Warioba: Please usijaribu kuchakachua maoni ya Watanzania

Warioba: Please usijaribu kuchakachua maoni ya Watanzania

politiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2010
Posts
2,376
Reaction score
1,508
Kitendo cha mwenyekiti wa Tume ya kuratibu maoni ya katiba joseph warioba kuwapiga marufuku waandishi wa habari na vikundi mbalimbali vya kijamii kuchukua details kuhusu maoni ya wananchi na pia kauli yake ya kumuunga mkono Rais jk kuwa anayo haki kutoa muongozo kwa niaba ya tume kinatia shaka kuwa warioba huenda akawa anatumiwa au anaruhusu kutumiwa na wahusika kwa ajili ya msalahi yao ya kisiasa.

Wasiwasi wa warioba ni nini mpaka kupiga maarufuku media, mtu mwenye kitu cha kuficha au asiyependa uwazi ndiyo
siku zote hapendi media iripoti kila anachokifanya kwani maoni yanatolewa wazi sasa kuna nini cha kuficha??
freedom of information ni kitu kinaliliwa sana nchi hii kwani kinazibiti usiri which can lead to abuse of power.

Ninavyohisi mimi ni kwamba wasiwasi wa warioba huenda unatokana na kitendo cha CUF zanzibar kuweza kufuatilia mikutano yote ya tume na kuweza kujua ni idadi gani ya watu imetoa maoni ya aina gani na ya kuyaweka kwy kumbukumbu zao something which should have been done by every watch dog groups from the beginning. kutokana
na haya anayoyafanya warioba kutaka kuingiza usiri kwy hii process basi kuna haja kutumia ule usemi wa rais Reagan
wa Trust but verify kuanzia sasa ili angalau wajue kuwa somebody somewhere is watching them wasije wakatu surprise
hawa watu kwani sababu mojawapo ya watu kutaka hayo mabadiliko ya katiba ni kuachana na mfumo unaoendekeza kuendesha mambo ya kwa usiri.
 
Utafikiri hiyo katiba ni mali yake mwenyewe ndio maana haka kababu kana anguka anguka ovyo kwa roho mbaya
 
mimi sina imani na serikali ya magamaba na takataka wao wote..
 
Sina imani na serikali ya awamu ya nne
 
Hapa naona wanataka watufanyie surprise ktk kutoa matoke,mbona huwa wanaingia gharama kutangaza mikutano ya vyama sembuse hili linalogusa hatima ya maisha ya mtu?.Kuna kitu hakipo sawa.
 
Warioba umekuwa unawafikia viongozi wote walio stafu ili kupata maoni yao juu ya katiba mpya ,tunacho kukumbusha na kukusisitiza tume yako isije ikajifanya hamnazo na kujifanyakumsahau Aliyekuwa Rais wa Zanziba Mzee Aboud Jumbe kwa kutumia visingizio visivyokuwa vya ukweli ,Mzee Aboud jumbe akili yake ni timamu na mawazo yake ni muhimu sana katka mchakato huu wa katiba ,mchango wake ni huhimu zaidi kuliko hata baadhi ya viongozi wengine mliofika kuwahoji
Mnyonge mnyogeni lakini haki yake mpeni (Bila ya Mzee Aboud pasingekuwapo na CCM)
 
Vipi kuhusu komando?(Salmin)naskia amewehuka,ila pia si mbaya kama watapata maoni yake,
 
Chonde chonde Warioba historia itaandikwa KATIBA niya watanzania. Usichakachue maoni kwa masilahi ya waliokuteua.!
 
Tusubiri Katiba ya ajabu itakayowafeva wakoloni weusi, itakayoendeleza utumwa ndani ya nchi, KATIBA MBUFU MBOFU mnadhani Wakoloni weusi wameurahia hii mambo eti ya katiba mpya? MASIKINI TUTASUBIRI SANA huenda katiba yenyewe imeshaandikwa inasubiri tu kuletwa mbele ya halaiki.
 
Back
Top Bottom