Mchanganuo wa takwimu hizi unaonyesha kuwa kwa upande waTanzania Bara, 13% walipendelea Serikali moja, 24% walipendekeza Serikali mbili na 61% walipendekeza Serikali tatu. Kwa upande wa Zanzibar, 34% walipendekeza Serikali mbili na 60% walipendekeza Muungano wa Mkataba, na 0.1% (watu 25) walipendekeza Serikali moja. Aidha, taasisi nyingi kama vile vyama vya siasa, asasi za kiraia na jumuia za kidini zil ipendekeza muundo wa Serikali tatu. Baadhi ya taasisi za kiserikali, ama moja kwa moja au kwa tafsiri ya mapendekezo yao, pia zilipendekeza Serikali tatu. Kwa mfano, Baraza la Wawakilishi Zanzibar lilipendekeza kuwe po kwa mamlaka huru ya Zanzibar, mamlaka huru ya Tanganyika na mamlaka ya Muungano na iwekwe wazi maeneo, uwezo, nguvu, utendaji na mipaka ya kila mamlaka. Ofisi ya Waziri Mkuu imependekeza mfumo wa serikali tatu ili kuondoa kero za muungano. Aidha, Mamlaka ya Mapato Tanzania imependekeza kuwepo kwa Serikali tatu ili kutoa majibu ya kero zilizopo na kuleta utulivu zaidi ilimradi upangiliwe vizuri.
http://katiba.go.tz/attachments/article/186/HOTUBA YA MWENYEKITI 30 DISEMBA, (PDF).pdf (pg13)
http://katiba.go.tz/attachments/article/186/HOTUBA YA MWENYEKITI 30 DISEMBA, (PDF).pdf (pg13)