ndio yaliyochukuliwa kwa wingi. Je CCM inataka kudhibithi sehemu ilyobaki ya mchakato wa katiba? Lengo lao nio nini? Na je Jaji Warioba yupo sahihi au la?